Muungano ukivunjika

Muungano ukivunjika

Zanzibar kuwa full membership united nation
Zanzibar kuwa na mabalozi wake all over the world

Zanzibar kuwa member wa Fifa
Zanzibar kuwa member wa Caf
Zanzibar kuwa member wa OIC
Zanzibar kuwa na passport yake
Zanzibar kuwa member wa East Africa community(EAC)
Zanzibar kuwa na nyanja nzuri za kiuchumi, kimataifa na kitaifa bila ya vikwazo.
Zanzibar kuwa na sarafu yake.
Zanzibar kuwa na wizara yake ya elimu,
Zanzibar kuwa na wizara ya Anga
Zanzibar kuwa na bank kuu.
Zanzibar kuwa na jeshi lake coast guard
Zanzibar kuwa na jeshi la polisi lake
Zanzibar kuwa na usalama wa taifa
Zanzibar kuwa free port, kama dubai.
Zanzibar kuwa member wa AU


Wizara hizi zote zina ajira zaidi ya 10,000 ni faida kwa wazanzibari.

Kwa upande wa Tanganyika, nahisi kuwa watatumia jina la Tanzania .

Watatumia influence ile ile ya Jamuhuri ya Muungano na Jamuhuri ya Tanzania au tanganyika, ni kubadili kidogo tu.

Siwezi kusubiri case ya Muungano kuja kusikilizwa huku Zanzibar, kwa maana nina kila sababu ya kuunga mkono, faida ni nyingi kwa Wazanzibar kuliko hasara.

InshaAllah
utavunjikaje wakati wauza chips za ukwaju,pweza na kuku sekela mpaka urojo ndo tunawetegemea kuendeleza muungano bara
 
hizo meli wanazo?ili ujitenge watakiwa walau uwe umejizatiti kila idara..sasa wao hata umeme hawana wamechukua huku..mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha kisiwa kinazid kua kidogo jumlisha na populition kuongezeka kila siku..hao watu watakaa wapi
Umeme Zanzibar hawapewi bure wananunua,ni biashara Mkuu,Tanesco wakikata umeme Zanzibar itakuwa imekula Kwao,watakosa mabilioni ya shilingi,Popolation ya Zanzibar sio tatizo hiyo ni faida kwa Zanzibar,tizama kisiwa kama cha japan kina watu wengi kuliko ukubwa wa Kisiwa,Japan ni nchi moja iliyoendelea duniani
 
Hapo ndio mnapofeli, wakati wengine mkijifanya Karume hakufanya chochote na kuwatukuza kina Shamte ndio hapohapo wengine wanapowaona nyinyi ni mamluki, wengine wanaamini kabisa Karume alikubali muungano baada ya kuwastukia nyinyi masalia wa Sultani mtamsumbua baadae na ndio sababu hiyo hamuwezi kukaa meza moja kwani mna ajenda mbili tofauti.
Yale mnayofanya pale Kisonge ndio taswira halisi ya mnapokwama.

Unataka kuniambia Shamte alifungwa Tanganyika baada ya muungano na huo mlioufanya sio uvamizi?? Nimemtaja Karume hapo?
 
Sasa ukisoma hapo hujui hata maana ya neno Inasemekana? Wewe yale uliyotuletea kupitia migazeti yako unaweza kutuwekea ushahidi hapa?



Inasemekana hiyo ni dhana na ndio nikakuomba ulete ushahidi wa huyo aliyekupa hiyo mipasho
 
Sasa ukisoma hapo hujui hata maana ya neno Inasemekana? Wewe yale uliyotuletea kupitia migazeti yako unaweza kutuwekea ushahidi hapa?
Nimekuletea mpaka tarehe ya hilo gazeti wewe niwekee huko ulikosikia ni wapi gazeti ?redio au mtu gani?au Padri gani??
 
Bila Tanganyika Hamna Zanzibar utaskia Mimi mpemba au Mimi muunguja au Mimi mmafia msiombe damu ya ubaguzi iendelee kusambaa bora tuje na wazo la serikali tatu kuliko kujitenga
Mafia sio Zanzibar, at least mpemba na muunguja, unajua tayari tanganyika kuna ukabila, usukuma sasa hivi upo kipao mbele, kama sio msukuma utahenyeka sana. Soon Wamasai, wapare, Mtwara huko, Arusha, mutagawana nchi
 
Kibaya zaidi 75% ya watu wa huko wana asili ya bara, biashara ya utumwa ndiyo imewapeleka huko. Hivyo kuna koo za huku bara zina uhusiano wa karibu na za huko, yaani watu waliyoko kule wengi wametokana na vizazi vya watu wa bara. Wazanzibar kwa asili ni wachache mno.

Hebu siasa za wanasiasa zisiwafanye mchukue maamuzi mabovu, wale wamelipwa kupigia kampeni suala hilo ili Zanzibar iwe koloni la wakubwa zao waliyowaweka kama vibaraka.
Hamjui kuna mchezo mchafu mnachezewa, waarabu wanaitaka ile ardhi usultani ulipoisha utarudishwa kinamna hiyo.
Au hakukuwa na muungano wa nchi ya kiarabu na Zanzibar uliyopangwa na taifa fulani la waarabu kabla ya Karume kuchange gia angani?
Hebu waulizeni wazee wenu, mnatayarishwa koloni kama lile linalotawaliwa na nchi ya Morocco
 
Kibaya zaidi 75% ya watu wa huko wana asili ya bara, biashara ya utumwa ndiyo imewapeleka huko. Hivyo kuna koo za huku bara zina uhusiano wa karibu na za huko, yaani watu waliyoko kule wengi wametokana na vizazi vya watu wa bara. Wazanzibar kwa asili ni wachache mno.

Hebu siasa za wanasiasa zisiwafanye mchukue maamuzi mabovu, wale wamelipwa kupigia kampeni suala hilo ili Zanzibar iwe koloni la wakubwa zao waliyowaweka kama vibaraka.
Hamjui kuna mchezo mchafu mnachezewa, waarabu wanaitaka ile ardhi usultani ulipoisha utarudishwa kinamna hiyo.
Au hakukuwa na muungano wa nchi ya kiarabu na Zanzibar uliyopangwa na taifa fulani la waarabu kabla ya Karume kuchange gia angani?
Hebu waulizeni wazee wenu, mnatayarishwa koloni kama lile linalotawaliwa na nchi ya Morocco
Nimekwenda oman wapo wenye asili ya bara wengine sana, Yemeni pia wapo, America wapo, United Emirates wapo, Zanzibar wapo, lakini usitufanye sisi tusijatambue three generations au zaidi zimepita Zanzibar, hivyo sio Watanganyika tena, ni wazanzibari, uzanzibari unaweza kuwa wa asili au kizazi tu au wa kuzaliwa, kwa hio tuache tudai nchi yetu, Zanzibar ni nchi ilikuwa huru kabla ya Muungano.

Imefika wakati sasa Zanzibar ina watu zaidi milioni, tunaweza kujilinda, tunaweza kujenga nchi yetu, hivyo ni wakati Zanzibar kurudishiwa uhuru wake, kama muungano, East Africa community itatuunganisha, hata bila ya hivyo, hata huu udugu wetu utakuwepo tu.


Zanzibar kwanza
 
Hebu waulizeni wazee wenu, mnatayarishwa koloni kama lile linalotawaliwa na nchi ya Morocco
Wewe nani anatawaliwa na Morroco?!!Jamhuri ya wath wa Sahrawi iko huru,na Morocco wana tamaa na kuiteka na kuikalia kimabavu nchi hiyo lakini kila mara wanakula kichapo.
JESHI LA SAHARA YA MAGHARIBI.
morocco-polisario2_0.jpg
12799231_962204583826888_5054333812137804164_n.jpg
polisario.jpg
downloadfile-2.jpg
 
Jamhuri ya watu wa Sahrawi sio jamhuri ya kumsukuma mlevi,wamejizatiti kwelikweli na kumfanya mfalme wa Morocco kuvaa bukta na kueneza fitna za kidiplomasia dhidi watu wa Sahrawi.
 
Vingi ya hivyo vitu ulivyo orodhesha kama faida au mtakavyo kua navyo haviingizi PESA instead vinatumia PESA; umejiuliza source of fund ya hivyo vifaida!? Well, ningependa hata mimi kuwaona Wazanzibar mnajitegemea kabla SIJAFA mkuu, I wish the same brother
 
Kibaya zaidi 75% ya watu wa huko wana asili ya bara, biashara ya utumwa ndiyo imewapeleka huko. Hivyo kuna koo za huku bara zina uhusiano wa karibu na za huko, yaani watu waliyoko kule wengi wametokana na vizazi vya watu wa bara. Wazanzibar kwa asili ni wachache mno.

Hebu siasa za wanasiasa zisiwafanye mchukue maamuzi mabovu, wale wamelipwa kupigia kampeni suala hilo ili Zanzibar iwe koloni la wakubwa zao waliyowaweka kama vibaraka.
Hamjui kuna mchezo mchafu mnachezewa, waarabu wanaitaka ile ardhi usultani ulipoisha utarudishwa kinamna hiyo.
Au hakukuwa na muungano wa nchi ya kiarabu na Zanzibar uliyopangwa na taifa fulani la waarabu kabla ya Karume kuchange gia angani?
Hebu waulizeni wazee wenu, mnatayarishwa koloni kama lile linalotawaliwa na nchi ya Morocco


HIZO NI MBINU ZA KANISA NA PROPAGANDA ZAO

Asili ya ugaidi na magaidi duniani
 
Ungekuwa unataka kujua ungeuliza kiungwana, ila hapo nimeona shida yako ni kutaka turushiane kashfa na si kufafanua kiundani kwa kile kila mmoja alichoeleza.

Si mtu wa aina hiyo ya lugha unayoitumia, nikutakie siku njema. Pia usinihusishe na dini nisiyoifuata


Unafuata dini gani kwani hicho ulichokiandika ndio mafundisho ya kanisa , unategemea ujibiwe namna gani ???

AU HUJAMSIKIA LUKUVI AKIONGEA KUHUSU ZANZIBAR NA MUUNGANO KULE KANISANI ??

 
Wenzenu wanazidi kuungana nyie mnafikiria kutengana!! Badala ya kufikiri ni vipi tunaweza kwenda hatua kubwa zaidi katika umoja wa EA tunafikiria kuadd member mwingine Zanzibar!

Hakuna kinachozuia Zanzibar kuendelea ambacho kinakwamishwa na muungano, achilia mbali fikra za jumuiya za misaada.

Nchi inajengwa kupitia rasilimali zake. Leo mafuta yakipatikana Zanzibar yatabaki kuwa ya Zanzibar na hakuna la kubadili hilo. Umoja wetu ndio nguvu yetu, msidanganywe!
Watu wanaungana kwa wema sio kwa ubaya. Mnajiita ndugu zetu kumbe wanafiki, mna hiari kwenda kuchukua sukari Brasil wakati magunia ya sukari Zanzibar yamejaa? Mnataka kuzuia meli za container zisishushe mzigo zanzibar eti zishushe bara kisha mizigo ya Zanzibar itiwe kwenye meli itoke bara ije Zanzibar? ishu sio misaada kutoka nje, na asitusaidie yoyote aliepo nje Zanzibar inaweza kujisaidia wenyewe! tatizo lilokuwepo ni hili koti limekuwa linabana sana tena, Marehemu Karume kashasema likikubana ulivue, lakini viongozi wa Zanzibar wanachaguliwa dodoma, hawataki kulivua!!!! Yaani lile chaguo la wanaCCM zanzibar linapigwa na chini dodoma anachaguliwa wanaemtaka!!! Scotland, ambao wanamuungano mzuri tu wanataka kujitoa, ije kuwa sie mnaotudhulumu? Ushawahi kusikia Ujerumani au Ufaransa anataka kuungana na kufanya nchi moja na jirani yake?

Umelishwa uchafu mkuu!
 
Unafuata dini gani kwani hicho ulichokiandika ndio mafundisho ya kanisa , unategemea ujibiwe namna gani ???

AU HUJAMSIKIA LUKUVI AKIONGEA KUHUSU ZANZIBAR NA MUUNGANO KULE KANISANI ??

Hayo mambo ya Lukuvi sifuatilii, hiyo habari niliyoiandika naijua zaidi ya miaka nane sasa. Mengine wazawa wa kule wamethibitisha wenyewe.

Hayo ya kanisa na Lukuvi siyajui
 
Hayo mambo ya Lukuvi sifuatilii, hiyo habari niliyoiandika naijua zaidi ya miaka nane sasa. Mengine wazawa wa kule wamethibitisha wenyewe.

Hayo ya kanisa na Lukuvi siyajui


Huyo aliyekuambia kuwa kuna wabara walioko Zanzibar ambao wazee wao walikuwa ni watumwa , mwambie akupatie jina la mtu mmoja tu ambaye babu yake alikuwa ni mtumwa Zanzibar,
Kwa mujibu wa kanisa utakuta hao waarabu unaoambiwa siku zote , ujuwe ni waislamu

Kwa mujibu wa vitabu vya kanisa muislamu yeyote awe mweusi kuliko makaa kwao wao ni mwarabu , hii ni mikakati Yao ya kuupiga vita uislamu.


Na J. Hussein


HISTORIA ya Zanzibar kwa kiasi kikubwa imehusishwa na biashara ya utumwa. Bahati mbaya ni kwamba wengi wa waandishi wa historia hiyo wameunasibisha utumwa na Uislamu. Katika makala hii mwandishi wetu SAID MZEE anatuelezea juu ya historia ya utumwa katika Zanzibar.DUNIA imepata kupitiwa na mifumo mingi ya maisha katika mwanadamu kutaka kuishi maisha bora kwa lengo la kuzalisha mali. Moja kati ya njia hizo ni utumwa.

Utumwa ulikuwako katika nchi zote duniani kuanzia za Ulaya, Asia hadi Afrika. Kwa mujibu wa Tarekh wazungu ndio waliokuwa watu wa mwanzo kuwafanya wazungu wenzao kuwa watumwa baadaye wakafuatiwa na Wachina.

Chanzo cha utumwa katika jamii zote kilikuwa aidha kushindwa katika vita, kushindwa kulipa deni unalodaiwa, adhabu kufuatia uhalifu uliotenda n.k.

Wazungu ndio waliokuwa wahalifu wakubwa kabisa katika kuendeleza biashara hii ya utumwa kwa niaba ya msalaba. Kati ya makabila yote ya Kizungu waliotia fora walikuwa ni Waingereza na Wamarekani ambao ni Wakristo wa Kiprotestant na Katoliki ambao leo wanajigamba na kujidai ati ni wao walioondosha utumwa.

Kama tulivyotangulia kusema awali kwamba utumwa ulikuwa ni mfumo wa maisha pale Waingereza walipopendekeza kuondoshwa kwa utumwa ulikuwa ni kwa sababu utumwa haukutia faida tena za kiuchumi na ilibidi ubadilishwe na uzalishaji mali mpya wa kibwanyenye nasio kwa sababu kwamba Wazungu walikuwa na huruma sana na Waafrika.

Kwa njia ya kudau kuondosha utumwa Manuwari na Merikebu za Kiingereza zilidiriki kuchoma na kuteketeza kwa moto madai na majahazi ya wafanya biashara yakiwa na watumwa au la, na matendo yao hayo kubainika na watawala wao. Pengine ajenda ambayo imefichwa hadi leo na Waingereza hao juu ya ukatili wao huo ni kuwa lengo kubwa lilikuwa ni kukata mizizi ya biashara baina ya Afrika Mashariki na nchi za Mashariki ya Bahari ya Hindi.

Kwa kutumia njia hii Waingereza waliweza kuhodhi uchumi wa Afrika ya Mashariki na kuua kabisa biashara baina ya Afrika ya Mashariki na Mashariki ya Bahari ya Hindi biashara ambayo ilishadumu kwa karne nyingi. Wakati Muingereza alidai kupiga vita usafirishaji wa watumwa kutoka Afrika ya Mashariki, upande mwingine aliruhusu uuzaji na uzalishaji mali wa watumwa katika bara la Afrika ya Mashariki na kwa kutenda hivyo aliweza kujinufaisha kisiasa na kiuchumi kupitia biashara hiyo ya watumwa.

Kwa vile Zanzibar ilikuwa ndio kitovu cha biashara katika Afrika ya Mashariki na kati Muingereza aliweza kuuwa uchumi wa Zanzibar na hivyo kumuwiya rahisi kutawala sehemu yote ya Afrika ya Mashariki. Zanzibar iligeuzwa bandari na soko mojawapo maalumu la watumwa, vituo vingine vikiwa sehemu za jirani na visiwa hivi kama vile Bagamoyo na Kilwa.

Pamoja na kwamba Zanzibar ilikuwa ni bandari na soko muhimu la watumwa, hakuna Mzanzibari ambaye alifanywa mtumwa bali watumwa hawa walitoka mabara ama kutokana na kusakwa na wachuuzi wa watumwa wa Kiarabu na wa kienyeji au kutokana na kuwa mateka wa vita baina ya machifu, mapigano baina ya makabila mbalimbali kama vile Wamakonde, Wamakua, Wayao n.k. au ni kutokana na kushindwa nguvu na kutekwa na wenzao.

Kufikia mwaka 1873 Zanzibar ilipiga marufuku biashara ya utumwa lakini cha kushangaza ni kwamba Wareno na Wafaransa waliendelea na biashara hiyo na Muingereza hakunyanyua mkono wkae kuwakemea.

Ingawa sheria ya kukomesha utumwa ilipitishwa rasmi 1873 cha kustaajabisha ni kwamba hadi leo wanasiasa wetu wamekuwa wakiwadanganya wananchi na wageni wanaofika Zanzibar kwamba utumwa uliondoshwa na mapinduzi ya Januari 1964.

Kama neno lenyewe linavyoonyesha, utumwa ni njia mojawapo ya uzalishaji mali ambayo ni kashfa kubwa mtu kunasibishwa nayo na kwa mujibu wa sifa za ubinadamu anayekashifika zaidi ni yule muuzaji wa watumwa hao kuliko watumwa wenyewe, kwani yeye huwa ndio kaonyesha upungufu mkubwa wa kibinadamu kwa kukubali kumuuza binadamu mwenziwe.

Pengine kwa kutambua hili ndio maana Sultan hakutaka kuwaona raia wake wa Zanzibar wakifanywa watumwa. Nchi za Ulaya ambazo leo zinajipa au kupewa sifa za utu bora ndio zinazotumia uzalishaji mali kupitia njia za watumwa na kuyawezesha matabaka ya juu yaliyokuwa yakitawala kujinufaisha kwa kiasi kikubwa. Mfano mzuri wa Waafrika wa Kimarekani (Black American) waliojenga uchumi wa Marekani kwa jasho na damu yao wakati tabaka lao likisehelea katika umasikini.

Wakoloni wote wakiongozwa na Waingereza wamekuwa wakifanya njama za siri na dhahiri za kujifanya wao ni wazuri na kuja kwao Afrika kulikuwa na madhumuni ya kuleta kheri na mafanikio kwa Waafrika pasi na kuwa na lengo jingine lolote.

Njia moja kubwa waliyoitumia ni Makanisa na Mapadri. Wazungu hao walidai kwamba wamekuja kupiga vita ushenzi na kuleta staarabu.

Wakoloni wa Kiingereza mara tu baada ya kuwanyang’anya hatamu wazalia wa Zanzibar na kuuhifadhi utawala wa Kibuu Said walimpa jina ambalo lililokuwa na dhamira ya kuwapa faida zaidi wao.

Waingereza kwa sababu zao waliuita utawala huo kuwa ni wa Waarabu. Lengo la kuuita utawala huo kuwa ni wa Kiarabu lilikuwa ni kuufanya Uislamu uonekane ni mbaya na umekandamiza Waafrika na Wazungu na Ukristo ndio mzuri kwa vile unapiga vita biashara ya watumwa.

Bahati mbaya sana watu wengi hadi hii leo wamenasa katika mtego huo wa Waingereza na wengine pamoja na kusoma kwao kote basi wameshindwa kulielewa lengo na dhamira hii ya Muingereza. Ukweli ni kwamba utumwa ulikuwepo Afrika ya Mashariki hata kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (as) kwa hiyo hata kabla ya kuja Mtume Muhammad (saw) utumwa ulikuwa umeshaota mizizi ulimwenguni, lakini Waingereza na wakoloni wenzao wa Kizungu kwa kutumia Kanisa wakaufanya utumwa umeletwa na Waarabu kwa lengo lile lile la kuonyesha kwamba Uislamu ndio ulioleta utumwa.

Wakati ambao utumwa ulipigwa marufuku Zanzibar, Wareno na Wafaransa walishughulika na biashara ya utumwa katika nchi za Mashariki ya Afrika na kazi hiyo walifanya bila ya kuingiliwa kati na Manowari za Kiingereza zilizowekwa maalum kulinda usafirishaji wa watumwa.

Ukweli huu hausemwi na Muingereza wala vibaraka wake wa Kikristo ingawaje wanafahamu kwamba kulikuwa na Waingereza hapa hapa Zanzibar ambao walikuwa wakifaidika kutokana na jasho la watumwa hao na ndio maana utaona kwamba kilichopigwa marukufu na Wazungu ni usafirishaji wa watumwa na si kumiliki watumwa.

Jambo jingine ambalo Waingereza na vibaraka wao wamesahau kulisema ni kwamba huko kwao pia kulikuwa na utumwa ingawaje hakukuwa na Uislamu. Katika hili Waingereza wanajifanya hawatambui juu ya maafa ya Waafrika wa Afrika Magharibi (Nigeria, Ghana, Liberia) waliopelekwa Marekani ya Kaskazini, Kusini na Caribbean ambako nako hakukuwa na Uislamu. Wazungu walipokwenda Marekani waliwenda kwa niaba ya jina takatifu la Ukristo na kwa niaba ya jina la Msalaba, wakawateketeza wenyeji wa huko na kuwafanya watumwa, lakini hilo leo hawalisemi badala yake wanasingizia Uislamu ndio ulioleta biashara ya utumwa.

Njama za kuufanya Uislamu uonekane mbaya Afrika ilikuwa ni kuleta chuki za kugonganisha vichwa baina ya Wazanzibari kwa Wazanzibari, Watanganyika kwa Watanganyika ili kuweza kuwatawala kwa urahisi na kuweza kusambaza dini yao ya Kikristo.

Hilo ndilo lilikuwa na linaendelea kuwa lengo maalumu la kampeni hiyo, ingawa wengi wa Wazungu hao walikuwa na wanaendelea kuwa hata huyo Mungu mwenyewe hawamuamini bali hutumia Ukristo kuwatawala kimawazo na kiuchumi Waafriak tu. Waingereza hawa na vibaraka wao wamesahau kwamba Christopher Columus aliwateketeza Wahindi Wekundu kwa niaba ya Ukristo na kazi hiyo ovu ikaendelezwa na Waingereza mkoloni hadi leo hajatuambia ni kwa nini aliwateketeza wenyeji wa Australia na New Zealand kwa maradhi mbalimbali. Je, wakati wakifanya hayo nao walikuwa ni Waislamu?

Ni bahati mbaya sana kwamba Wazanzibari badala ya kuamka na kuzitamka mbinu za mkoloni za kutugonganisha vichwa Waislamu kwa Waislamu badala ya kukaa kitako na kujaribu kutatua tofauti zetu za kisiasa na nyingine za kijamii, tumezama katika kuendeleza mifarakano.

Jambo jingine ambalo Muingereza na Kanisa wamesahau kuwaambia Waafrika ni kwamba katika biashara ya utumwa Zanzibar Waislamu hawakufanywa watumwa na wale ambao walisimu walitolewa utumwani. Lakusikitisha ni kuona hata wale waandishi na wataalamu wanaodaiwa kuwa wameendelea wametekwa nyara na tafsiri potofu ya utumwa kama ilivyotolewa na Kanisa.

Uislamu hadi leo unapigwa vita sehemu zote ulimwenguni ingawaje leo hazitumiki sababu za utumwa lakini bado kwa kiasi kikubwa zinanasibishwa na matukio ya utumwa. Ni budi Wazanzibari tukumbuke kwamba kwa kutumia Uislamu badala ya tafsiri ya kitabaka aliyoiandaa yeye mwenyewe Muingereza alifanikiwa kuleta chuki na uhasama baina ya wakazi wa visiwa hivi, wakati mwenyewe akishirikiana na kuuhifadhi utawala huo aliouita wa Kiarabu.

Kwa njia hiyo Muingereza alifaulu kutufanya tukabane roho wenyewe kwa wenyewe na kusahau kumpiga vita adui yetu mkubwa ambaye ni yeye na Kanisa lake, kama alivyofanikiwa leo kutugonganisha vichwa kwa masuala ya kisiasa na kuwaacha maadui wetu wakubwa ukizidi kuiangamiza jamii yetu kwa kasi ya kutisha.
 
Kwa mipaka ya ukoloni eneo la zanzibar ni mpaka bara km 16
Sasa sijui tumejiandaaje kisaikolojia watu wa mzizima Bagamoyo na ukanda wa pwani kiujumla kuwa wazanzibari na ndio sababu hata mchonga aliona mbali kuwa ikulu ya Magogoni ipo zanzibar ndio michakacho ya Dodoma ikaasisiwa.
Tutaonana baadaye nimewapa pakuanzia
 
Vingi ya hivyo vitu ulivyo orodhesha kama faida au mtakavyo kua navyo haviingizi PESA instead vinatumia PESA; umejiuliza source of fund ya hivyo vifaida!? Well, ningependa hata mimi kuwaona Wazanzibar mnajitegemea kabla SIJAFA mkuu, I wish the same brother
Pesa huzaa pesa
 
Back
Top Bottom