Mwakinyo anataka kutafunwa na zimwi limjualo

Nikupongeze kwa mawazo yako ila haina maana ndio sahihi zaidi.

Naona mahaba kwa Mwamini yamekubeba zaidi mpaka unazidisha viwango vya usifiaji sasa na inaonekana wewe kwenye ulingo wa ngumi ni mgeni sana .

Sasa kabla ya kuanza kupamba huko waulize wenye ngumi zao kuhusu Michael Yomba Yomba na Jumuiya ya madola.

Ila kama hutakuwa na haraka basi ulizia pia kuhusu Rashidi Matumla kama utakuwa na muda waulizie kizazi cha kina Kinyogori kisha soma ulichokiandika hapo juu.

Naomba kuwasilisha .
Ukisema ivyo hata kina fid sugu na wengine wengi wao ndio walia Anza bongo fleva ila hela wanakula kina diamond Kiba na wengine wengi
 
Ukiangalia mapambano yake hayavutii kwamba ni bondia mwenye kipaji tofauti na wengine kama anavyokuzwa
Hana jipya uingereza alishinda ndiyo tukamjua haya ya bongo mawili yote kabebwa
Wanavyo mkuza mwakinyo kwann wasimkuze na twaha kiduku kwann mpaka apigane na mwakinyo kama sio kutafuta nafasi???
 
Atapigwa huko nje,lakin mwakinyo hana uwezo wa kumpiga kiduku
Sasa yeye anasubir awe bondia mkubwa kwa kumpiga mwakinyo wakat mwenzake mwakinyo akienda popote pale anagawa dozi uyo twaha kiduku kapigwa mapambano yote ya nje kwa tko mwenzake kashinda mapambano mengi ya nje kwa tko alafu Leo mtake kumringanisha mbuyu na mchina kisa huota kwa stail moja
 
Mwakwinyo aache kupigana na mabondia waendesha bodaboda, walinzi, part-time boxers kama PAZ, inatakiwa apigane na wale magwiji wenyewe.
 
Kwahiyo kosa la Kiduku ni nini? Kuomba pambano na champion?, Sasa usipoomba pambano na champion unataka aombe na nani? Ni kawaida kwenye masumbwi bondia yeyote mwenye lengo la kufika on top lazima apigane na wa juu yake ili aipate hiyo nafasi, hata kina Antony Joshua tunaowajua wasingepata majina kama wasingepigana na 'matop' kina Klitschko na kuwapiga, Andy Ruiz dunia haikuwa inamtambua hadi alipompiga AJ. Na juzi hapa nimemuona bondia no1 one pound for pound anaitwa Crawford alipompiga Kelly Brook na alipoulizwa yupi unamtaka next, akajibu anamtaka Man Pacquiao, Je jiulize kwanini anamtaka zaidi Man Pacquiao wakati kuna mabondia wazuri wengi kwenye division yake kama Errol Spence Jr, Keith Thurman, Shawn Porter, Garcia, n.k. Jibu; anamtaka zaidi Pacquiao kwakuwa 1. Ana mkanda 2. Ni maarufu zaidi (so kibiashara anatarajia kupiga hela zaidi) 3. Ni legend tayari (Ukimpiga legend cv yako inakuwa kubwa zaidi) 4. Kujiongezea fanbase (kwakuwa Pac ana mashabiki wengi hivyo sikuhiyo anauhakika wa kupata mashabiki wengi wapya endapo akiperfom vizuri hivyo kumuweka vizuri zaidi kibiashara). Hivyo Mwakinyo akiombwa pambano na Kiduku asipanic, inapaswa awe proud kwamba yeye ni mkubwa tayari ndio maana mabondia wengine wakubwa wako interested naye ili na wao wafike hapo juu alipo, hata kama anakataa pambano atafute sababu za kukataa zenye mashiko maana sio lazima akubali (pambano la lazima ni la mandatory tu ila haya mengine ana hiyari ya kukubali au kukataa), ila anachoboa watu ni ile mipasho yake na dharau zisizo na maana, angekuwa anakataa kistaarabu tungemuelewa tu. Na sio kusema huwezi kupigana na bondia wa Moro, wakati baada ya kutoka Uingereza alipigana na bondia mchovu kabisa wa Tanga anaitwa Said Yazidu, that's NONSENSE
 
Mwakinyo sio bondia mkubwa sema anatafuta watu wake mabondia wa vichochoroni wa huko nje ili apate umaarufu tu
 
kiduku anatafuta jina kupitia Mwakinyo aende nje huko akapambane
Kwani mwakinyo anakataa nini kupigana naye ili ajitengenezee cv nzuri?ujue anaogopa kupigwa na kutia aibu ndio maana anaokoteza vibondia vya uchochoroni ili apate umaarufu kumbe watu wamemstukia
 
T
Usanii bongo unaharibu michezo na mambo yakiendelea hivi mabondia watagoma kuja bongo kucheza angalia pambano la juzi uniambie liliisha vipi me sielewi
Jifunze kwanza TKO zinakuwaje ndo ulete ubishi...ule sio ugomvi zile ni ngumi zinasheria....Kaangalie pambano la kwanza kati ya Lennox vs Krishko au pambano la pili kati ya wilder vs Tyson Fury utajifunza kitu.
 
Ukisema ivyo hata kina fid sugu na wengine wengi wao ndio walia Anza bongo fleva ila hela wanakula kina diamond Kiba na wengine wengi

Mwakinyo bado hana mafanikio makubwa ya ngumi kulinganisha na sifa anazopewa ila haina maana kuwa ni bondia mbaya hapana ila bado aongeze jitihada na juhudi.
 
T
Jifunze kwanza TKO zinakuwaje ndo ulete ubishi...ule sio ugomvi zile ni ngumi zinasheria....Kaangalie pambano la kwanza kati ya Lennox vs Krishko au pambano la pili kati ya wilder vs Tyson Fury utajifunza kitu.
TKO unakubali kushindwa baada ya kuona umezidiwa na hautashinda na huwenda utashindwa kwa Ko kama ukiendelea kukaza kwa hiyo unakubali mapema kuepusha hilo
Katika pambano letu haikuwa hiyo refa aliingilia katikati ya movement na kuwatenga mabondia mpinzani bado alikuwa anajiweza na mpaka refa alipigwa ngumi ni kama mazingira ya kutengeneza tu moja ya member wa muagentina alikuwa anadoubt haelewi nini kimetokea
Angalia jinsi pambano lilivyoisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom