Serikali inapaswa kuachana na Sheria na Sera za kunyang'anya watu Magari na Mifugo katika maeneo ya uhifadhi, ni sheria za kikoloni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE. EDWARD LEKAITA AISHAURI SERIKALI KUACHANA NA SHERIA ZA KUNYANG'ANYA MIFUGO KWENYE UHIFADHI

Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mhe. Edward Ole Lekaita amesema Wizara ya Maliasili na Utalii inapaswa kuachana na Sheria na Sera zilizopo za kunyang'anya watu Magari na Mifugo yao katika maeneo ya uhifadhi kwani hizo ni sheria za kikoloni

"Nampongeza Rais Samia kwa kupitia filamu ya Royal Tour watalii wameongezeka sana. Nampongeza Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kazi nzuri wanayoifanya" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Utalii na uhifadhi ni vitu viwili tofauti ila vinasaidia kuiongezea nchi mapato na kufungua nchi yetu. Uhifadhi ndiyo Hardcore ya Utalii na Utalii ndiyo Softpart (Business Element). Mtu anayelinda maeneo ambaye ni Mtaalamu wa Wanyamapori, anayepambana na majangiri, huyu huyu mtu ndiyo aendeeshe Utalii wetu? Hapana siamini hivyo?" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Waziri wa Maliasili na Utalii tengeneza timu zako, iwepo timu inayosimamia Utalii pekee yake na timu ambayo inafanya mambo ya uhifadhi. Jeshi Usu wanatakiwa wapambane na majangili, mimea vamizi, waandike vitabu ili wajaribu kuitangaza nchi yetu" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Waziri umesema Wananchi ni wahifadhi namba moja na watu wa hifadhi watapimwa kutokana na wanachosema Wananchi juu yao. Waziri hizi kauli mbili ukizishikilia unaweza kuwa Waziri bora ambaye hajawahi kutokea tangu nchi ipate Uhuru" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Ukitazama mahusiano kati ya wananchi na wanyamapori maeneo ya hifadhi ni mabaya mno. Ilani ya CCM 2020-2025 inasema: "Kuimarisha mahusiano kati ya maeneo ya hifadhi na wananchi na kulinda mali za wananchi na wananchi wenyewe, kutoa elimu na kulinda maslahi ya wananchi" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Katika maeneo ambayo bado tuna mambo ya ukoloni ni eneo la Utalii na uhifadhi. Sheria ya Uhifadhi ya Fauna mwaka 1951 ina mambo kunyang'anywa Magari, Mifugo ya wananchi pale wanapokuwa wameingia kwenye hifadhi zetu. Forfeiture (Kunyang'anywa) ilianza tangu kipindi cha mkoloni" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Waziri wa Maliasili na Utalii ni lazima hizi sheria na Sera tuziboreshe ambazo zinaendelea kutesa watu wetu. Kuingia kwenye hifadhi ni kosa lakini isiwe sababu ya kumfanya mtu awe masikini. Nakubaliana na Conservation for people and by the People" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Hifadhi ni kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi. Ng'ombe akikamatwa anachajiwa laki moja kwa Ng'ombe mmoja. Bunge lilishasema kiwango cha juu na cha chini cha faini. Unatoza faini kutokana na kosa. Haiwezekani Ng'ombe anauzwa kwa laki moja na nusu halafu mnatoza laki moja kwa faini. Haiwezekani!" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Kuna Ng'ombe nyingi zimekamatwa na watu wameshinda kesi mahakamani lakini mpaka leo wananchi hawajapata Mifugo yao. Waziri na timu yako mliangalie hili vizuri na mtengeneze mahusiano mazuri na wananchi" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Waziri ukipata ripoti za Wataalam wa Maliasili na Utalii pia njoo maeneo ya uhifadhi uongee na wananchi, utanufaika zaidi kwa kusikia wananchi wanasema nini kama ulivyofanya Serengeti" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-06-05 at 22.43.47(1).mp4
    56.6 MB

Similar Discussions

Back
Top Bottom