Kuna rasilimali ambazo hazipo direct kama vile gas au mafuta, Zanzibar peke yake ni rasilimali, watu pia rasilimali, sasa mkuu kwa nini Hamtaki kupunguza mambo ya Muungano na kila siku mnazidisha?
Sarafu - kwa nini Hamtaki Zanzibar iwe na sarafu yake? Kwa maana mnafaidika.
Michezo - kwa nini mnatumia jina la tánzania katika michezo kimataifa? Kwa maana mnafaidika na kuifunika Zanzibar.
Mikopo - kwa nini Hamtaki suala la mikopo kuwa nje ya Muungano? Kwa maana mnafaidika.
Uhamiaji - uraia--kwa nini Hamtaki Zanzibar iwe na uraia wake, ili kulinda ardhi yake ihali mnajua eneo dogo kama mnavyo sema? Mnafaidika
Anga - kwa nini Hamtaki Zanzibar iwe inaongoza wizara hii nje ya Muungano? Mnafaidika tu.
Ulinzi na usalama - kwa nini Hamtaki kuondoa kwenye orodha ya mambo ya Muungano? Mnasema hatuchangii, Zanzibar kuna zaidi ya 6000 jeshi na usalama kutoka tanganyika, mnafaidika.
Police - kwa nini Hamtaki Zanzibar iwe na police yake, badala ya kung'ania kuwa muungano? Mnafaidika.
Wazanzibar wanautaka Muungano lakini sio huu wa kinyonyaji, hao wajitao viongozi wanao sema unatusaidia ni wanafiki, mbona Wazanzibar wanalalamika? Kama asilimia 89 za maoni ya katiba nakukumbusha, tulitaka Muungano wa mkataba. [emoji111]