Mwaka wa tano sasa tangu nimalize Chuo (SUA) sina kazi

TZCHINA

Senior Member
Dec 6, 2019
126
152
Habari jamii forum,

Kama kichwa cha Habari kinavyo sema mimi ni mhitimu chuo cha SUA mwaka 2016 bsc environmental sciences and management sijapata kazi na msoto mtaani unaendelea kuwa mkubwa zaidi. Hivyo basi kwa mwenye CONNECTION naomba msaada kazi yoyote nafanya.
 
maisha ya mtaani yasikie tuu kama hayajakukuta huwezi elewa kadhia yake ila mkuu kuwa mvumilivu.... kwa waislamu kuna phrase inasema "Mungu yupo na wenye kusubiri"


subira.jpg
 
Mkuu kasome zile kozi za OSHA ziko 2 ukizimaliza unapata kazi viwandani, migodini na site za ujenzi. Usibweteke.
Tatizo lake hata hiyo hela ya kupata kusoma hizo course ni shida. Mtu akishafikia kukuambia yupo teyari kufanya kazi yoyote, jua hana hata kabiashara cha kumuingizia siku au kulima. Ni mtu leo anaweza akapata zali, kisha likapita hata mwezi patupu.
 
Mkuu kasome zile kozi za OSHA ziko 2 ukizimaliza unapata kazi viwandani, migodini na site za ujenzi. Usibweteke.
Natamani sana kusoma hizi kozi lakini UWEZO ndugu yanyu upo chini sana.

Gharama nadhani haipungui kuanzia tshs. 180,000/=, ila nikipata kazi yoyote ambayo itanisaidia kupata chochote nitaanza kusave ili baada ya miaka 2 nikasome hizi cozi.
 
Back
Top Bottom