Muuguzi KCMC auawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali uchochoroni

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Muuguzi wa hospitali ya KCMC Moshi Khudheifa Changa (26)

Akitoa taarifaa hiyo kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Simoni Maigwa amesema kuwa walio kamatwa ni watuhumiwa watatu wanaume na wanawake wawili (majina yao yamehifadhiwa kwa sababu wengine wanaendelea kutafutwa) kwa tuhuma za kusababisha mauaji ya mfanyakazi huyo tukio lililotokea mtaa wa Malindi, kata ya Mawenzi, wilaya ya Moshi Manispaa usiku wa kuamkia Julai 2, 2023.

Kamanda Maigwa amedai kuwa siku ya tukio hilo marehemu alikuwa akipita eneo hilo kwenye njia ya uchochoro ndipo alipo vamiwa na watu hao kwa nia ya kumpora mali alizonazo.

1688503716404.png

"Katika purukushani hizo marehemu alijeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye mbavu upande wa kushoto usawa wa moyo na kupelekea kifo chakepapo hapo." alisema Kamanda Maigwa.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema lilifanikiwa kupata taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao walitoweka baada ya kutenda unyama huo ambapo Watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Rufaa KCMC Moshi kwa uchunguzi zaidi.
 
Daaaaa

Ulikosea ,ulimchoma wann tulikuwa tunachukua vituu TU ,mwanaa

Umeharibu mwanaaa
Asilimia kubwa ya matukio ya kuuawa kwa mtu anayekabwa ni kwa sababu ya kutaka kujitetea au kuleta ubishi wakati wa tukio la kunyang'anywa,au wengine kupiga kelele Kali za kuibiwa,ndiyo wanakuzima. Wahuni wa kibongo siyo wauaji endapo hautaleta purukushani au kuwaletea za kuleta. Ukiwa mtata ndiyo unakuta wahuni wanazamisha bisibisi kwenye mbavu changa,unakufa.

Niliwahi kumpoteza mshikaji kwa sababu ya kuwavimbia wahuni wasimuibie simu yake,ilikuwa usiku wa manane anatoka kulewa akijichanganya kupita mitaa ya wahuni.

Nishawahi kukutana na wahuni mitaa ya kizinga wakanibananisha mbele na nyuma Wana panga,visu na bisibisi. Ningeweza kujitetea ila niliona uhai ni Bora kuliko simu nikawaambia wazee chukueni simu hii hapa, wakaniangalia chini wakaniambia acha na viatu nikaona siyo kesi nikavua wakanitengenezea njia bila kunigusa nikaishia zangu.

Hatujui kilichotokea kwa marehemu wakati wa tukio,ila kwenye matukio ya usiku Ni heri kuepusha Shari kwa kuwaacha wachukue wanachotaka ila wakuachie uhai tu,coz tuna uhai mmoja na tukifa haturudi tena.

Maehemu kafa akiwa mdogo Sana,hajafaidi ajira. Apumzike kwa amani!!
 
Asilimia kubwa ya matukio ya kuuawa kwa mtu anayekabwa ni kwa sababu ya kutaka kujitetea au kuleta ubishi wakati wa tukio la kunyang'anywa,au wengine kupiga kelele Kali za kuibiwa...
Unavyojaribu kuwaongelea kama watu wa maana, Inaelekea hata wakitaka kukupenya huna noma, unachuma mboga tu ile kiroho safi ili mradi wasikuumize!!
 
Huko kwenye matusi umeenda mbali Sana,Sina haja ya kukurudishia tusi.

Point yangu kwa mwenye akili ni rahisi kuielewa.

Kwa kifupi namaanisha,kwenye matukio ya kukutana na wahuni wakataka kukubananisha wakuibie Ni vema tu ukawaachia,maana Mara nyingi wanalenga kukuibia hela na simu alafu wanatokomea.

Kuna scenario Kama hii ya muuguzi wa KCMC, ilitokea kwa mwanafunzi wa Kampala University aliuawa kwa sababu Kama hii,wahuni walimkaba akaona wacha akaparangane nao. Wakamzima mazima. Kuna muda maisha ni Bora kuliko material things. Tikiibiwa tutanunua vipya,vipi uhai?

Hata jambazi akiingia ndani ukijifanya mtata Sana ndiyo anakuzima,ila ukijifanya ewala na kuwachia wachukue wanachotaka, watapiga mikwara tu na kuiba wanachotaka lakini hawaui mtu.

Uhai ni Bora kuliko vitu,na hakuna kaburi la mjinga,hiyo ndiyo ilikiwa point yangu,siyo kuwatukuza wezi Kama ulivyodhani nakuishia kunitukana.
 
ukiona umekiepuka kifo jua siku zako za kufa ziko mbali unaweza ukawa mpole nabado ukaihama dunia
Ni sahihi,ila Kuna vifo vingine vinahepukika. Kifo ni kama ajali tu,Kuna mwendo unaona kabisa hapa dereva anaweza kutumwaga,ila ajali ikitokea watu wakafa mnamsingizia Mungu ndiyo amepanga.Kuna muda unajua kabisa hii njia na huu muda siyo rafiki,ila unaamua kusema potelea mbali nitajua huko huko mbele,siwezi kujizungusha njia kubwa yenye watu wengi kisa nitachelewa kufika home. Ukikutana na wahuni unasema Mungu amepanga,siku zake zilifika tu.

Huo mtaa wa malindi,mida ya usiku unakuwa siyo eneo salama kwa wanaopita.
 
Hiyo malindi ndio Njoro ya zamani, hivi kweli police wale wa mafunzo wanavyotembeaga moshi usiku hapo ni sehem ya kushindwa kupadhibiti kwel?
Katikati ya mji mtu anaporwa ?
 
Asilimia kubwa ya matukio ya kuuawa kwa mtu anayekabwa ni kwa sababu ya kutaka kujitetea au kuleta ubishi wakati wa tukio la kunyang'anywa,au wengine kupiga kelele Kali za kuibiwa,ndiyo wanakuzima. Wahuni wa kibongo siyo wauaji endapo hautaleta purukushani au kuwaletea za kuleta. Ukiwa mtata ndiyo unakuta wahuni wanazamisha bisibisi kwenye mbavu changa,unakufa.

Niliwahi kumpoteza mshikaji kwa sababu ya kuwavimbia wahuni wasimuibie simu yake,ilikuwa usiku wa manane anatoka kulewa akijichanganya kupita mitaa ya wahuni.

Nishawahi kukutana na wahuni mitaa ya kizinga wakanibananisha mbele na nyuma Wana panga,visu na bisibisi. Ningeweza kujitetea ila niliona uhai ni Bora kuliko simu nikawaambia wazee chukueni simu hii hapa, wakaniangalia chini wakaniambia acha na viatu nikaona siyo kesi nikavua wakanitengenezea njia bila kunigusa nikaishia zangu.

Hatujui kilichotokea kwa marehemu wakati wa tukio,ila kwenye matukio ya usiku Ni heri kuepusha Shari kwa kuwaacha wachukue wanachotaka ila wakuachie uhai tu,coz tuna uhai mmoja na tukifa haturudi tena.

Maehemu kafa akiwa mdogo Sana,hajafaidi ajira. Apumzike kwa amani!!
Bora umesema kabisaa, vibaka wa bongo sio wauaji ukiwapa wanachotakaaa, ila ukileta ubishii, unapewa beto ya tumbooo.

Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Muuguzi wa hospitali ya KCMC Moshi Khudheifa Changa (26)

Akitoa taarifaa hiyo kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Simoni Maigwa amesema kuwa walio kamatwa ni watuhumiwa watatu wanaume na wanawake wawili (majina yao yamehifadhiwa kwa sababu wengine wanaendelea kutafutwa) kwa tuhuma za kusababisha mauaji ya mfanyakazi huyo tukio lililotokea mtaa wa Malindi, kata ya Mawenzi, wilaya ya Moshi Manispaa usiku wa kuamkia Julai 2, 2023.

Kamanda Maigwa amedai kuwa siku ya tukio hilo marehemu alikuwa akipita eneo hilo kwenye njia ya uchochoro ndipo alipo vamiwa na watu hao kwa nia ya kumpora mali alizonazo.

"Katika purukushani hizo marehemu alijeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye mbavu upande wa kushoto usawa wa moyo na kupelekea kifo chakepapo hapo." alisema Kamanda Maigwa.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema lilifanikiwa kupata taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao walitoweka baada ya kutenda unyama huo ambapo Watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Rufaa KCMC Moshi kwa uchunguzi zaidi.
Mungu anisamehe ila sidhani marehemu kama amewahi kuishi Dar.

Mm nimevamiwa Mara 3 sijawahi kubisha kutoa chochote nilichonacho.

Maana sina sababu
 
Huko kwenye matusi umeenda mbali Sana,Sina haja ya kukurudishia tusi.

Point yangu kwa mwenye akili ni rahisi kuielewa.

Kwa kifupi namaanisha,kwenye matukio ya kukutana na wahuni wakataka kukubananisha wakuibie Ni vema tu ukawaachia,maana Mara nyingi wanalenga kukuibia hela na simu alafu wanatokomea.

Kuna scenario Kama hii ya muuguzi wa KCMC, ilitokea kwa mwanafunzi wa Kampala University aliuawa kwa sababu Kama hii,wahuni walimkaba akaona wacha akaparangane nao. Wakamzima mazima. Kuna muda maisha ni Bora kuliko material things. Tikiibiwa tutanunua vipya,vipi uhai?

Hata jambazi akiingia ndani ukijifanya mtata Sana ndiyo anakuzima,ila ukijifanya ewala na kuwachia wachukue wanachotaka, watapiga mikwara tu na kuiba wanachotaka lakini hawaui mtu.

Uhai ni Bora kuliko vitu,na hakuna kaburi la mjinga,hiyo ndiyo ilikiwa point yangu,siyo kuwatukuza wezi Kama ulivyodhani nakuishia kunitukana.
Sikiliza, usidhani hatuwajui vibaka. Hao siyo wahuni ni vibaka. Usidhani hao ni mafala, kwamba wakuibie halafu wakuache ili baadaye uje uwasumbue wakati hapo walipofanyia hilo tukio ni maskani yao.
Unavyoongea utadhani wewe ni mmoja wa hao vibaka kwa jinsi unavyohitimisha kuwa ni sababu alijifanya kubishana nao wakati taarifa haijaongelea hicho kitu.
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Muuguzi wa hospitali ya KCMC Moshi Khudheifa Changa (26)

Akitoa taarifaa hiyo kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Simoni Maigwa amesema kuwa walio kamatwa ni watuhumiwa watatu wanaume na wanawake wawili (majina yao yamehifadhiwa kwa sababu wengine wanaendelea kutafutwa) kwa tuhuma za kusababisha mauaji ya mfanyakazi huyo tukio lililotokea mtaa wa Malindi, kata ya Mawenzi, wilaya ya Moshi Manispaa usiku wa kuamkia Julai 2, 2023.

Kamanda Maigwa amedai kuwa siku ya tukio hilo marehemu alikuwa akipita eneo hilo kwenye njia ya uchochoro ndipo alipo vamiwa na watu hao kwa nia ya kumpora mali alizonazo.

"Katika purukushani hizo marehemu alijeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye mbavu upande wa kushoto usawa wa moyo na kupelekea kifo chakepapo hapo." alisema Kamanda Maigwa.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema lilifanikiwa kupata taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao walitoweka baada ya kutenda unyama huo ambapo Watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Rufaa KCMC Moshi kwa uchunguzi zaidi.
Apumzike kwa Amani! Damu na nguvu kazi changa kabisa, inasikitisha!
 
Huko kwenye matusi umeenda mbali Sana,Sina haja ya kukurudishia tusi.

Point yangu kwa mwenye akili ni rahisi kuielewa.

Kwa kifupi namaanisha,kwenye matukio ya kukutana na wahuni wakataka kukubananisha wakuibie Ni vema tu ukawaachia,maana Mara nyingi wanalenga kukuibia hela na simu alafu wanatokomea...
Wenye akili tumekuelewa, kuna dogo pia walimdaka hapo Malindi wanataka pesa na vitu aliwaachia

Hapo malindi unaenda kununua chips anakuja mwizi anaku search, watu wengi hapo ni wezi na wanajuana vizuri. Sikuwa napenda kutembea mtaa huo usiku
 
Back
Top Bottom