Mwakyembe amshushua Tundu Lissu...

Mwakyembe amshushua Tundu Lissu...

Mnafiki tu yule hana lolote.Msomi gani unatumwa kuchunguza jambo halafu ukija unatoa taarifa nusu na nyingine kuzificha eti kumwokoa JK asiporomoke. Wasomi ni akina Warioba, Nyalali na Robert Kisanga ambao wao waliita koleo ni koleo na sio kijiko kama alivyofanya yeye kwenye richmond mnafiki mkubwa

Njaa tu, hakuna jibu lingine.. hata kuficha ilikuwa ni kama hongo kwa JK ili amkumbuke maisha.
 
Kwa mara ya kwanza kusikia akichangia bunge la katiba leo asubuhi nimejifunza mambo makuu yafuatayo.

1.Mwalimu hawawezi kukufundisha kila kitu anachokijua kwa kuwa anajua ukijua kila kitu unaweza kumzidi. Ukisikiliza namna alivyochangia utagundua kuwa Tundu Lissu alisoma vijarida tu vya sheria pale Mlimani badala ya kusoma vitabu vya sheria.
Namnukuu dr mwakyembe akihoji kitabu chake kutumiwa vibaya na tundu lissu "Mh mwenyekiti huwezi ukakisoma kitabu hiki kwa haraka haraka ukakielewa kama unavyosoma gazeti la Tanzania Daima"

2. Tundu lisu anaweza kunyanganywa degree yake wakati wowote. Akichangia leo amewataka waalimu waliomfundisha Tundu lisu kuanza kufikiria namna ya kumnyanganya tundu lisu degree yake hii ya mlimani kwani anakitia chuo hiki AIBU.

3.Maalimu Seifu hata siku moja hawezi akadai serikali tatu na ndio maana hakubaliani na wana UKAWA kuhusu serikali tatu ila yeye kasimamia kwenye hoja ya serikali ya mkataba sababu ni hii:- Akichangia leo dr mwakyembe alinukuu baadhi ya maneno ya maalimu seifu aliyowahi kuyasema na nukuu "Mh mwenyekiti unapokuwa kiongozi unatakiwa usimamie maneno yako naoma nimnukuu mh maalimu sefu maneno yake aliyokwisha kuyatoa bungeni kwamba nanukuu hatuwezi kuuvunja muungano wa tanganyika na zanzibar kwani kufanya hivyo umewarahisishia wale tuliowafukuza njia ya kurudi. Adui yao mkubwa na kikwazo kikubwa cha wao kutorudi ni muungano huu" . Katika hoja yake maalimu seifu alitahadharisha pia kuwa si kwamba muungano hauna dosari ila ni vizuri kuzitatua dosari hizo kuliko kuuvunja muungano.

4. Tundu Lisu ni MJINGA kabisa na anatakiwa arudi darasani kujifunza tena upya na ikiwezekana abadilishe fani kabisa SHERIA imemkataa.Katika uchangiaji wake dr mwakyembe alihoji kuwa hata mwananchuo wa mwaka wa kwanza anajua kuwa kama umedumu na muungano huu kwa miaka 50 na hujauhoji leo huwezi kuhoji sain au makataba wake kwani kwa muda ambao umedumu nao ni kwamba umeshaubariki kuna neno la kisheria alilitumia hapa.

5. Kuna hatari ya maproffesor na ma dk kukataa Tundu lisu asiwa wanukuu maandiko yao kutokana na kuyapotosha nafikiri hili linaruhusiwa. Atabaki kunukuu vitabu vya shigongo vya mapenzi na vya nyambari nyangwine.

LABDA MIMI NIULIZE SWALI TU: Ukawa (Including Tundu Lisu) wamesusia Bunge maalum la katiba, akina Mwakyembe na wengine wamebaki bungeni. KWANINI AJENDA YAO KUBWA NI TUNDU LISU ? Kwanini hawajadili rasimu ya katiba? Maana siku zinaisha, tunasikia tu kuhusu Tundu Lisu, Tundu Lisu, Tundu Lisu, Lipumba,Jusa, na vijembe kibao.

Ukumbuke pia waliorejea maandiko ya Mwakyembe SIO Tundu Lisu peke yake. Tunafuatilia pia maendeleo ya bunge hilo; mfano mdogo tu, Mbatia alirejea maandiko ya Mwakyembe, Mbona hawamjadili Mbatia ? Ukumbuke pia Mwakyembe hakupanua mdomo wa kutoa hoja wakati hao akina Tundu Lisu wakiwa bado Bungeni, unadhani alihofia nini ? Labda unataka pia tuamini kuwa wajumbe woooote waliobaki bungeni wana mawazo yanayofanana ? maana HAKUNA ANAYEPINGANA NA MWINGINE. Pamoja na yote, ebu ifike wakati sasa wabunge waliobaki wajadili sura za rasimu ya katiba. Sisi watazamaji tunaamini kuwa kumtaja taja mtu kila saa na kila siku ni kumjengea umaarufu wa bila sababu. Ukiamka tu TUNDU LISU, kabla ya chai TUNDU LISU, wakati wa chakula cha mchana, TUNDU LISU, wakati wa chakula cha jioni, TUNDU LISU, kabla hujalala, TUNDU LISU, ukilala na kwenyewe unaota TUNDU LISU, Hiyo ni dalili mbaya sana.
 
Huyu ni Dr Mwakyembe ni wa kwenye vitabu tu hamna kitu hapo. Dr wa Neuro surgery tunategemea kwamba atakuwa alikwasha wafanyia wagonjwa kadhaa neuro surgery na kupona. Dr wa sheria tutnategemea atakuwa ameshasimama mahakamani na kushinda kesi, au kutoa msaada wa kisheria kwa watu mbalimbali. TL has a track records ya kushinda kesi nyingi mahakamani. Huyu Dr. Mwakyembe hata hana record moja ya kushinda kesi mahakamani hata ya wizi wa kuku. Kesi ya Richmond aliyoisimamia kwa mbwembwe bungeni tumebwagwa (serikali) chini ICT. Sasa anawezaje kujilinganisha na Lissu anaye practice sheria. Eti utetezi wake ni kwamba alichoandia katika Thesis yake ni kigumu kueleweka SIC! Watu tunasoma nuclear physics na bado tunaelewa, ije hiyo DS aliyoandika kwenye thesis yake ndiyo tushindwe kuelewa! Poor Mwakyembe. TL pia amewahi kupewa MSC ya heshima katika chuo kimoja USA kwa mchango wako aliuotoa kwenye tasnia ya sheria. Atwambie yeye Mwakyembe zaidi ya UDSM wapi anapotambulika academically?
 
hata uwe msomi kiasi gani ukishaingia ccm lazima uwe panya na akili kama Lusinde
 
Tatizo lililopo humu kama mtu yeyote akitoa mada ambayo haita gusu malengo yetu,hata kama hiyo mada inaukweli nilazima tubishane nayo,kaazi kweli kweli,
 
Mwakyembe ni mnafiki mkubwa na mwenye uchu wa madaraka. Huyu ndiye alitumwa kuchunguza Richmond alipotoa taarifa akaficha baadhi ya mambo eti kwa kisingizio cha kuepusha kuanguka serikali yote na kisha kuamua kumbebesha mzigo wote Lowassa. Haifai kabisa huyu amejaa tamaa na kujiona yeye ndiye mjuaji kabisa. Huyu ni msomi ambaye hajaelemika katumwa akatafute ukweli baada ya kuupata kauficha na kuleta ukweli nusu ambao huwa ni nusu ya uongo. Mnafiki mwenzake mwingine ni Samweli Sitta aliyeimaliza hoja ya Richmond kihuni wakati huo akiwa spika na baada ya hapo naye akajifanya ni msafi anapinga ufisadi. SHAME ON THEM!



Yani tokea aseme maneno hyo pale bungeni. Nimetokea kuto mkubali kabisa mwakyembe.na muona nimnafiki tu
 
babu mwakyembe duuuhhhhhh.......unajikana mwenyewe kuwa wewe c mwakyembe bali ni mawenge pole mzee
 
Hoja inayohusu wasomi yenye content ya kisomi [sheria] hujadiliwa kisomi. Hoja yako umeileta kimipasho zaidi nakudhihirisha kuwa huna tofauti na wabunge wengi wa chama tawala ambao ni vihiyo. Don't be biased bhana, always discuss the facts.

Baada ya kusema hayo yote hawakupiga makofi??
 
Wana jf hapa hawawezi kuchangia wanapenda mambo ya uongo uongo mwakyembe kafafanua vzur kwel mnajfanya mmekufa

Mkuu upo sahihi kabisa hata maoni Mengi ya humu yamekaa kiunafikinafiki tu na kama yangetendewa kazi basi Tanzania isingekuwepo leo, Nashukuru mtabaki kuandika mawazo yenu ya kinafiki ila hakutakuwa na utelezaji wala kuisisimua jamii
 
mi namshuri Mwakyembe hakae kimya asiendelee kujizalilisha mbele ya umma ccm wote sasa hawazungumzii katiba bali lissu na ukawa
 
mi namshuri Mwakyembe hakae kimya asiendelee kujizalilisha mbele ya umma ccm wote sasa hawazungumzii katiba bali lissu na ukawa

Ccm wote hawana jipya zaidi kukusanyana na kukung'ng'ania serikali 3 tusitegemee mabadiliko kutoka ccm zaidi ya sisi wananchi wenyewe kuamua tunatakaje!!
 
Naamini Lissu ni hatari jwa wezi na waongo!!!
Sasa Mwakyembe anataka aseme maneno yale aliandikiwa na mtu na si yake?
Au Lissu alijitungia?

Nadhani Mh. Dr Mwakyembe aachane na siasa hizi za uchafu alinde heshima yake ambayo katika ccm kidogo bado tunamwona ni mtu wa maana. Akiendeleza ubishi usio na hoja kama huu, ataishusha heshima aliyonayo.

Lissu, endelea kamanda. Wewe ni jasiri maana watu kibao wameiomba hi hati hawajaoneshwa, ila Mnyika alipolianzisha umetufundisha mengi ambayo hayamo kwenye vitabu shuleni, mwishoni wakathubutu kuleta walau fake!!!
 
Hakuna mtu anaeweza kuwa katikati,lzm uwe na upande

kwa mara nyingine mwakyembe ameingia kwenye mfuko wa kikwete km walivyofanywa kina lukuvi
poor mwakyembe baada ya unafki wako nitakuzadharau daima.
Ulibakia manyoya sasa,unarud ndan ya mifuko ya maadai zako
 
Nimeandika siku zote kwamba kwasababu vijana mnadanganyika kirahisi imekua rahisi matapeli wa kisiasa walioko CCM kuwaghiribu kwamba wao ni tofauti na makambale yaliyo jazana huko na nyie mkawaona wasaka tonge aina Mwakyembe na Magufuli ni mashujaa zenu!! Mtasubiri sana kama hamtastukia deal za watu!
 
Leo nikiwa kijijini kwetu hapa Ipinda -kyela nimesikia kupitia kituo cha redio Ebony fm. kuhusu mchango wako juu ya rasimu ya katiba ukimlaumu T.lisu kuwa ni mtoto mdogo sana kwenye mambo ya sheria na kuwa amesoma mstari mmoja tu ndo kakomaa nao kukunukuu Tulivyo muelewa Lisu ijenga hoja nzito zilizobeba utetezi wa s3 kuliko ulichosema wewe Jana kama mpiga kura wako nimegundua umetoa hoja dhaifu na hukueleweka ukilinganisha na alivyo nukuu Lisu, vile vile hata hiyo speech yako ya Jana ukiambiwa uirudie hutaiweza maana ulikuwa ukibabaika na kukosa confidence tofauti na nikujuavyo na hata tukiwapima kwenye mizani Lisu anonyesha yuko juu ktk ku-refer vifungu kuliko ww, nijuavyo Mimi wewe Mwakyembe ni type za akina Warioba na Ramadhan ni aheli ungekaa kimya kuliko kutoa utetezi dhaifu kiasi kile na kwa hilo umempaisha sana Lisu tofauti na ulivyo dhani mbona kwenye mambo ya msingi unakuwa strong imekuaje leo? angalia usiwe kama nyuki ang'ang'anie kupita kwenye dirisha la kioo akiamini liko wazi kumbe ni mwanga tu mwisho hufia hapo.
 
Back
Top Bottom