Mwaka huu mikoa ya Dar na Pwani ina maajabu

kimbendengu

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
6,032
10,254
Wakuu wa JF, nimeishi kwenye hii mikoa kwa miaka kumi sasa lakini nikiri kuwa sijawahi kushuhudia baridi ya kiwango cha mwaka huu yaani upepo balaa baridi yenyewe hatari.

Jana nyuzi joto ni 22c lakini hata leo hali ni hiyo hiyo hali ya hewa hii nimezoea kuona Iringa, Ruvuma na Mbeya kwa wale wataalamu nipeni mabadiliko hayo.

Asanteni
 
Hali ya hewa tu haiko poa hata huku kwetu Mtwara Kuna baridi wakati sio asili yake.
 
Hii inanikumbusha mwaka 2010, ile baridi ilikuwa kiboko pia. Ilikuwa ikifika saa 11 jioni kama hujaoga basi ufanye mpango wa kupasha maji.
 
Huu ni muda wa 'winter' huku Southern Hemisphere. Sehemu nyingi ni baridi kupita maelezo. Jua kali linakuwa Northern Hemisphere.

Ukifika mwisho wa mwaka, mtatafutana na hilo joto.
 
Oooh sawa, Kisarawe ipo juu kidogo lazima kaubaridi katakua kakali kuliko sehemu za mabonde kama Bagamoyo ingawa kweli mwaka huu kama baridi imekua kali kidogo.

Nilim qoute Msingida hapo juu aliyesema alipo yeye temperature inashuka hadi kufikia nyuzijoto 9, nikamuuliza ni wapo huko alipo?
Hii inaweza kuwa Mbeya au makambako maana kuna siku nilicheki usiku ilikuwa inasoma 11 degrees...
 
Nahisi imesababishwa na Corona.

Kipindi ugonjwa umepamba moto, shughuli nyingi zilifungwa hasa viwanda vikubwa na Ndege nyingi zinazochafua hali ya hewa ziliacha kuruka. Hivyo haya unayoyaona sasa yanawezekana endapo tutatunza mazingira.
+1
Hata anga limekuwa la blue zaidi, viwanda na ndege vinachangia sana kuchafua hali ya hewa , na ndio sababu mikoa hii ya pwani na dar Sasa hivi inaonekana kuwa na baridi
 
Hii inaweza kuwa Mbeya au makambako maana kuna siku nilicheki usiku ilikuwa inasoma 11 degrees...
Kwa viwango vya Tanzania hiyo ni baridi kali sana Mkuu. Maana tumezowea temp. iki drop mpaka 22 au 23 tunalalamika baridi, sasa ikiwa 11 au hiyo 9 si hatari kabisa hiyo
 
Nahisi imesababishwa na Corona.

Kipindi ugonjwa umepamba moto, shughuli nyingi zilifungwa hasa viwanda vikubwa na Ndege nyingi zinazochafua hali ya hewa ziliacha kuruka. Hivyo haya unayoyaona sasa yanawezekana endapo tutatunza mazingira.
Point
 
Back
Top Bottom