leo katika mikutano miwili iliyofanyika jimboni kwake Mhe Mwakyembe amewaliza watu baada ya kuamua kuvua kofia yake na gloves na miwani waone jinsi alivyoathiliwa na sumu kali. Katika hotuba yake ametumia muda kuwasihi wananchi kuacha majungu badala yake wamuunge mkono ili amalizie kipindi chake cha uongozi. Hata hivyo hakutaja watu waliomdhuru lakini aliwashukuru wananchi kwa maombi yao na madaktari kwa juhudi zao katika kuokoa uhai wake.
Teacher1,
Mbona Mwakyembe hakuongelea kabisa mambo ya kuathiriwa na sumu? Kasema ni ugonjwa tu na anakunywa vidonge 25 kwa siku.
Pia kasema hata Sitta alikuwa na haki kusema aliyosema kwani ilikuwa ni hisia zake kwa jinsi alivyomwona Mwakyembe akiumwa. Anasema itakuwa makosa serikali kumshitaki Sitta maana alisema alichokuwa anahisi.
Anasema 2015 atakuja kuwaambia kama anagombea au hagombei. Ila wananchi wamchague anayeweza mapambano kama yeye maana huko kuna mapambano makubwa kama wanavyo mwona yeye alivyosasa, hayo ni matokeo ya mapambano.
Pia aliwaambia wananchi wampokee tu Lowassa akija kuchangisha pesa kwenye kanisa. kwamba ni kiongozi mwenzake na yeye Mwakyembe atakuwepo pia kwenye hiyo harambee ya Lowassa.
Mengine aliongelea barabara ya Kikusya mpaka Matema kwamba mchakato umekamilika na itajengwa kwa kiwango cha lami mpaka matema.
Pia aliwashukuru wananchi kwa maombi yao ambayo yamesaidia kumponya.
Hakukubali maswali maana wananchi walitaka kumuuliza hasa hilo la sumu au sio sumu.
Baada ya mkutano wananchi kwenye makundi gumzo lilikuwa imekuwaje ghafla kageuka mpiga debe wa Lowassa wakati kwa miaka kama minne sasa kila akiwa Kyela ilikuwa ni kumtukana Lowassa?
kwa kifupi ni hayo, wengine waongezee waliyoyasikia.