Mwafrika ahatarisha uhai wake kumuokoa Mzungu...

Dogo apewe pongezi zake, zima moto wamfikirie mambo ya rescuing unit.

Then siku hizi Hakuna ubaguzi kabisa

Wanasema eti
"when they go black they never come back"
 
Katika hali ya kawaida, wala isingekuwa ishu ya "wa rangi gani amemwokoa wa rangi gani". Kama mtakumbuka hivi karibuni katika ajali ya meli iliyozama Zanzibar, kulikuwa na Wazungu waliookoa Waafrika na Waafrika waliookoa Wazungu bila kujali nani ni nani. Lakini kuwa binadamu tumekuwa si wa kawaida, tunaweka mbele hisia za uzawa na rangi kabla ya ubinadamu.


 
huyu kijana ametoa meno shauri zake ka wako huko bila makaratasi wajomba watawagongea nyumbani kwao hawanaga shukrani wale
 
Kweli mkuu, ila nadhani angekuwa kijana wa kiarabu asingesaidia! Sijui waarabu wanawaonaje wazungu!

Umejiwekea dosari mwenyewe kwakuwa tayari ni mbaguzi wa rangi na sishangai ukawa mbaguzi wa dini au kwa maana nyingine ukawa ni extremist.Shame on you
 
Habari nzuri ...Lakini Kichwa Cha Habari That's Racist...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hongera sana kwa kijana Nelson kwa moyo wa kujitolea, hivi ndivyo binadamu tunavyotakiwa kuishi, yeye mwenyewe alitoa msaada HAKUANGALIA anasaidia famia ya rangi gani, sasa siye wengine haya ya ubaguzi yametoka wapi????///
 
Kwa iyo muafrika ni mtu asiyetegemewa kutoa msaada mpaka heading ya habari hii iwe hivi???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hapa issue isiwe rangi bali mtoto ambaye ni malaika na ni binadamu. Unajuaje kama mtoto aliyekuwa anakabiliwa na kifo angekuwa muafrika na mzungu akasikia asingekuja kufanya alichofanya muafrika. Acheni kujenga imani za kibaguzi. Hujui kuwa mtoto ni malaika hata nyoka angeweza kumuokoa achia mbali huyo mswahili? Je wangekuja zimamoto wangeulliza nyumba inayoungua ni ya mswahili au mzungu? Tafuteni sababu zinazoingia akilini badala ya kuendekeza ubaguzi. Ungeandika muafrika ahatarisha maisha yake kumuokoa mzungu. Je ulitaka nani amuokoe huyo malaika? Hapa alichofanya ni kumuokoa jirani yake. Na hii ndiyo mila ya kiafrika na binadamu wengine. Ubaguzi ndiyo upo lakini tusiuanzishe au kuupa nafasi kwenye mawazo yetu kama mleta mada alivyofanya.

Kosa kubwa kumwita au kumfananisha huyo mtoto na Malaika. Tunawapenda watoto lakini kosa kubwa ambalo wengi wanalifanya ni kuwafananisha watoto na Malaika. Ikumbukwe kwamba Malaika ni viumbe watakatifu ambao ni watumishi wa Mungu na wasiotenda dhambi. Mtoto ana asili ya Adam. Ni mwanadamu na ana dhambi ya asili na ndiyo maana hata kama ana umri chini ya mwaka anaweza akaonyesha hisia zake za hasira aidha kwa kulia au kwa kutupa kitu au kwa jinsi yeyote ya kuonyesha ule ubinadamu na dhambi ya asili. Kwa hiyo kuwafananisha watoto na Malaika ni kosa. Vinginevyo nampongeza kijana kwa kufanya ubinadamu kwa kumuokoa huyo mtoto wa jirani ninaamini hakujitosa kwenye moto kumuokoa kwa vile ni mzungu bali dhamira aliyokuwa nayo ya kumuokoa binadamu mwenzake.
 
Pole sana Shenkalwa maana hujui usemacho. Hiyo dhambi ya asili ni utunzi wako wala haipo. Mie hiyo dhambi yako ya asili sina na Mungu si mpuuzi kumwadhibu mja kwa makosa ya bibi wala babu yake. Nadhani hili liko wazi. Anyway sina muda wa kukufundisha kusoma na kufikikiri badala ya kukariri hata yasiyoingia akilini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom