Mpigamsuli
JF-Expert Member
- May 24, 2012
- 3,885
- 584
rudi nenda kavue kyupi tu utapata kazi
mpigamsuli una ugomvi na huyu dada nn
Pole sana mdada...ila usikate tamaa na usiweke mawazo kwenye kuajiriwa.
Nenda kwenye shule za private fundisha kwa muda then ujipange kujiajiri.
pole sana dada yangu,jaribu kufikiria nje ya field yako na angalia pia fursa katika mazingira yako na kazi za kujitolea ili ujenge network yako.feeling sorry,usichague kazi ili mradi iwe halali,all the best
Ungekua umejua mapema unge volunteer ingekupa experince then ungeomba unachukuliwa mapema kwa ajili ya experience utakayokuwa nayo
badilisha hiyo avator imekaa kichawi, au mwenzangu mchawi tujue
hahahah! course nyengine ukiona jina tu unastuka!SOCIAL PROTECTION!!!
Wasalaam,
Ndugu zanguni ni mwaka wa saba sasa natafuta kazi bila mafanikio.
Niliomba kazi kila mahali lakini sijafanikiwa. Nikajaribu kuwaomba maboss mbalimbali lakini niliambulia kuombwa rushwa ya -- nikawa nawakimbia. Hapa nilipo hadi hamu ya kutafuta kazi sina maana naona kama napoteza muda. Interview huwa naitwa lakini naishia kwenye written siendi mbali na hapo. Nafasi zenyewe zinakuwa chache lakini mnaitwa watu kibao. Natamani biashara lakini sina hata mtaji.
Maisha yamekuwa magumu mpaka mtaani waliofeli wanasema flani mwenyewe kasoma lakini mbona yupo tuuu. Inaniuma sana. kama kuna mtu anaweza nisaidia angalau nipate hata pa kuamkia nitashukuru sana wapendwa. Naishi Dar na nimesoma kozi ya social protection frm IFM.
Nisaidieni jamani.
Price amekushauri vizuri,naomba niongezee kuwa,jitahidi "kujishusha" nimeweka kwenye mabano coz simaanishi uvae vibaya au usionekane kama msomi,ila namaanisha usidharau kazi,hasa zile za kujiajiri,lkn pia kama unajua komputerPole, kama unaweza somo lolote fungua tuition au Nursery school jus kwa muda huku ukiwa unaangalia utaratibu mwengine.
Mkuu wewe tumefanana na ni kweli kabisa uyasemayo,Na baadhi ya niliofanyanao vibarua hivyo walidhani kusoma hakuna maana kama na mimi nasotaTusifarijiane kiujanjajanja wengine mnachagua sana kazi,mimi nlipata kazi 2012 wakati nipo chuo mwaka wa mwisho,na UE ya mwisho nimefanya huku natokea kazini,nilikua nalipwa 160,000/=Tsh,kwa mwezi,uliza now nadaka kiasi gani!!!,coz nilikubali kuanza padogo na bila kuchagua,so tafakarini sana graduate wa miaka hii,ok pm me nikuelekeze what to do.......!
Una elimu gani? Samahani lakini. Pole sana
Miaka 7 unatafuta kazi? Huwezi ukawa siriaz!!
tatizo la kwanza ni hiyo kozi uliyosoma,market yake ipo chini kwa nchi yetu,pili inaonekana unachagua kazi,nakushauri kuwa tayari kufanya kazi yoyote hata kama hujaisomea kama bank teller,loan officer na nyinginezo ukisubiri mungu akushushe kwenye kile ulichosoma.