Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Kanda Maalum ya Uwekezaji na Uchumi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

MBUNGE EDWARD LEKAITA AKICHANGIA MSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA KANDA MAALUM YA UWEKEZAJI (MAUZO YA NJE) NA UCHUMI

Mhe. Edward Ole Lekaita akichangia Bungeni jijini Dodoma katika Mswada wa Mabadiriko ya Sheria ya Kanda Maalum ya Uwekezaji na Mauzo Nje ya Nchi na Mswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Kanda Maalum ya Kiuchumi iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bungeni Dodoma.

"Bunge lilipitisha Sheria mpya baada ya mjadala wa Wabunge kutaka Tume Mpya ya Mipango ya Nchi tulete. Mwezi Juni 2023 tulibadirisha tulitunga Sheria mpya ambapo Kifungu cha tatu kinasema Tume itaundwa na Mheshimiwa Rais na itakuwa na wajumbe ambaye mmoja ni Waziri wa Mipango na Maendeleo ya Taifa" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Baada ya Bunge kupitisha Mabadiliko ya Sheria tulijua wazi kuna Mabadiliko ya Serikali. Mheshimiwa Rais tarehe 22 Juni, 2023 kupitia gazeti la Serikali aliunda Wizara mpya ya Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mipango ambaye Prof. Kitila Mkumbo aliteuliwa kuwa Waziri wake" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Baada ya Mabadiliko ya Sheria ni mchakato, Bunge kwasababu ya kuwa na Wizara Mpya ilibidi na sisi tubadirishe kanuni za Bunge kupitia Kamati ya Bunge ya Kanuni ili kupanga Wizara pale kwenye Kamati na Majukumu ya Kamati" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameleta Mabadiriko ya Sheria mbili (The Export Processing Zones Act). Mabadiliko haya ni madogo sana, yanaainisha tu Majukumu ya Waziri wa Viwanda kwenda kwa Waziri wa Uwekezaji" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
 

Attachments

  • IMG-20211013-WA0080.jpg
    IMG-20211013-WA0080.jpg
    60.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom