balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 14,473
- 12,593
Hapo Jangwani na Zanaki ndo zilikuwa na A level na ni za wasichanaJangwani na Zanaki,kisutu na Forodhani,Kibasila hazikua Secondary?,naanza kupata wasiwasi na wewe
Hapo Jangwani na Zanaki ndo zilikuwa na A level na ni za wasichanaJangwani na Zanaki,kisutu na Forodhani,Kibasila hazikua Secondary?,naanza kupata wasiwasi na wewe
Nakumbuka nilikuwa nasumbua kata nzima na kwa tarafa nakuwa wa pili au wa tatu kwenye ile mitihan tulikuwa tunafanya pamoja(nishasahau inaitwaje)
Kimbembe necta 1st selection sikuchaguliwa
Basi hata wale mafala wakapata cha kujitetea kwa wazazi wao( utasikia " we mpaka fulan amefeli me ndio ningefaulu mtihani ulikuwa mgumu) ikawa topic
Sikutoka ndani week kadhaa nalia tu aisee sitosahau maana mzee ilibid aingilie kati kunitafutia private ndio akili ikakaa sawa
Hata shule niliyosoma mimi pia kulikuwa na choo kinachonuka maana kilikuwa kikongwe sana.Mkuu umenionesha bweni langu la Kimweri hapa Tabora boys kwa chini huku uwanjani kuna choo kinanuka ukitaka kuingia lazima uvue nguo zote nje ndio uingie vinginevyo ukitoka wenzako wanakukimbia
Wanafunzi wengi wanapata fursa ya kusonga mbele tofauti na zamani
Zamani sana hii mkuu1990 mkuu
Hahahahaaaa very true. Uncle wangu aliniambia hii pia mkuuKabisaaa... Mambo ya twisheni hatukuwa nayo kabisa
Hongera sana mkuuAisee mimi ni mmojawapo... Na tulikuwa tunatoka sita tu mkoa mzima kwenda IFUNDA TECH kila mwaka... Nilijulikana ile mbaya yaani
Mzee Kikwete alijitahidi sana enzi zake...Mkuu hii ishu iliishia 2004 kurudi nyuma
Kuanzia 2005 alipoingia Kikwete ni mwendo wa shule za kata hata Kama ulikuwa unapasua
Naam Naam... Form one ukifika unakutana na wenzio waliongoza mkoa/wilaya walizotoka.Wakati huo kupangiwa shule kama 'uboyzini' ilibidi uwe 'kipanga' kama CCNP Engineer
Safi sana umenikumbusha mbali sana, Wape hi pande za Kinyerez huko
Tanzania imetoka mbali sana mkuuMkuu hii ishu iliishia 2004 kurudi nyuma
Kuanzia 2005 alipoingia Kikwete ni mwendo wa shule za kata hata Kama ulikuwa unapasua
Nakumbuka nilipomaliza darasa la Saba shule yetu tulikuwa 232
Ila tuliochaguliwa(kufaulu) tulikuwa 14 tu wavulana Tisa na wasichana 5
Aisee tulikuwa tunaonekana watabe sana na alwatan sana kitaa
Jangwani, Zanaki, Kisutu ilikuwa ni Wasichana tu.Jangwani na Zanaki,kisutu na Forodhani,Kibasila hazikua Secondary?,naanza kupata wasiwasi na wewe
Kwahiyo kufaulu wachache na kufaulu wengi kipi bora?. Yani kipi bora wachache waelimike au jamii nzima ielimike?. Acheni husda ngoja maisha yawanyoosheBaada ya kumaliza darasa la Saba wakati ninasubiri matokeo mzee alinipeleka sehemu nijifunze kushona suti, mwalimu wangu alikuwa katili mno vibao vya nguvu vilitua kwenye shavu langu pindi nilipoangalia kwingine tofauti na kumuangalia anavyoshona. Hali hii iliniathili kisaikolojia kila wakati sikuwa na amani, matokea yalivyotoka nilikuwa nimechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Kijiji kizima nilianza kuonekana kama mtu special hata yule mwalimu wangu wa kushona suti alianza kuniheshimu. Wazazi wangu walianza kuhofia kuwa huenda mwanao atalogwa maana shule nzima wamechaguliwa wanafunzi watatu tu, siku hizi cha kushangaza hata wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu kwenda sekondari.