PreGE2025 Mussa Zungu: Rais Samia amejivua mamlaka ya kupendekeza Mwenyekiti wa Tume, amewarudisha Wapinzani wote waliokimbia Nchi

PreGE2025 Mussa Zungu: Rais Samia amejivua mamlaka ya kupendekeza Mwenyekiti wa Tume, amewarudisha Wapinzani wote waliokimbia Nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chawa watupu wajitokeza soko la Vingunguti

Alhad Mussa Salum Leo tarehe 22 mei 2025, imefanya ziara ya kutembelea soko la kisasa la nyama choma la Kumbilamoto lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam Tanzania
1748086456101.jpeg

Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), chini ya Mwenyekiti wake Dr. Alhad Mussa Salum Leo tarehe 22 mei 2025, imefanya ziara ya kutembelea soko la kisasa la nyama choma la Kumbilamoto lililopo Vingunguti, kwa lengo la kujionea maendeleo ya mradi huo na kutambua mafanikio ya serikali katika kuboresha maisha ya wananchi.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa JMAT, Dr. Alhad amesema

Tunashukuru kualikwa kutembelea mradi huu wa kimkakati na wa kombozi kwa wananchi. Maendeleo tuliyoyaona hapa yametufurahisha sana. Tumeridhika kuona kuwa wananchi wameondokana na adha walizokuwa wakizipata wakati wa jua kali na mvua. Tunatoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka mazingira bora ya kazi kwa watu wa kipato cha chini.”

Aidha, JMAT imesisitiza kuwa kusaidia kazi za mikono kwa wananchi ni njia madhubuti ya kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, huku ikitoa wito kwa watanzania kuendeleza mshikamano na kumuomba Mungu aendelee kuilinda nchi kwa amani na utulivu ili kazi iendelee kufanyika kwa mafanikio.

Katika ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya masoko huku akimpongeza Mkurugenzi wa Jiji hili Ndugu Elihuruma Mabelya, kwa kusimamia na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa viwango vya kisasa.

Soko hilo la kisasa linategemea kuwa na zaidi ya wafanyabiashara 232, wakiwemo wauzaji wa nyama choma, mama lishe, wauzaji wa vinywaji, mbogamboga na viungo. Soko hilo linatarajiwa kuongeza mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa wastani wa shilingi milioni 11 kila mwezi, ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 100 kwa mwaka. Ujenzi wa soko hili umegharimu kiasi cha shilingi milioni 700.
 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu akiongea na wananchi wa Dar es Salaam katika Hagla ya uzinduzi wa soko la Nyama choma la Kumbilamoto lililopo Vingunguti jijini hapo amesema:

"Rais Samia amejivua mamlaka ya kupendekeza Mwenyekiti wa Tume, hayo yatafanywa na Kamati Maalumu" na kusisitiza kuwa "hilo ni jambo kubwa sana ambalo Rais amelifanya"

Ameongeza pia; "Rais Samia amewarudisha na kuwakaribisha Wapinzani wote waliokimbia Nchi kwa kuogopa ili warudi wajenge Taifa pamoja, niwaombe sana Wapinzani, ndugu zetu ambao tulikuwa nao Bungeni wao wanajua hakuna Uchaguzi mgumu kama wa 2015 wakati Tume haikuwa na maboresho kama hii mpya"

"Wapinzani waliingia Bungeni 112, CHADEMA 69, CUF 41, NCCR Mageuzi 1 na ACT Wazalendo 1"

Huyu kikongwe huwa, natamani, nimpate nimchape nao,style ya, "back breaking" Mpaka ajambe mishuzi, yote
 
"Rais Samia amejivua mamlaka ya kupendekeza Mwenyekiti wa Tume, hayo yatafanywa na Kamati Maalumu"
Hiyo kamati maalum wajumbe wake wanapatikana vipi?

Ikiwa imesheheni machawa wa ccm itakuwa haina maana
 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu akiongea na wananchi wa Dar es Salaam katika Hagla ya uzinduzi wa soko la Nyama choma la Kumbilamoto lililopo Vingunguti jijini hapo amesema:

"Rais Samia amejivua mamlaka ya kupendekeza Mwenyekiti wa Tume, hayo yatafanywa na Kamati Maalumu" na kusisitiza kuwa "hilo ni jambo kubwa sana ambalo Rais amelifanya"

Ameongeza pia; "Rais Samia amewarudisha na kuwakaribisha Wapinzani wote waliokimbia Nchi kwa kuogopa ili warudi wajenge Taifa pamoja, niwaombe sana Wapinzani, ndugu zetu ambao tulikuwa nao Bungeni wao wanajua hakuna Uchaguzi mgumu kama wa 2015 wakati Tume haikuwa na maboresho kama hii mpya"

"Wapinzani waliingia Bungeni 112, CHADEMA 69, CUF 41, NCCR Mageuzi 1 na ACT Wazalendo 1"

sijaelewa, amemrudisha nani? au anaonngea kama hadithi ya kichwa kinongea wakati wa ajali kikieema kama siyo kutumia akili ningelikufa (wakati kichwa kiko separate na kiwiliwili) johnthebaptist
 
Zungu wa mama analeta porojo!
No Reforms No Election 🔥!
 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu akiongea na wananchi wa Dar es Salaam katika Hagla ya uzinduzi wa soko la Nyama choma la Kumbilamoto lililopo Vingunguti jijini hapo amesema:

"Rais Samia amejivua mamlaka ya kupendekeza Mwenyekiti wa Tume, hayo yatafanywa na Kamati Maalumu" na kusisitiza kuwa "hilo ni jambo kubwa sana ambalo Rais amelifanya"

Ameongeza pia; "Rais Samia amewarudisha na kuwakaribisha Wapinzani wote waliokimbia Nchi kwa kuogopa ili warudi wajenge Taifa pamoja, niwaombe sana Wapinzani, ndugu zetu ambao tulikuwa nao Bungeni wao wanajua hakuna Uchaguzi mgumu kama wa 2015 wakati Tume haikuwa na maboresho kama hii mpya"

"Wapinzani waliingia Bungeni 112, CHADEMA 69, CUF 41, NCCR Mageuzi 1 na ACT Wazalendo 1"

MUUNDO WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI

Tume inaundwa na Wajumbe saba (7), miongoni mwao wakiwemo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambao wanapaswa kuwa na sifa ya Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani. Katika Uteuzi, Rais anazingatia kuwa endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano. Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Kifungu cha 5 cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Na. 2 ya Mwaka 2024..

Aidha, Mjumbe mmoja anateuliwa kutoka miongoni mwa Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) na Wajumbe wengine wanne (4) wanatakiwa wawe na uelewa wa kutosha kuhusiana na kusimamia nakuendesha Uchaguzi wa Wabunge au sifa nyingine kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano atakavyoona inafaa kwa ajili ya kuendesha shughuli za Tume.

Hiyo Kamati Maalum anayozungumzia Mheshimiwa ni hii hapa:

Kamati ya Usaili 9.-(1) Wakati wowote inapobidi kuteuliwa mjumbe au wajumbe wa Tume, Rais ataitisha Kamati ya Usaili. (2) Kamati itakayoitishwa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni Mwenyekiti; (b) Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti; (c) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; na (d) mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais kwa kuzingatia jinsia. (3) Katibu wa Kamati ya Usaili atakuwa afisa mwandamizi katika utumishi wa umma atakayeteuliwa na Rais.

Mbona hazungumzii uchaguzi wa 2020?

Amandla...
 
Kajivuaje hayo mamlaka ambayo yapo kisheria?

Watu wasio na akili ni shida sana kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom