Sasa hapo waziri Kamani anataka kutueleza nini?
Ni kama vile, anapingana na uamuzi wa waziri mwenzie.
Inaelekea Kamani anataka uendelezwe mfumo ule ule, wa wafanyakazi wa serikali kuendelea kuboronga na kuendelea kulindwa, ukiona mfanyakazi wa serikali kawajibishwa sana, basi atahamishwa kituo cha kazi, ili akaendeleze hayo madudu katika kituo chake kipya.
Kama kweli mmoja wa wafanyakazi waliotimuliwa kazi na Mwakyembe, alishastaafu kazi, basi inawezekana wakubwa wa wizara ya kilimo, hawakutaka kumwondoa kwenye payroll, ili waendelee 'kufaidi' mishahara ya mstaafu huyo!!

Hii ndiyo tanzania!yaani hakuna serikali kabisa
Duh! huku sasa kuumbuana.kwa nini waziri kamani asimtafute kwanzan Dr. Mwakyembe ili waweke sawa records zao kabla ya kuruka hewani?
Kwa hiyo hao jamaa kwenye CCTV wanaoonekana wanachukua mpango angewaacha tu, au sivyo!
Waziri Titus kamani amesema mmoja wa watu waliotangazwa na Mwakyembe juwa wamefukuzwa aiport jana alishastaafu tangu 2013 na sio mfanyakazi wa serikali tangu wakati huo.
Waziri Kamani amesema ameshangazwa kuona mstaafu anatangazwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa wizara yake kama alivyotangaza Mwakyembe jana.
Hata hivyo waziri kamani amesema anasubiri taarifa zaidi toka kwa Dr Mwakyembe kuhusu hatua alizotangaza jana kufukuza wafanyakazi wa wizara yake waliokuwa wakifanya kazi JKNIA.
Source:Radio one Habari
Sasa hapo waziri Kamani anataka kutueleza nini?
Ni kama vile, anapingana na uamuzi wa waziri mwenzie.
Inaelekea Kamani anataka uendelezwe mfumo ule ule, wa wafanyakazi wa serikali kuendelea kuboronga na kuendelea kulindwa, ukiona mfanyakazi wa serikali kawajibishwa sana, basi atahamishwa kituo cha kazi, ili akaendeleze hayo madudu katika kituo chake kipya.
Kama kweli mmoja wa wafanyakazi waliotimuliwa kazi na Mwakyembe, alishastaafu kazi, basi inawezekana wakubwa wa wizara ya kilimo, hawakutaka kumwondoa kwenye payroll, ili waendelee 'kufaidi' mishahara ya mstaafu huyo!!
na hapa ndipo panapotia mashaka kwa hawa watawala wetu, huku ni kukurupuka kama si kujidhalilisha,kulikuwa kuna ulazima gani sasa wa huyo kamani kukimbilia kwenye media huku akidai kusubiri taarifa ya mwakiembe, wame expose udhaifu wao sasa!
Na kwanini Waziri Mwakyembe asimtafute mwenzie Kamani ili wajadiliane kabla ya kuwafukuza wafanyakazi wa wizara ya mwenzie kazi?
Kama nimesikia vizuri Mwakyembe hajawafukuza kazi, ila amewarudisha kwa muajiri wao yeye hataki kuwaona pale airportHuko ndiko kunaitwa kukurupuka. Lakini pia sina uhakika taratibu za kazi serikalini zinasemaje kama Waziri anaweza kumfukuza kazi mfanyakazi yeyote wa serkali hata kama hayuko kwenye wizara yake!!!!! Nafikiri kwa kuweka mambo sawa Mwakyembe angetangaza kuwafukuza hao wafanyakazi kutoka kwenye nafasi zao ndani ya airport ili warudi kwenye wizara zao na huko angemshauri waziri mwenzake kuwafukuza kazi. Lakini sio yeye kuwafukuza kazi.
Tiba
Kama nimesikia vizuri Mwakyembe hajawafukuza kazi, ila amewarudisha kwa muajiri wao yeye hataki kuwaona pale airport
Hii mijadala ndo inachelwesha utendaji. Hata hivyo wabongo ni wanafiki sana, tunataka afanyeje? aunde tume kwanza ama? Akifukuza watu waovu tunasema kakurupuka, akiwaachia uchunguzi uendelee tunasema wanabebwa, sasa mnataka iweje? bongo bila kuwa kauzu huwezi. Dawa ndo hiyo na kama mawaziri na watendaji wote wangekuwa wakali mambo yangeenda. Hata hivyo hajawafukuza kazi ila kawatoa uwanja wa ndege. Hilo swala hata mimi liliwahi kunikuta pale nilitozwa sh 50,000 eti kwa ajili ya cheti cha ugonjwa wa manjano wakati kinauzwa sh 5000 tu
kwa mujibu wa hiyo link hapo chini nanukuu baadhi Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amewatimua vigogo 13 kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Afya na Ustawi wa Jamik atika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kuwarejesha kwenye wizara husika kwa hatua zaidi za kinidhamu na kisheriaMkuu mbali ya kuipata hii habari hapa JF, nimesoma pia gazeti la mwananchi. Gazeti linasema Mwakyembe amewafukuza kazi na kutaka wizara zao kuwachukulia hatua za kisheria. Kwa kuelewa kwangu amewafukuza kazi na anataka wizara zao ziwashitaki.
Inawezekana nimeelewa kinyume.
Tiba
Serikali hawana Mfumo mmoja km Titus anaumoja na Mwakyembe angemtafuta kwanza..,alafu inamaana kuna mishahara hewa ming nchi hii 2ache muvi iendelee...