Mwakinyo amtaka Asemahle kumziba mdomo asijione kamaliza

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,463
21,194
Bondia Hassan Mwakinyo ukipenda muite Colorado King A.K.A CHAMPEZ ONE TIME , Tornado amtaka Asemahle Wellem amuoneshe kazi baada ya kuona Watanzania wamenyoosha mikono kwamba hawamuwezi bwana mdogo ni bora wasikubali kucheza naye kinyume na hapo atazidi kuwadhalilisha mabondia Watz kama alivyowafanya mabondia top 2 wanaotazamwa zaidi hapa bongo kwenye uzito wao wa super middle weight ambao ni Selemani Kidunda na Twaha Kiduku.

Mwakinyo mwanzoni hakuonesha interest ya kupigana na huyu kijana licha ya kuitwa mara kadhaa ila safari hii ameona dharau zimezidi acha aingie mzigoni.

Asemahle baada ya kumchapa Twaha, bondia aliyemtaka alikuwa ni Hassan Mwakinyo lakini management ya Mwakinyo haikutoa ushirikiano mzuri ndipo Selemani Kidunda alipoiomba hii mechi alipe kisasi matokeo yake naye kajumuishwa kwenye listi ya waliopigwa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

-327824375.jpg


Screenshot_20240302-201728_1.jpg

Mwakinyo kigezo cha kwanza anachoangalia kwa bondia wa kupigana naye ni mkanda ,na kwa kuwa Asemahle ana mkanda wa WBF kwa hiyo ameshakidhi kigezo cha kwanza cha kupigana na Mwakinyo.

Kigezo cha pili huwa anaangalia maslahi , hivyo ni rahisi hili pambano kufanyika ,kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha Asemahle hivyo ni rahisi mapromota kuingia mzigoni maana pambano lao litabeba attention kubwa sana.

Binafsi sina imani sana na Mwakinyo ,maana mara nyingi hakosi visingizio yani kama attention seeker fulani hivi 😂😂😂😂😂😂😂.

Mbali na Mwakinyo, Twaha naye amelitaka hili pambano kwa mara ya pili ili kurudisha heshima yake aliyoipoteza .
 
Yule asemale ni kama jini mwakinyo asilete ujuaji anaweza akaaibika mtu asemale ni mjanja mjanja sana ukutumia nguvu anakuuwa
Mwakinyo muongeaji tu.

Mwenye nia ya dhati haswa ni Twaha Kiduku, japo pambano la Mwakinyo na Asemahle ndilo lenye mvuto zaidi
 
Mwakinyo nilikua namshabikia zamani ila nimekuja kugundua ni attention seeker na hapo ndio aliponipoteza kabisa.

Yaan maneno meeengi na visasi vya kike, shenzi kabisa
 
Back
Top Bottom