Mwakyembe awaliza watu wa Kyela

Teacher1

JF-Expert Member
Jan 29, 2011
333
149
leo katika mikutano miwili iliyofanyika jimboni kwake Mhe Mwakyembe amewaliza watu baada ya kuamua kuvua kofia yake na gloves na miwani waone jinsi alivyoathiliwa na sumu kali. Katika hotuba yake ametumia muda kuwasihi wananchi kuacha majungu badala yake wamuunge mkono ili amalizie kipindi chake cha uongozi. Hata hivyo hakutaja watu waliomdhuru lakini aliwashukuru wananchi kwa maombi yao na madaktari kwa juhudi zao katika kuokoa uhai wake.
 
Mwakyembe hajaathirika na sumu. Hebu acheni majungu. Nashangaa sana mheshimiwa waziri anatembelea Kyela kisiasa wakati ana kazi ofisini, kwani yupo leave?
 
Starehe garama ndugu
alifikiri wajinga kumpa vx na unaibu waziri...hata ningeishia la saba na vita yote hata siskumoja nisingetarajia kuikubali post serikalini
 
leo katika mikutano miwili iliyofanyika jimboni kwake Mhe Mwakyembe amewaliza watu baada ya kuamua kuvua kofia yake na gloves na miwani waone jinsi alivyoathiliwa na sumu kali. Katika hotuba yake ametumia muda kuwasihi wananchi kuacha majungu badala yake wamuunge mkono ili amalizie kipindi chake cha uongozi. Hata hivyo hakutaja watu waliomdhuru lakini aliwashukuru wananchi kwa maombi yao na madaktari kwa juhudi zao katika kuokoa uhai wake.

Mwongo wewe
 
Mwakyembe hajaathirika na sumu. Hebu acheni majungu. Nashangaa sana mheshimiwa waziri anatembelea Kyela kisiasa wakati ana kazi ofisini, kwani yupo leave?
Utashangaa sana!
Ukitaka kushangaa zaidi na kuacha mdomo wazi hadi inzi wajae mdomoni, nenda Arumeru, utakuta Mawaziri kibao wako huko kwa mwezi mzima na walishaweka makufuli maofisini kwao!
 
Utashangaa sana!
Ukitaka kushangaa zaidi na kuacha mdomo wazi hadi inzi wajae mdomoni, nenda Arumeru, utakuta Mawaziri kibao wako huko kwa mwezi mzima na walishaweka makufuli maofisini kwao!
Hila inabidi aache uzushi na yeye na kutafuta cheap publicity, tunasikia kapitia chemotherapy huko India, nadhani unaelewa effects zake temporarily if you dont ndio hizo ( na in most cases cancer is involved). Sasa aseme what is wrong with him or who poisoned him and for what? (afadhali hata Faiza Fox, alituonya mdomo wake na kesi ya visima anaweza na yeye akapewa discipline).

Tumechoka na hawa wanasiasa wazushi wanaotumia ignorance ya society kutatua vita yao huko CCM.
 
Kitendo cha kusema kuwa watu wasimjadili kilikuwa ni sawa na kujipiga risasi ya kichwa kwenye public sympathy. I was very concerned with his health lakini kwa kuwa ameamua ku-compromise ukweli kuhusu kilichompata ili aendelee kuwa waziri basi sidhani kama anawatendea watu haki kwa kuwavulia kofia na gloves. Inatakiwa ugonjwa wake sasa uwe private maana aliisha ikana public support yeye mwenyewe.
 
sasa kwa hali yake ilivo anaweza tena kuendelea vizuri na kazi za uwaziri?? kwa nini asiwe mzalendo akaachia hiyo nafasi ili apate muda waa kupumzika na kucheki zaidi afya yake!!yaani wapiga kura wake wanamwona huruma na kutaka kujua kilichompata mbunge wao yeye anasema waache majungu??acha afe na kamba shingoni!!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom