Wenzio tulipomaliza vyuo, serikali ilisimamisha ajira zote (enzi za SAP kama uliwahi kuisikia au kuisoma kwenye kozi zenu)! Kwa maana hiyo tuli-graduate na kuagwa kama kwamba hatukusoma. Kufika mtaani kulikuwa hakukaliki na ukikumbuka enzi hizo za miaka ya '90. Wallah hatukuchagua kazi, tulipiga hadi kibarua cha ufundi mwashi, siyo haba hatukulia ajira kama unavyojilizaliza hapa, mpaka hatimaye wakaja wakaachia wenyewe wakubwa tukazama kwenye ajira kama hatutaki vile!! Mbona jamani ajira zipo za kumwaga? Hujaona matangazo ya ajira TAMISEMI? Wanatafuta mpaka watendaji wa vijiji, Kata n.k Hizo siyo ajira? Au unataka mpaka uende ukakalie kiti cha kuzunguka? Utasubiri sana!!!
Mtu umesoma Social Protection halafu unachagua kazi!!!! Acha hizo, mwishowe umri wa kusataafu utakukuta uraiani na hapo ndo itakuwa imekula kwako!! Kama huwa unaitwa kwenye usaili unaishia kufanya written interview, basi jichunguze vizuri, pengine CV yako haina mashiko au huwa unajibu kile ambacho hakijaulizwa. Ukute mtu una GPA ya 2.0 halafu uataka kushindana na wenye 4.0 hapo lazima uachwe!! Asikudanganye mtu, hayo nayo huwa yanaangaliwa!!
Mama kwa vile umesoma kozi ambayo ina nafasi chache za ajira, usithubutu kuchagua kazi piga yoyote itakayokuja mbele yako, hata ikibidi utendaji wa kijiji mengine yatajipa mbele ya safari. Na hili liwe fundisho kwa wengine katika kuchagua kozi za kusoma kwa vile tumelelewa kusomea ajira na si vinginevyo!! Elimu ya TZ majangaaaaaaaaaaaa!!!