Mwakyembe ndani ya kanisa la Gwajima; ashukuru kwa maombi akiri kulishwa sumu!

Mimi binafsi naamini Richmond yalikuwa makosa ya kiutendaji ya serikali na siyo UFISADI wa aina yoyote ile, kwsababu tumemambiwa na hawa hawa wakina Mwakyembe kwamba hakuna hata senti tano iliyolipwa Richmond na Serikali. Kwenye hili simlaumu Kikwete, Lowassa, Mwakyembe, Msabaha na hata yeyote mwingine aliyoshiriki mchakato, UDHARURA ulikuwa wa ukweli, ingawa siku hizi tumeshazoea migao ya umeme kwahiyo nahisi hamna udharura tena. Lakini basi naomba tuache huo UPOTOSHAJI wa Ths 156M kila siku - NI UONGO WA KUFA MTU, tutafute hoja nyingine kama tunadhani upotoshaji huu unatusaidia wenine kisiasa.

Cha msingi kinachonisikitisha, tunataka kujengewa mazingira kwamba Richmond ndiyo ituamulie siasa zetu kila siiku. Tangu mwaka 2008 hili jambo linajengewa mazingira ya kutoisha kwenye jamii, iwe kupitia zile kesi mahakamani mabazo zote zimeisha na hao Richmond wametushinda serikali au iwe kupitia zile kesi za Dowans kule ICC na sasa inakuja hii ya sumu. Hivi kwanini hao watu wa Richmond wampe Mwakyembe sumu leo, miaka minne baadaye, na tena baada ya kushinda kesi zote mahakamani. Mimi sipati majibu hata kidogo.

Watu wengi humu ndani ya JF mnfahamu vizuri credibility ya Dk Mwakyembe, siyo vyema kumsema mtu vibaya akiwa kwenye hali ile kiafya, lakini naamini Mungu mkubwa, atamponya vizuri kabisa. Bwana yesu Asifiwe, Ameen. Lakini huyu Dk Mwakyembe ndiyo ambaye aliandika barua ya ukurasa sijui kumi kwenda kwa IGP na kutoa vielelezo vya namba za magari ya polisi na ya serikali yaliyokuwa yakitumika kwenda kwa waganga ili kumloga na afe na hapo pia alimtuhumu Sheikh Yahya kuhusika kwa kiasi kikubwa. Uchunguzi wa haraka ikathibitka kwamba yale magari hata polisi wenyewe hayapo tena na magari mengine yalikuwa kama ya Mzee Paul Kimiti amabye alsikitishwa sana kuhusishwa na upuuzi ule. Ripoti ya polisi iliandikwa ili kulinda heshima ya serikali kwababu ni naibu Waziri, lakini mwisho wake ilikuwa ni aibu.

hii habari ya sumu leo iansikitisha sana, habari zilizoko kwenye familia yake ni tofauti kabisa na kuna ugomvi mkubwa ndani ya familia ambayo wameanza kutuhumiana vibaya, lakini cha kushangaza zaidi ukija kwenye data za serikali na mdakatari wake waliomsaidia, wanasema hii ni RARE GENETIC DISEASE ambayo inaelekea kwenye CANCER ya damu, lakini mwenye mamlaka ya kuhabarisha umma ni Mwakyembe mwenyewe, na ametuambia ni sumu. Yetu macho, movie ya Richmond Part 2 inaendelea.. Inasikitisha sana.

Hivi wale waliokuwa wamejipanga kanisani KAWE, hivi kwenye mambo ya msingi kama haya ya Mgomo wa Madakatari, mbona hatusikii juhudi zao? au hizi hazina umaarufu? au wakiitukana serikali wanajua watavuliwa uwaziri na ulaji utapotea? Hii nchi inahitaji maombi mengi sana, hamna mtu anataka kujadili mambo muhimu ya nchi.
 
wafu wanakokotana
Wanabodi, kwenye siasa, hakuna rafiki wa kudumu, wala adui wa kudumu, kuna just common interest.
Japo katika bandiko hili, nilitofautiana na Gwajima, lakini kufuatia kwa sasa ni mimi ni kada, na mgombea aliyepitishwa na chama chetu kwa jimbo la Kawe ni Gwajima, naomba kudeclare kuwa sasa namuunga mkono Gwajima 100% kwa 100% nikalikomboe jimbo, tulirejeshe CCM!.
Mimi na Gwaji Boy...dam dam!.
P
 
Back
Top Bottom