Dr Willibrod Slaa
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 675
- 1,523
Ben,Dr Slaa,
Kwanza nitoe pongezi za dhati kwa kazi nzuri mlioifanya kufanikisha ushindi wa jimbo la Tarime.
Pili, sasa hivi kuna mbimu mbalimbali zimetumiwa ili kuhakikisha CHADEMA inayumbishwa,suala mojawapo ni hili la kuendelea kukichafua chama ambalo linafanywa hata na wanasiasa ambao jamii haijaweza kuwatambua kwamba wako katika siasa kwa malengo gani hasa.Linapofanywa au kusemwa jambo na mtu ambae jamii inamtambua kama mwanaharakati wa haki,huwa ni lazima jamii itamuamini hata kama ni uongo.Na uongo huu huu ukiachwa,basi utaaminika kwamba ni ukweli.Sasa tuchukulie mfano maneno anayoeneza Mch. Mtikila kwamba CHADEMA imehusika na kucheza rafu katika kifo cha mhe.Wangwe na bado ana mpango wa kusambaza nyaraka milioni moja nchi nzima,
Je,CHADEMA kukabiliana na hili Tatizo au kwa kuanzia CHADEMA kama taasisi imechukua hatua gani mpaka sasa?
Tatu, Tuongelee utaratibu uliotumika kwenye kampeni bila shaka kila mtu atakubaliana nami nikisema ulikua mzuri na makini.Je,bajeti ya uchaguzi ilikua kiasi gani au ni lini itawekwa hadharani?
Nne, Bila shaka CHADEMA imejenga imani kubwa kwa watanzania lakini kinachowanchanganya wananchi zaidi ni kwamba uchaguzi mkuu unakaribia na hakuna dalili za kuanzisha rasmi muungano wa vile vyama vyenye nia ya kweli katika upinzani.Naamanisha kama CUF kwani angalao ndiyo walioonekana kwamba ni bold katika politics zenye mafanikio ya kweli na sina uhakika sana na TLP.Je CHADEMA ukizingatia pia tarehe ya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti ni hadi March next year tutakua tumejiandaa vya kutosha ku-balance na vyama au chama tutakachokua tunaungana nacho? pia kumbuka bado kuna chaguzi za mitaa.
Pia kuna jambo moja ambalo ni la muhimu sana,tunajua taifa liko katika wakati mgumu ,Maandamano,migomo,kurushiana mawe nk. yaani ilimradi tumekua kama vile tuko ukanda wa Gaza,sasa kuna hili suala la waalimu kunyanyaswa na mishahara yao.Ningeshauri katika zile halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA hususani Tarime,chama kiangalie kama kitaweza kufanya fund raising kuhakikisha angalao waalimu wanaongezewa asilimia kadhaa ili kurahisi au ku-buy more political credits.Najua CHADEMA kama taasisi kina limited resources but kina uwezo wa kufanya angalao jambo kama hilo na kuwaambia jamani ee sisi uwezo wetu ndiyo huo.Hapo tutakua tumepiga hatua moja mbele.
Kila la heri
Thanks a lot. Kwa niaba ya viongozi wote wa Chadema ninakuhakikishia tumepokea Pongezi na nimekwisha kuwafikishia wote sasa hivi kwani tuko pamoja hapa tulipo.
i) Kuchafuliwa: Ben nadhani sasa ni dhahiri kuwa Chadema imechafuliwa zaidi kwa wanaosoma magazeti na wasio kwenye ground. Kwa watu walioko field hakuna dalili kabisa ya Chadema kuchafuliwa na maneno haya ya kupachikwa. Watanzania ni watu wenye upeo sana japo wengi hawajaenda shule kubwa. Hivyo, usiwe na wasiwasi, ndio maana Tarime haikutupa shida wakati msingi mmoja wa kuchaguliwa ni mtu wao. Wana Tarime waliwadharau wote waliokuwa wanaendesha siasa za kuchafuana. Kwa upande wa Chama hakuna ukweli wowote kuwa Chama kimeyumbishwa. Kwa bahati nzuri, hapa tulipo tuna documents kuwa wanaoeneza mambo haya wana malengo ambayo mwanzo hatukuyajua lakini sasa tunayafahamu hivyo haitusumbui.
ii) Ni kweli tuliendesha Kampeni nzuri Tarime, japo tumefanyiwa kila aina ya huduma, rushwa zimetumika sana, shahada zimenunuliwa sana, na Nguvu za polisi zilitumika mahali ambapo haikuwa lazima kabisa. Punde tutatoa Bajet yetu halisi ikihusisha Magari na mafuta, mafuta, ukodishaji wa Helcopter,chakula cha Timu yetu ya Kampeni na malazi yao. Bado tunakusanya taarifa kutoka kwa watu mbalimbali hasa waliojitolea resources zao. Kutoka Chama matumizi yetu yalikuwa kama 60 Million lakini kwa vyovyote tukiweka thamani ya yote yaliyotolewa na watu wenye nia njema itakuwa zaidi ya hapo. Hata hivyo, tunachofurahi ni kuwa japo siku zote, Chadema ilisakamwa sana kwa kutumia helcopter, watani wetu walianza kutumia Helcopter Uchaguzi Mdogo wa Kiteto na sasa wametumia mbili. Hii ina tafsiri mbili a) wenzetu siku zote wame copy kutoka kwetu mambo mengi tunayoyafanya. b) Japo tulisakamwa sana na kujenga picha ya anasa kwa kutumia helcopter, ubadhirifu kwa kutumia helcopter kwa wenzetu kumbe yote sasa ni halali! Tunazidi kupata picha ya wenzetu.
iii) Taarifa kamili siyo tu itatolewa hadharani, lakini pia itakuwa kwenye Website ya Chama very soon. Inaweza kuchelewa kidogo kwa vile Staff yote ya Chadema Makao Makuu ipo kwenye "Operation Sangara" ambayo ni operation maalum ya kujenga Chama katika ukanda wa Ziwa kuanzia 19 October, 2008.