CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,358
- 6,422
Huu ndio upuuzi unaoifanya nchi hii kubakia maskini. Rubani kazi yake ni kuendesha ndege, kuongoza shirika la ndege lazima uwe umebobea katika STRATEGIC Management na sio urubani. Paul Chizi alikuwa boss wa JETLINK, shirika la waKenya, kwa wakenya kumpa uboss mtanzania hawezi kamwe kuwa mbabaishaji, hata kidogo kwa vile kule kuna ushindani sana. Waziri Nundu alimuomba aache kazi kule aje kuokoa jahazi nchini kwake, nyie mnataka afanyiwe interview wakati credentials zake ziko clear!? Kwa muda mchache aliokaa amefanikiwa kuleta ndege ambayo ndo most competent kwenye soko la afrika masharika. Boeing 737-500 inabeba watu 108 na inatumia saa moja kamili DAR to Mwanza kwenye abiria wengi. Iko very efficient kwenye fuel. Precision wana boeing yao inabeba abiria 137 lakini mara nyingi haijai na inakula mafuta zaidi pia inatumia saa moja na dk 10 Dar to Mza. Fly 540 wanatumia Jet inabeba abiria 54 tu ingawa iko fuel efficient kama hii ya ATC lakini inatumia saa moja na dk 15 Dar to Mza. Kama umeenda kidogo shule calculate COMPETITIVE ADVANTAGE hapo then utaona kwa nini hata bei Bw Chizi aliweka chini kuliko bei za hao wengine. Jamaa wa mashirika binafsi huyu jamaa aliwanyima usingizi kabisa. Sisi tunaotumia huu usafiri mara nyingi tumehuzunishwa sana na kuondolewa kwa huyu jembe kwa alitupa bei ya ukombozi na ndege inakuwa full wiki nzima toka imefika. Labda kaondolewa kwa kuwa yuko KAMBI YA LOWASSA!!!!
Kwa nini amemwachisha kazi? Hilo ndilo muhimu. Any clue!?