Mwaka unaisha, umefanikiwa kufanya nini?

Mwaka unaisha, umefanikiwa kufanya nini?

Niliweka lengo la kupanga chumba...na limetimizwa

Niliweka lengo la kukuza biashara na limetimia kwa asilimia 80

Nilipanga kujaza vitu vyote vya muhim chumban na limetimia

Kiufupi namshukuru Mungu huu mwaka nmetimiza mengi

2020 naomba lile lengo kuu nlopanga litimie
Amina Mungu awe nawe
 
Mimi namshukuru Mungu (Alhamdulillah)

SHULE: nimegraduate mwaka huu
KAZINI: nimeongezwa cheo na mshahara
HOBBY: nimesoma vitabu vingi
MUONEKANO: nimekuwa smart
TABIA: nimekuwa na mitazamo chanya, MARAFIKI: marafiki wazuri, wengine mashuhuri na wenye mafanikio zaidi

2019 is a beautiful year to me, regardless of many bad challenges I faced. Welcome 2020 inshallah nipo tayari (malengo yapo tayari nimeshayaandika kwenye diary nakusubiri wewe tu 2020)

Asante Mungu.
 
Mwaka huu:

1. Nimeongeza ujuzi kwenye forex.

2. Nimejifunza website development (Hii nataka niitumie sana mwakani, infact mpaka sasa nimetengeneza websites mbili).

3. Nimesoma vitabu vinne vya kuongeza maarifa.

4. Nimeboresha ujuzi katika kazi yangu.

5. Nimejifunza kwamba "Bila pesa furaha hakuna".

6. Nimejifunza social media marketing hasa kwenye facebook na instagram.

MWaka huu sehemu kubwa nimetumia katika kuongeza ujuzi hasa maeneo yasiyo ya fani yangu!

The idea ni kuwa na wigo mpana kiuchumi! Kuanzia mwaka natarajia kuanza kuona matunda kwa uwekezaji wa elimu/ujuzi nilioufanywa mwaka huu.

Kwa sasa nakumbuka hayo.
Umejitahidi hadi nimeona sijafanya kitu [emoji22][emoji22][emoji22].
 
Nimefanikiwa japo Kujenga nyumba yangu japo sijamalizia. Mungu akisaidia 2020 nitaimalizia
IMG_20191012_114311.jpeg
 
Back
Top Bottom