Museveni kwisha habari yake, sasa ategemea Jeshi na Polisi tu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,654
218,143
Huyu mzee tulimuonya tangu mapema sana kwamba miaka aliyoingoza Uganda inatosha , mwaka ujao asigombee tena , kwa bahati mbaya sana akapuuza.

Akaanza Juhudi za kishetani za kupunguza miaka yake kwa kushrikiana na Maaskofu njaa , eti umri wake ulikosewa ! baadaye akaamua kuondoa vifungu vya katiba vilivyomtaka mtu aliyefikisha umri wa miaka 75 kutogombea Urais wa Uganda ili agombee hadi atakapokuwa na mkongojo .

Lakini sasa hali imembadilikia , Waganda hawataki hata kumsikia , achilia mbali kumuona , Mzee ushawishi wake umepukutika mithili ya majani ya mti uliokauka, hawezi kushinda Urais labda apore kama wanavyofanya madikteta wengine wa kiafrika .

Poor Museveni

FB_IMG_1609354933422.jpg
 
Back
Top Bottom