Mvinyo wa Jack Daniels uligunduliwa na Mwafrika

Swahili AI

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
6,183
46,745
1621675049524.png

Ukitazama vyema picha hii, utagundua kuna mtu mmoja tu mweusi (Muafrika). Huyo ndiye Nearest au “Master Distiller” kwa jina maarufu. Alizaliwa wakati wa utumwa mnamo huko nchini Marekani 1820. Huyu bwana ndio mwalimu aliyemfundisha Jack Daniels jinsi ya kuchakata mvinyo huo. Ilikuwaje?

Jack Daniel ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 10 wa tumbo moja la Mama Lucinda na Baba yao Calaway Daniel. Mama yake Jack alifariki Jack angali mtoto sana, hivyo Baba yake kuamua kutwa jiko jingine na kujaaliwa kupata nae watoto watatu. Baba yake Jack, Calaway, alikwenda vitani (American Civil War), na kufika huko, baada ya kifo cha Baba yake Jack alishindwa kuishi nyumbani na Mama wa kambo, hivyo kutimkia mtaani akajikuta akiishi kituo cha watoto yatima.

Jack akiwa kituoni pale, aliasiliwa na mchungaji mmoja kwa jina Dan Call. Dan Call ni mfanyabiashara mbalimbali na alikuwa mtu wa kazi lukuki ikiwamo utengenezaji wa mvinyo ambao kwa wakati huo, ulikuwa haramu nchi marekani, hivyo aliutengeneza usiku mwingi. Jack alikuwa mdadisi sana, hadi Bwana Dan kuamua kumfundisha taratibu kutengeneza mvinyo, lakini ukweli ni kwamba, hata Bwana Dan mwenyewe hakuwa mtaalamu sana kwenye sekta hiyo kama ilivyo kwa mtu mweusi mmoja kwa jina Bwana Nearest.

Dan Call alimchukua Jack na kumkabidhi wa Nearest au Green wa jina jingine, na kumuambia kuwa, “Mfundishe mtoto huyu vyote unavyojua kuhusu kutengeneza mvinyo”.. Nearest alimfundisha Jack mbinu zote na utaalamu wa kutosha kuhusu mvinyo hadi Jack akaiva kisawasawa, Jack alikuwa na umri wa miaka 8 tu wakati huo. Pia Mchungaji yule alimwambia Nearest, “Nataka Jack awe mchakataji mvinyo mkubwa duniani”

Baada ya mkataba wa kusitisha biashara ya utumwa kutiwa sahihi marekani 1865, mwaka mmoja baadae Jack alifungua kiwanda chake cha mvinvyo na kumuajiri Mwalimu wake na kuwa mkuu wa utengenezaji mvinyo kiwandani hapo. Hata baada ya Nearest kufariki, kiwanda kiliendelea kuwaajiri watoto wa Nearest hadi kufika 2017 vitukuu na hadi vilembwe vilikuwemo ndani ya kampuni hiyo.

Tukumbuke, wakati huo watu weusi hata kuhesabiwa hawakuhesabiwa kwenye sensa, hivyo kujua umri wao sahihi ni ngumu sana. Hawakupiga kura wala kumiliki biashara licha ya kuwa na uwezo na akili za hali ya juu... Afrika, tunaweza sana, tujiamini na tupende mila na desturi zetu.

1621675650735.jpeg
 
Niliwahi kusoma mahali Fulani kuwa hata machine ya kukata majani ilivumbuliwa na mwafrika aliyekua mtumwa
 
View attachment 1793799

View attachment 1793827
Mvinyo?
 
Hiko kiwanda kipo Lynchburg,Tennessee(Lafayette hwy 50) karibu na mji wa Tallahoma,TN. Kuna kambi ya Air Force
 
Ndiyo cha Mwafrika kujivunia hicho?
 
Back
Top Bottom