Mwakyembe amechoka, apumzishwe!

Nchi yetu ilifika mahali ikawa kama haina wenyewe,Mwakyembe alikuwa sahihi kabisa kosa kubwa alilofanya alikurupuka hakujipanga kuleta hoja na hakufanyia kazi
Tunahitaji wataalam hasa wenye vichwa baridi kuokoa taifa letu wageni wanaoa kila siku hapa Tanzania
Itafutwe jinsi ya kuwabana wageni wanaotumia mgongo wa kuoa mtanzania na kupata uraia
Hakuna nchi yoyote duniani inafanya upuuzi kama huu,yaani unaoa raia na kupata uraia easy like abc
Mwakyembe jipange upya kama kweli wewe ni proffessional ili kujisafisha
Mwakyembe na Makufuli wote wamekurupuka!
 
Polonium Ina tabia ya kujirutubisha isipofanyiwa intensive neutralization.Madhara ya POLONIUM yameanza kuwa wazi kwa Mwakiembe, Raid achukue maamzi magumu ya kumpumzisha Huyu Jamaa na amrudishe INDIA haraka iwezekanavyo.
 
Kwakuwa si kosa kumchukua mwanamke na kuishi naye kinyumba haswa baada ya kukubaliana, basi kwa tangazo la Mwakyembe ndoa zingeendelea kwa jinsi ambavyo vyeti vya ndoa havitolewi
 
Huyu Jamaa mimi ni jirani yake,nataka anieleze pale ikolo kijijini kwetu wale vijana hata jina Rita hawajui maana yake,nataka aniambie office za Rita pale ikolo silikugu?badala ya kuzungumzia barabara ya Darajani -katumbasongwe ambayo muda wote shida unaleta upuuzi,

Umevimbiwa indima sasa hata akili imehama,vyama vya ushirika kyela vipo wapi,amakoko isala isi yanalanguliwa umeshindwa hata kuhoji ilikuwaje vyama vya ushirika kyela vimekufaje unaleta upuuzi ambao mtanzania wa kawaida haumsaidii hasa wanakyela ulitojofu.
 
Nchi ya wakurupukaji hata makonda alikurupuka akatangaza list kwenye TV kumbe hana ushahidi sasa anadaiwa vyeti kaamua kujitoa fahamu.
 
Umechanganya mambo humu. Nchi kibao duniani watu wanachukua uraia au resident kwa kuoa au kuolewa. Mantiki ya agizo lake ni sawa lakini utekelezaji wake haukuzingatia jiongrafia na uhalisia wa Tanzania. Utekelezaji unahitaji walau miaka mitatu ikiwa pamoja na kuweka utaratibu wa dawati la Rita katika kila dispensari nchini. Wananchi kuhamasishwa vya kutosha na ikibidi kuondoa na chaji zinazotozwa katika kipindi cha utekelezaji. Lakini vilevile serikali wakati mwingine kama haina "masterplan".
 
Naamini Ana mtu standby aliyempa ubunge hivi karibuni. Binafsi nili doubt credibility yake kuhusu Lowassa wakati kamati haikumhoji, sio kwamba nilikuwa nampenda Lowassa, la hasha ni masuala tu ya kuzingatia haki sawa kwa wote.
 
Ueledi wa masuala ya sheria unatia shaka na kuacha maswali mengi ya kujiuliza dhidi ya waziri wa katiba na sheria Dk Harison Mwakyembe!
Uteuzi wake ulipofanyika wengi waliona kuwa wizara imepata mtu sahihi lakini ni kama vile wizara inaendeshwa kwa mihemko na sifa na siyo kwa kutumia ueledi wa taaluma!
Hivi majuzi alitangaza ni marufuku kufunga ndoa kwa mtanzania yeyote kama hana cheti cha kuzaliwa, deadline akasema tarehe 1/5/2017, lakini mapema tu Rais akajibu mapigo kuwa hilo suala alikuwa halijui na limemshtua, Rais akatengua kauli yake!
Sipingani na suala la kuwa na cheti cha kuzaliwa maana hilo ni suala tu ambalo mtu anaweza akalishughulikia kadri ya utaratibu ulivyo na kupatiwa!
Ila mkurupuko wa kusema watu wasifunge ndoa huku hata mkuu wako hukumshirikisha inaonyesha ni jinsi gani Mwakyembe anavyofanya kazi bila kutumia ueledi!
Jambo lingine ni hili alilotamka kuifuta TLS, kwa matamko hayo ni dhahiri kuwa ueledi wake katika taaluma yake ni wa mashaka hasa ikizingatiwa TLS si taasisi ya serikali ila yeye akaingiza matamko yake ya hovyo kabisa!
Sasa wanasheria wanaojua jinsi ya kutumia ueledi wao wamemuonyesha jinsi wasivyobabaishwa kwenye huu uchaguzi wa TLS.
Kama alivyosema Masha naunga mkono Mwakyembe afutiwe uanachama TLS..
 
Anajitahidi labda atamfurahisha aliye juu matokeo take mtu mzima anaumbuka.
 
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wachache tuliolaumiwa kwa KUMKOSESHA UWAZIRI MKUU MWAKYEMBE pale nilipoamua kumtukuza Mungu kwa kupinga wizi wa kura za ubunge Kyela .

Nina majina ya watu waliokuja inbox kunilaumu , lakini najipongeza sana , hivi huyu kama angekuwa PM angekuwaje ?
 
Ashapumzishwa akapige blablah habari maelezo arudi nyumbani mambo ya Sheria hayawezi
 
Huyu Mwaki-embe sijui Mwaki-chungwa nilikuwa namuheshimu sana wakati aliposimamia ile kamati ya Richmond hadi kuiangusha serikali kwa kuonesha wazi kuwa W/Mkuu wa enzi zile alihusika kwenye uchafu ule. But with time, nimetokea kumdharau sana na kuona kumbe hata issue ile ilikuwa ni dili lililopangwa purposely na kikundi fulani kwa maslahi yao. Nasema hivi kwa kuwa mtuhumiwa alipojitokeza na kusema kuwa "wenye ushahidi wa yeye kuwa fisadi waende mahakamani" nilishangaa kuona kimyaaaaa! Na, ndio maana sasa naelewa ni kwa nini mtuhumiwa mkuu wa richmond kabla hajajiuzulu alisema "tatizo ni Uwaziri Mkuu"! Hii inamaanisha kuwa huyu Mwaki-nani sijui amejaa unafiki wa hali ya juu, mtu wa kimaslahi zaidi na anapenda sana kujifunika na kanisa ili aonekane yupo sahihi, hapana, Mungu anakuona.

Haiwezekani mwenzio aondelewe kwenye nafasi yake ya uwaziri kwa kusimamia kile anachokiamini na ambacho kwa mujibu wa wengi alikuwa sahihi halafu uwekwe wewe uliye "safi kiroho", ukubali nafasi hiyo (kwa mshangao wa wengi) na sasa unajaribu ku-justify kuwa mtumbuliwa alikosea! Eti, "Wewe kama mwanasheria ni mwiko na hutapeleka kitu ambacho unaona hakijakamilika kwani kwa taarifa ulizonazo kupitia vyombo vya habari ni kuwa taarifa yote inatokana na ushahidi wa mlalamikaji ambae ni Clouds". Kama wewe ni mwanasheria tena MZAMIVU, jibu swali hili: Ni kwa nini mahakama huwa inaamua kesi kwa kukubaliana na upande mmoja wa mlalamikaji ikiwa mlalamikiwa hakutokea mahakamani baada ya jitihada kadhaa za kumtaka kufika mahakamani kugonga mwamba? Please, give us a break!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…