figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,058
- 64,206
Na Mwandishi Wetu,
Namtumbo: Njama zilizokuwa zimepangwa na mmoja wa watia nia wa ubunge Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma kuzuia makabidhiano ya gari jipya la wagonjwa (ambulance), zimekwama.
Taarifa zinadai kwamba mtia nia huyo, Juma Zuberi Homera, aliwaandaa vijana kadhaa ili wafanye fujo kuzuia hafla iliyofanyika Kata ya Magazini, Namtumbo mkoani Ruvuma, Jumanne ya Aprili 22, 2025.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, mkazi mmoja wa Magazini aliyehudhuria hafla hiyo, alisema gari hilo lililotolewa na serikali lilikabidhiwa kwa wananchi na Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa.
“Maombi ya mara kwa mara ya Mbunge kwa serikali kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wakazi wa maeneo ya vijijini waliokuwa na changamoto ya usafiri wa dharura, yamezaa matunda.
“Kitu cha ajabu ni kwamba wapo watu ambao hawakufurahia jambo hili, wakapanga kuzuia kufanyika kwa hafla kutokana tu na tamaa zao,” alisema.
Kata ya Magazini ipo umbali wa kilomita 254 kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Namtumbo.
Taarifa zinathibitisha kuwa jitihada za kushangaza na za hovyo za kuzuia haflahiyo ziliratibiwa na Juma Zuberi Homera; kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
“Nia yake ni kuharibu taswira nzuri ya jambo hilo kubwa kwa wananchi wa Magazini ambao wamekua wakipata shida wanapohitaji usafiri wa dharura kwenda hospitali,” alisema mwananchi mwingine.
Njama hizo zinabainisha kwamba kulikuwapo kundi la vijana waliopangwa kufanya vurugu, kurusha mawe na kuharibu utaratibu mzima.
Pia vijana hao walipangwa kuandaa mabango ya kukashifu hafla sambamba na juhudi za Mbunge (Kawawa) ambaye amekuwa akiwapigania wananchi bungeni akiiomba serikali kujenga vituo vya afya na magari ya wagonjwa jimboni kwake.
Hata hivyo, makabidhiano yalifanyika na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali walioungana na wananchi waliojaa bashasha na shukrani tele kwa Mbunge wao.
Gari hilo limetolewa na Serikali baada ya maombi ya Mbunge ikiwa ni ishara wazi ya juhudi za serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwajali wananchi wa Kata ya Magazini.
Ni Rais ndiye aliyemtuma Mheshimiwa Kawawa kukabidhi gari hilo kwa niaba ya Serikali.
“Njama zozote za kuzorotesha shughuli hii ni za hovyo na zinazopaswa kukemewa. Inasikitisha hasa njama hizo zinaporatibiwa na kada wa CCM. Hizi ni siasa chafu na ni jambo la aibu linalopaswa kukemewa,” alisema kiongozi mmoja wakati wa hafla hiyo.
Huu ni mwendelezo wa kampeni chafu zinazoendeshwa na Juma Zuberi Homera; Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anayeutaka ubunge wa Jimbo la Namtumbo kwa kila hali.
Inadaiwa kuwa tayari ameshatumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kampeni hata kabla muda wa kampeni kuzinduliwa.
Kwa sababu ya kukosa ushawishi miongoni wa wapiga kura, Homera ameamua kutumia mbinu za kuzorotesha kazi za Mbunge aliyeepo madarakani ili kumtisha na kumpunguzia ari ya kuwatumikia wananchi wake.
Rushwa nje nje!
Kwa upande mwingine, Homera anadaiwa kutumia nguvu ya fedha kuwashawishi wanachama wa CCM watakaoshiriki kupiga kura za maoni ili wamchague.
Aprili 13, 2025, Diwani wa Lisimonji, Bakili Mawila, akiambatana na Katibu wa Tawi la Matepwende na Mwenyekiti wa Kijiji cha Matepwende, walifanya kikao cha Halmashauri Kuu ya Tawi la Matepwende.
Kikao hicho kilihudhuriwa na mabalozi na wajumbe kadhaa wa shina.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao zinasema kwamba wakati mkutano unaedendelea, mjumbe anayeaminika kuwa mpambe wa Homera, alimpigia simu kwa hoja kwamba anataka kuwasalimia.
“Hazikuwa salamu za kawaida kwa kuwa Ndugu Juma Zuberi Homera alitumia fursa hiyo kujinadi kwa wajumbe,” alisema mmoja wa wajumbe na kumsikilizisha mwandishi wa habari hii sauti ya Homera iliyorekodiwa kwa simu.
Katika sauti hiyo, Homera anasikika akisema kuwa amewawezesha wajumbe hao ‘kutembea kilomita 10,000’.
Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba kila mjumbe aliyehudhuria alipewa posho ya Sh 10,000 kutoka kwa Homera.
Katika sauti iliyorekodiwa, Homera anasikika akiuliza idadi ya wajumbe na kujibiwa kwamba walikuwa 244.
“Ninawashukuru sana. Kwa sasa nipo kwenye ziara Mbarali. Ninawaahidi kuwa nitakuja kuchukua fomu (za kugombea ubunge) ili tushirikiane kuijenga wilaya yetu,” alisikika Homera akisema.
Inadaiwa kuwa Homera amekuwa akikusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara wa Mbeya kwa ajili ya kampeni za Namtumbo.
“Yaani kila Mkuu wa Mkoa anataka ubunge; maDC nao wanataka pamoa na maDED pia. Sasa sijui kwenye maeneo yao nani atasimamia siasa wakati wa uchaguzi?” alihoji mwananchi mmoja
Anguko la Wilaya ya Namtumbo
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba aina ya mgombea kama Homera ni hatari kwa maendeleo ya jimbo lolote nchini.
“Homera anatumia gharama kubwa sana kuwahonga wajumbe na kuwarubuni ili wamwamini kuwa ni kiongozi anayewajali, sasa gharama hizoatazirejeshaje?” alihoji mchambuzi mmoja
Alitoa mfano wa kugawa Sh 10,000 kwa baadhi ya wajumbe akihoji: “Mtu anataka ubunge anatoa Sh 10,000?
Yaani ubunge wa miaka mitano anaununua kwa Sh 10,000; maana yake ni Sh 2,000 kwa mwaka mmoja?
“Fedha hizi tujiulize anazitoa wapi? Mbona hana uchungu nazo!
Wananchi wa Namtumbo hawahitaji mtu anayejali maslahi binafsi, wanahitaji mtu anayejali maslahi ya wananchi wote kwa kuhakikisha anasimamia vema miradi ya maendeleo.”
Alisema kwa mwendo wa kugawa fedha kata hadi kata, Homera anaelekea kuliangamiza Jimbo la Namtumbo.
Hata hivyo, fedha anazozigawa kwenye vikao kwa njia ya simu ilhali yeye hayupo eneo la tukio zinawanufaisha mabalozi na viongozi wa matawi na kata na si wananchi wote.
Mchambuzi huyo alitoa wito kwa taasisi husika hasa TAKUKURU kumchunguza Homera kufahamu ni biashara gani anayoifanya Mbeya na kumuingizia fedha nyingi kiasi hiki.
Mmoja wa wapambe wake aliyejitambulisha kama Mwalimu Homera alisikika akiwaeleza wajumbe kwa mbwembwe na kutamba kuwa tayari Dk. Homera ameshamwandikia Rais kuwa hatoendelea tena na ukuu wa mkoa.
“Hakuna mtu wa kumkata. Jina lake lazima litarudi, hakuna mwenye ujanja wa kumkata,” alisema Mwalimu Homera kuonyesha jinsi mtia nia alivyojipanga kutumia fedha kila ngazi kuhakikisha anapata ubunge.

Last edited: