Mwafrika ahatarisha uhai wake kumuokoa Mzungu...

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
[h=2][/h]

Kijana pichani Nelson Fonangwan mwenye miaka 17 amefanya hivyo.Alikuwa amelala nyumbani kwao na kuamshwa na kelele za majirani ambao walikuwa wakiunguliwa na nyumba.

Aliamka na kwenda kuangalia nini kinaendelea akakuta nyumba ya jirani ikiungua na mama mwenye watoto wawili akihangaika kuvunja dirisha kwenda kumuokoa mtoto wake mdogo Adam mwenye miaka 2.
Mama alivunja dirisha bila mafanikio huku moto ukizidi kuwaka ndipo Nelson alipokuja akavunja dirisha na kuingia ndani kumuokoa mtoto.Mama akapiga simu 999 ikaja gari ya zimamoto.

Akisimulia moto ulivyotokea mama wa mtoto anasema alikuwa ameenda nje kutupa uchafu akiwa amemuacha mwanae mdogo jikoni.Kurudi mlango ukawa umejifunga na kumbe aliacha fying pan jikoni ikaanza kuungua na baadae moto kuanza kuwa mkubwa.Alijitahidi kuvunja dirisha na mkono ambao aliumia sana huku akipiga kelele ndio kijana Nelson kutokea na kumsaidia.
Tukio hili lilitokea nchini Uingereza maeneo ya Southampton.Kijana Nelson Fonangwan asili yake ni Cameroon.
 
Hapa issue isiwe rangi bali mtoto ambaye ni malaika na ni binadamu. Unajuaje kama mtoto aliyekuwa anakabiliwa na kifo angekuwa muafrika na mzungu akasikia asingekuja kufanya alichofanya muafrika. Acheni kujenga imani za kibaguzi. Hujui kuwa mtoto ni malaika hata nyoka angeweza kumuokoa achia mbali huyo mswahili? Je wangekuja zimamoto wangeulliza nyumba inayoungua ni ya mswahili au mzungu? Tafuteni sababu zinazoingia akilini badala ya kuendekeza ubaguzi. Ungeandika muafrika ahatarisha maisha yake kumuokoa mzungu. Je ulitaka nani amuokoe huyo malaika? Hapa alichofanya ni kumuokoa jirani yake. Na hii ndiyo mila ya kiafrika na binadamu wengine. Ubaguzi ndiyo upo lakini tusiuanzishe au kuupa nafasi kwenye mawazo yetu kama mleta mada alivyofanya.
 
Nimefurahi sana kwa huyo kijana kuokoa maisha ya huyo malaika
 
Hii story inam-portray huyu mwafrica kama sub-human species. Ni kama vile mwafrica hawezi kufanya kitendo kama hicho. Na hapo mjinga flan kaona hiyo ni habari worth to be publish. Hivi sisi Waafrica tuna shida gani?
 
Mleta mada mwenyewe anaitwa Boflo...
____
_||__| | ______ ______ ______
( | | | | | | |
/-()---() ~ ()--() ~ ()--() ~ ()--()

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kwenyd majanga au tatizo hakuna mzungu wala muafrika,kama position inaruhusu kwann usisaidie bu Kisa ni uafrica wa huyo jamaa.
Kuna kpind nilienda kula bata kisiwa cha bongoyo,katika kupiga mbizi za hapa na pale nikajikuta navutwa kuelekea far from the beach,ule mkondo wa pale wanadai ni mkondo wa maji unaotembea. Nikaomba msaada kwa wenzangu kwa kunyoosha mkono juu huku natumbukia naibuka,wenzangu c waogeleaji kivile wakisogea kidogo wanarud nkajsemea duh ndo mwisho nn nlikuwa nimechoka balaa. Wakaenda kuomba msaada wakaja wahind flan wakashindwa mida kidogo akatokea dada mmoja akaogelea mpaka nilipo akisaidiana na wale wahind kunivuta mpaka nje. Baada ya ku2lia ndo nikamdadic yule dada ni mfaransa alikuwa kwenye vacation ya 2 weeks in tz hata ngel ilikuwa inasumbua.
All in all msaada ni popote mwenzako anapouhitaj tuache kujitenga wenyewe nimejifunza kutoka kwa huyo sista bila yeye siku hiyo sijui.
 
Aiseeee babaangu ni swala la ujirani mwema 2 "mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe" amri kumi za mungu

ngoja nipate kisusio hapa mamsera kwa mwarabu
 
Amefanya jambo zuri, kama hao wazungu walikuwa na tabia ya ubaguzi watakuwa wamepata funzo na wao.
 
Ujiko hapo Nelson. Wazungu walivyo, hapo tayari amekaa moyoni mwa mama huyo na kumtoa ni kazi kubwa. Unanielewaeeh?
 
Hapa issue isiwe rangi bali mtoto ambaye ni malaika na ni binadamu. Unajuaje kama mtoto aliyekuwa anakabiliwa na kifo angekuwa muafrika na mzungu akasikia asingekuja kufanya alichofanya muafrika. Acheni kujenga imani za kibaguzi. Hujui kuwa mtoto ni malaika hata nyoka angeweza kumuokoa achia mbali huyo mswahili? Je wangekuja zimamoto wangeulliza nyumba inayoungua ni ya mswahili au mzungu? Tafuteni sababu zinazoingia akilini badala ya kuendekeza ubaguzi. Ungeandika muafrika ahatarisha maisha yake kumuokoa mzungu. Je ulitaka nani amuokoe huyo malaika? Hapa alichofanya ni kumuokoa jirani yake. Na hii ndiyo mila ya kiafrika na binadamu wengine. Ubaguzi ndiyo upo lakini tusiuanzishe au kuupa nafasi kwenye mawazo yetu kama mleta mada alivyofanya.

Mkuu mbona unanishambulia mm...

Hii habari nimeicopya na kupaste na iko ktk source nyingi, google utaona mwenyewe acha upashkuna
 
Dini ya Afrika ni upendo wa dhati. Dini za kigeni ndizo zilizoleta ubaguzi wa rangi.
 
[h=2][/h]

Kijana pichani Nelson Fonangwan mwenye miaka 17 amefanya hivyo.Alikuwa amelala nyumbani kwao na kuamshwa na kelele za majirani ambao walikuwa wakiunguliwa na nyumba.

Aliamka na kwenda kuangalia nini kinaendelea akakuta nyumba ya jirani ikiungua na mama mwenye watoto wawili akihangaika kuvunja dirisha kwenda kumuokoa mtoto wake mdogo Adam mwenye miaka 2.
Mama alivunja dirisha bila mafanikio huku moto ukizidi kuwaka ndipo Nelson alipokuja akavunja dirisha na kuingia ndani kumuokoa mtoto.Mama akapiga simu 999 ikaja gari ya zimamoto.

Akisimulia moto ulivyotokea mama wa mtoto anasema alikuwa ameenda nje kutupa uchafu akiwa amemuacha mwanae mdogo jikoni.Kurudi mlango ukawa umejifunga na kumbe aliacha fying pan jikoni ikaanza kuungua na baadae moto kuanza kuwa mkubwa.Alijitahidi kuvunja dirisha na mkono ambao aliumia sana huku akipiga kelele ndio kijana Nelson kutokea na kumsaidia.
Tukio hili lilitokea nchini Uingereza maeneo ya Southampton.Kijana Nelson Fonangwan asili yake ni Cameroon.

nelson ashukuliwe sana kwa umbea wake ndio umenusuru maisha ya mtoto huyo..
Bravo nelly mkameruni
 
Suala la Uafrica na uzungu unatoka wapi???hapa ni binadamu kamsaidia binadamu mwenzie mwenye shida..Period.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom