Mvutano wa hisia za binadamu

Kibundi wa getto

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
455
875
Wakuu

Kuna kitu kinanichanganya sana,katika maisha yangu .Mimi sio MTU wa kupiga sana simu kwa watu.Huwa napokea sana lawama Juu ya hii tabia,naonekana jeuri japo Mimi sielewi kwanini nipo hivyo.

Kitu cha ajabu kinacho nishangaza ni kuwa,kila ninapomfikiria MTU ambaye sijaongea nae mda mrefu basi uyo Mtu lazima atanipigia simu.

Zamani nilikua sichukulii uzito ili swala lakini sasahivi limezidi sana.Yani siku nikianza kumuwaza MTU yeyote ambaye mda mrefu atujawasiliana basi lazima uyo MTU anipigie simu siku iyo iyo.

Siku nyingine nikiwawaza ata watu 3 lazima wote wanipigie.Mpaka kuna mda naogopa kuwakumbuka baadhi ya watu.

Hivi hii inatokana na nini?,kwa anayejua msaada tafadhali.
 
,...hata mimi nisipokuwa na voucher na nataka kuwasiliana na mtu huwa namvutia hisia kali za kina-then namwambiwa Juma/Preta(nataja jina) nipigie simu nataka kuongea na wewe sasa hivi.
.....hakwepi-muda si mrefu huyooooo hewani.

....wala sio uchawi ni sayansi/kanuni tu za nguvu za kimaumbile mkuu...take it easy
 
Mkuu hebu sema ukweli kama ww sio mm..

Mm hata ukitaja jina langu kimoyo mwili unasisimka, hua sutajwi nisisikie mwanzo nilikua nikilala naota yote yatakayo tokea mchana na inakua kweli.
 
Wakuu

Kuna kitu kinanichanganya sana,katika maisha yangu .Mimi sio MTU wa kupiga sana simu kwa watu.Huwa napokea sana lawama Juu ya hii tabia,naonekana jeuri japo Mimi sielewi kwanini nipo hivyo.

Kitu cha ajabu kinacho nishangaza ni kuwa,kila ninapomfikiria MTU ambaye sijaongea nae mda mrefu basi uyo Mtu lazima atanipigia simu.

Zamani nilikua sichukulii uzito ili swala lakini sasahivi limezidi sana.Yani siku nikianza kumuwaza MTU yeyote ambaye mda mrefu atujawasiliana basi lazima uyo MTU anipigie simu siku iyo iyo.

Siku nyingine nikiwawaza ata watu 3 lazima wote wanipigie.Mpaka kuna mda naogopa kuwakumbuka baadhi ya watu.

Hivi hii inatokana na nini?,kwa anayejua msaada tafadhali.
Brains intuitions, mawasiliano ya kiroho ama makutano ya kiroho ndio husababisha hiyo hali, haimtokei kila mtu though
 
Hizo ni dalili za psychic awakening...nakushauri google hiyo psychic awakening au nenda you tube utapata mafundisho ya mentors huko..dalili hizo ni karama uliyonayo ndiyo inaanza kufunguka kwa sixth sense au third eye..hiyo ya mtu kukupigia simu unapomfikiria inaitwa telepathy na itafuatiwa na clairvoyant then teleportation na mengineyo...mwisho utaishia kuwa mtenda miujiza kama akina tb joshua.
Nakushauri usiende kwa wachungaji uchwara au waganga watakuibia hiyo karama wewe jifunze masharti kupitia youtube na vitu vya kula na namna ya kujilinda pia nakushauri kama upo maeneo yenye msongamano wa watu na makelele mengi basi hamia nje ya mji maeneo yasiyo na kelele nyingi ili uweze kuwa karibu na nature nikimaanisha where the fields are evergreen and calm.pia pendelea kukaa mwenyewe zaidi hii itakufanya uweze kufikiri zaidi in form of meditation.
 
Ulipomtaja tb joshua ndio umeharibu..... mpka leo unawawaza hao watu tu.. duh
 
Ninamaanisha chanzo cha nguvu zao zilitokea wapi..hizi nguvu zinavyoanza ziko tu kama watoto wanapozaliwa kuna wakati wao wanachojuani kulia tu kisha wanaanza kuita mama au baba then dada au kaka baada ya hapo wanaenda shule wote wanafundishwa a e i o u baadae wanamaliza std seven kisha sekondari iv and vi baada ya hapo wengine wanasomea ujasusi au udaktari au uinjinia au vibaka na wapigaji...sasa kwa mantiki hii itategemea yeye atajiheshimuje au atakutana na akina nani ambao atashirikia nao kuendana na matamanio ya kibinadamu.hivyo huyo tb joshua unavyomuona au unavyomchukulia ni ile picha aliyojijengea au wale maadui zake wanavyomuelezea hivyo sijui wewe ni nafsi yako ilikufanya umchukulie kama ilivyo sasa au ni ushawishi kutoka kwa maadui/wapinzani wake walikushawishi umuone hivyo ila yote ni yote watenda miujiza wote hawatumii mapepo kama chanzo kikuu cha miujiza yao bali hutumia sixth sense zao ambazo kwa namna moja au nyingine mapepo hupenda kuwasaidia kupitia jamii za usiri.
 
,...hata mimi nisipokuwa na voucher na nataka kuwasiliana na mtu huwa namvutia hisia kali za kina-then namwambiwa Juma/Preta(nataja jina) nipigie simu nataka kuongea na wewe sasa hivi.
.....hakwepi-muda si mrefu huyooooo hewani.

....wala sio uchawi ni sayansi/kanuni tu za nguvu za kimaumbile mkuu...take it easy

Kuna kitabu nilikisoma kinaelezea hiyo kitu,kimsingi tunatakiwa tujue mawazo ni power,hisia za ndani za binadamu sio za kupuuzwa na yeye mwenyewe huwa zinazaa vitu halisi.
 
Ninamaanisha chanzo cha nguvu zao zilitokea wapi..hizi nguvu zinavyoanza ziko tu kama watoto wanapozaliwa kuna wakati wao wanachojuani kulia tu kisha wanaanza kuita mama au baba then dada au kaka baada ya hapo wanaenda shule wote wanafundishwa a e i o u baadae wanamaliza std seven kisha sekondari iv and vi baada ya hapo wengine wanasomea ujasusi au udaktari au uinjinia au vibaka na wapigaji...sasa kwa mantiki hii itategemea yeye atajiheshimuje au atakutana na akina nani ambao atashirikia nao kuendana na matamanio ya kibinadamu.hivyo huyo tb joshua unavyomuona au unavyomchukulia ni ile picha aliyojijengea au wale maadui zake wanavyomuelezea hivyo sijui wewe ni nafsi yako ilikufanya umchukulie kama ilivyo sasa au ni ushawishi kutoka kwa maadui/wapinzani wake walikushawishi umuone hivyo ila yote ni yote watenda miujiza wote hawatumii mapepo kama chanzo kikuu cha miujiza yao bali hutumia sixth sense zao ambazo kwa namna moja au nyingine mapepo hupenda kuwasaidia kupitia jamii za usiri.
Kwa iyo nafsi inatuma kuchukia tu haiwezi kukutuma wewe ukampenda bila sababu....

Tb joshua ana muujiza gan aliowah kuifanya unaokupagawisha wewe
 
Hizi hisia zipo maana kuna wakati unahisi kitu fulani kama hakipo sawa labda kwa ndugu, jamaa na marafiki baada ya mda ndio unapata taarifa kamili kichwani unasema ndio maana nilikuwa nahisi kitu
 
Mi nina uwezo wa kukimbia hatari zlizo mbele yangu matokeo mengi sana ya hatari nimeshawahi Kuya escape utakuta ghafla natoka eneo la tukio nikirudi naambiwa kuna jamaa kaja hapa kishari anakutafuta
 
,...hata mimi nisipokuwa na voucher na nataka kuwasiliana na mtu huwa namvutia hisia kali za kina-then namwambiwa Juma/Preta(nataja jina) nipigie simu nataka kuongea na wewe sasa hivi.
.....hakwepi-muda si mrefu huyooooo hewani.

....wala sio uchawi ni sayansi/kanuni tu za nguvu za kimaumbile mkuu...take it easy
hio chai mkuu
 
Back
Top Bottom