MUWAZA na pongezi kwa BLW


Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,899
Likes
8,133
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,899 8,133 280
Spika BLW Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho

MUWAZA inakutunukia pongezi zake za dhati kwa matamshi yako ya kizalendo ya kutetea uhuru, uwezo na nguvu za BLW kwa kutamka kwamba "Hakuna Mtu au Utawala wowote unaoweza kubadilisha maamuzi ya BLW".


MUWAZA imefarijika na inatoa pongezi kwa msimamo madhubuti huo ambao umeweka wazi Mamlaka ya BLW na kuondosha tafsiri za migongano zilizotolewa hapo kabla baada ya Mkutano wa NEC wa karibu huko Dodoma.


Kauli hiyo ilio wazi na isio na wasi wasi wowote ya Mh. Spika wa BLW imesaidia kutolewa kwa kauli sahihi ya Rais wa Muungano wa Tanzania Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete huko Uturuki na kufuatiliwa na kauli sahihi za ndugu zetu Waziri wa Mambo ya Kimataifa wa Tanzania Mh. Bernard Membe pamoja na kusahihishwa kwa kauli sahihi ya Katibu Muenezi wa CCM Mh. John Chiligati. MUWAZA imefurahishwa kusikia kauli sahihi na zilizorekibishwa na ndugu zetu hawa wa Bara kwa kuunga mkono maamuzi ya BLW na kuitakia Zanzibar mema.


MUWAZA inamshukuru Spika wa BLW Mh. Pandu Ameir Kificho kuwa ni chachu ya kuondosha wingu la suitafahum baina ya ndugu zetu wa Tanzania Bara na Zanzibar


MUWAZA vile vile inaomba kutumia nafasi kwa kupitia kwa Mh. Pandu Ameir Kificho kuwapongeza Wawakilishi wote wa Baraza la Wawakilishi kwa kuonyesha moyo wa maridhiano, kutetea mustakbal wa Zanzibar kwa pamoja bila ya kujali mirengo ya kisiasa, kusimama kidete kwa sauti moja katika dhamana yao ya kuondosha uhasama baina Wazanzibari na kuchimba misingi ya mashirikiano kwa maslah ya Zanzibar na kuzika uadui ulio wafarakanisha Wazanzibari kwa muda mrefu


MUWAZA vile vile kwa kupitia Spika wa BLW inawapongeza Wawakilishi wote kwa kusimamia utekelezaji wa:

Kusimamisha BENDERA ya Zanzibar,
Kuanzisha NEMBO ya Zanzibar,
Kuanzisha WIMBO WA TAIFA,
Kutetea MAFUTA ya Zanzibar
Kulilinda na kulitukuza BLW
Kulinda, kuitetea, kuihifadhi na kuitengeneza KATIBA ya Zanzibar

MUWAZA kwa kupitia Mh. Spika wa BLW inatuma pongezi zake za dhati kwa Mwanashria Mkuu Mh. Iddi Pandu Hassan pamoja na timu yake ya Wanasheria kwa kutunga kwa haraka Sheria ya Kura ya Maoni Zanzibar, sheria ambayo itaifungulia Zanzibar milango ya kheri siku za usoni.


MUWAZA haitakuwa mwizi wa fadhila kwa kusahau chanzo cha michango ya maraidhiano kwa hivyo papo inachukuwa fursa hii adhiim kuwapongeza tena Rais wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad kwa ushujaa na ujasiri wao kuiletea maridhiano ya Zanzibar.


Kwa niaba ya MUWAZA

Dr. Yussuf S. Salim Mwenyekiti wa Muda wa MUWAZA
 
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
6,901
Likes
340
Points
180
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
6,901 340 180
Ok I got it

MUWAZA = Jumuiya wa Wa-Zanzibari waishio Ng'ambo
 
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Messages
10,945
Likes
240
Points
160
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2008
10,945 240 160
Ok I got it

MUWAZA = Jumuiya wa Wa-Zanzibari waishio Ng'ambo
Nilikuwa sijui maana yake.
Asante sana
Vipi kuhusu MUWATA (Jumuiya ya Watanganyika waishio ng'ambo) hiyo ipo?
 
Elusive

Elusive

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2008
Messages
223
Likes
1
Points
35
Elusive

Elusive

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2008
223 1 35
Nonesence Rudini nyumbani muijenge nchi yenu kama kweli mnaipenda.
 
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,487
Likes
3,084
Points
280
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,487 3,084 280
Ok I got it

MUWAZA = Jumuiya wa Wa-Zanzibari waishio Ng'ambo
Bado sijakupata hapo! Hizo herufi za accronym M-U-W-A-Z-A zinasimama badala ya maneno gani? Just curious!
 
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2008
Messages
1,322
Likes
21
Points
135
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2008
1,322 21 135
Wengine tunachelea kutoa pongezi mpaka tuone matokea lakini mwanzo mzuri. Nini kirefu za MUWAZA?

Tafadhali Mwanakijiji.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Mwanakijiji wewe ndio msemaji wao msaidizi?
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
kwani huko nyumbani hakuna wanaoipenda!?
Siasa za Zanzibar ni za kubadilika sana sasa utaona baada ya kuwa uchaguzi umefika na kwenda kwenye uchaguzi na tena baada ya kuwa na serikali.
 
C

Calipso

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2009
Messages
284
Likes
2
Points
35
C

Calipso

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2009
284 2 35
M/kijiji Kikwete amesema nini huko Uturuki?,tuhabarishe baba...
 
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
MUWAZA=Mustaqbal Wa Zanzibar

Sijuwi hapo kama nitakuwa nimesaidia au nimeongeza mtafaruku zaidi na neno Mustaqbal :rolleyes:
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
238
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 238 160
Frosty,
Naona umeongeza mtafaruku. Neno Mustaqbal si Kiswahili sahihi.
 
Sonara

Sonara

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2008
Messages
729
Likes
5
Points
35
Sonara

Sonara

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2008
729 5 35
Frosty,
Naona umeongeza mtafaruku. Neno Mustaqbal si Kiswahili sahihi.
inategemea unaijuwaje tafsiri ya kiswahili kwani sio kila mtu anachimbuko la kiswahili kuna wengine ni waparamiajhi wa bandi wangoni kwa kushurutizwa na viongozi wa siasa ndio wamekuwa watumizi wa kiswhili
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
82,146
Likes
121,676
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
82,146 121,676 280
Bado sijakupata hapo! Hizo herufi za accronym M-U-W-A-Z-A zinasimama badala ya maneno gani? Just curious!
Nadhani ni Muungano wa Wazanzibar (Wa Pemba na Unguja).
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
238
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 238 160
inategemea unaijuwaje tafsiri ya kiswahili kwani sio kila mtu anachimbuko la kiswahili kuna wengine ni waparamiajhi wa bandi wangoni kwa kushurutizwa na viongozi wa siasa ndio wamekuwa watumizi wa kiswhili
Ukweli unabaki pale pale kwamba mustaqbal si kiswahili sahihi.
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
238
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 238 160
Do you want to call a friends or do you want 50 -50 ?
kwi!kwi!kwi!
Let me call a friend. Kiswahili sahihi ni "mustakabali." Alivyosema Bwana Frosty ni Kiarabu.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,652
Likes
32,395
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,652 32,395 280
Ukweli unabaki pale pale kwamba mustaqbal si kiswahili sahihi.
Jasusi, Mustakabali ndio sahihi, neno hili limetoholewa toka Kiarabu, alichofanya mwandishi ni kuliandika kwa uhalisia wake.

Kiswahili kimeazima asilimia kubwa ya maneno ya Kiarabu, ndipo kikafuatia Kireno, Kijerumani na hatimaye Kiingereza.
 

Forum statistics

Threads 1,251,881
Members 481,931
Posts 29,789,104