sibusiso dlomo
JF-Expert Member
- Apr 23, 2016
- 691
- 386
kikwete alianza vizuri sana sana katika miaka yake ya mwanzoni lakini alikosa usimamizi mzuri ndio maana walikuwa wanapiga sana dili...(maisha bora kwa kila mtanzania kwa ku pump hela nyingi kwenye economy)...lakini hizi hela nyingi hazikufika kwa walengwaWassalam..
Leo tar 25 oct 2016, ni mwaka 1 sasa tangu tupige kura kuchagua rais wa awamu ya 5 na mh. JPM aliibuka kidedea kwa asilimia 58 ya kura zote za watanzania waliopiga kura. Awamu yake ilitanguliwa na mh. Jakaya Kikwete aliyeshika madaraka kwa miaka 10 kuanzia 2005 mpaka 2015 akitusua kura zaidi ya asilimia 80 za watanzania waliopiga kura katika awamu yake ya kwanza (2005-2010).
Sasa katika awamu hizi 2 karibuni tukumbushane ndani ya mwaka mmoja wa kila Rais kipi kilifanyika kwa ustawi wa watanzania.
Karibuni.
Magufuli kaanza vizuri sana kwa kusafisha makosa mengi ya muhimu aliyofanya mh kikwete katika miaka yake ya mwisho (utawala bora,rushwa,mapato)..to me wote walikuwa na wana idea nzuri ila nadhani utawala wa Mh magufuli una nia njema sana na Tanzania ila sijajua kuhusu sheria,nguvu ya dola,demokrasia,viongozi kuingilia kazi zisizo wahusu,utumbuaji usiofuata sheria za kazi....nk
hatuwezi kusema nani anafanya mazuri zaidi au alifanya mazuri zaidi ila in 3years nadhani ndio tuangalie je ameweza kutekeleza yale anayoyasema