Mvua za Tanzania zina maajabu kweli kweli!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Mvua za Tanzania ni za maajabu kweli kweli!

Zinanyesha Maji yake yanakwenda kujaa kwenye mashamba ya miwa na kusababisha uzalishaji wa sukari kushuka na hivyo bei ya sukari kupanda hadi kufikia Tshs.5,000/= kwa kilo 1.
( Rejea maelezo ya Waziri Bashe)!

Wakati huo huo mvua zinazonyesha Maji yake hayaendi kwenye Mabwawa ya kuzalishia umeme na mgao wa umeme hauna ukomo mpaka pengine mwezi April 2024!
( Rejea maelezo ya Mkurugenzi wa Tanesco Eng.Nyamohanga)!

Tanzania ni Nchi ya maajabu kweli kweli!

Guinness book of records mnaachaje kuingiza Nchi hii kwenye records zenu!?

Kwa wasiojua jueni kuwa hakuna deal inayolipa kwa rushwa kubwa hapa Nchini kuliko deal la utoaji wa vibali vya kuagiza Sukari na kuingiza Nchini!

Hakuna mzalishaji anayekubali kuzalisha sukari wakati ya kuagiza inafika hapa Nchini kwa bei ya Tshs.1500/= kwa kilo 1 na wao wanawauzia wajinga kwa Tshs.5,000/= kwa kilo 1 !

Jiulize hapo Zanzibar tu sukari haijawahi kufikia Tshs.3,000/=, wao miwa na sukari wanatoa Dunia ipi?!

Tunajua uagizaji wa sukari ni deal za watu za kukusanyia rushwa kubwa kubwa katika utoaji wa vibali!

Uliona ujinga huu wa vibali vya hovyo hovyo vya kuagiza Sukari wakati wa Mwamba Hayati Magufuli!?

Magufuli alikuwa jiwe kweli! kweli! na Mwamba kweli kweli!!
Nyie pigeni pesa Tanzania ni Nchi ya wajinga wajinga , watu wa oya! oya !
 
Back
Top Bottom