Hassan Mwakinyo ashinda kwa KO round ya 7

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Bingwa Mtata Mtatuzi Hassan Mwakinyo amefanikiwa kunyakua Mkanda wa WBO baada ya kumtwanga Bondia kutoka nchini Ghana Elvis Ahorgah kwa KO raundi ya 7 katika pambano lililofanyika visiwani Zanzibar.

Bingwa huyo mtata Mtatuzi Champez Hassan Mwakinyo amewadhihirishia watu kuwa yuko fit na ana force KO muda wowote anaotaka yeye,hivyo kuwa bondia hatari kwa KO. Ni dhahiri Bingwa wa UBO Intercontinental,Bondia Twaha Kiduku amepata meseji na naamini atafanyia kazi KO za Champez Hassan Mwakinyo,Bingwa Mpya wa WBO.

Watanzania wengi wana hamu ya kuona pambano la Bingwa Hassan Mwakinyo vs Bingwa Twaha Kiduku na baada ya pambano hilo Watanzania wangependa tena kuona pambano lingine la kiufundi kati ya Bondia Loren Japhet vs Champez Hassan Mwakinyo,Naamini mkwanja utawekwa na mapromota na mapambano haya yatatokea mwaka huu 2024.

#HongeraChampezMwakinyo.
 
Hongera zake sanaaa....tunasubiri na Kiduku sasa....akimaliza kama itampendeza amtafute Mfaume Mfaume.....kelele ziishee
 
Ni fake,,umefurai we mçhawi.
Una matatizo makubwa mno. Mimi ni mpenzi wa ngumi na nina uzoefu na haya mambo. Ni kawaida kukutana mabondia wa Tanzania wakishinda mikanda feki ambayo haitambuliki duniani ndiyo maana nimeuliza ni WBO hii hii inayotambulika? Ulichotakiwa kufanya ni kujibu. BTW uchawi ni wewe unaamini, lakini wengine hatuko huko.
 
Wewe unayeijua mikanda fake na original ndio tunasubiri taarifa kutoka kwako, usijifanye victim. Uchawi maana yake sio kuruka na ungo.
 
Wewe unayeijua mikanda fake na original ndio tunasubiri taarifa kutoa kwako, usijifanye victim. Uchawi maana yake sio kuruka na ungo.
Taarifa kutoka kwangu: Hayuko kwenye orodha ya WBO. Nenda kwenye website yao, japokuwa unaonekana lugha gongana!
 
Twaha kiduku asithubutu kabisa kupigana na huyo mwamba atapasuka vibaya mno
 
20240128_193744.jpg
 
Taarifa kutoka kwangu: Hayuko kwenye orodha ya WBO. Nenda kwenye website yao, japokuwa unaonekana lugha gongana!

Mimi sio lugha gongana bwashee, I can brag here with my high school education, I spit 4 languages fluently. Ukiondoa lugha ya nyumbani kwa bibi, naongea Kiswahili fasaha, I speak English, hablo Español and ik spreek Nederlands. I'm not a homeboy fam.
 
Hongera mkuu
 
Divulge the locus of your English erudition. Is it native to your lexicon, or perchance acquired under the tutelage of another pedagogue?"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom