Museveni anapogonganisha vichwa vya marais wenzake

Museveni anapogonganisha vichwa vya marais wenzake

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
kabila%20na%20wengine.jpg
6.jpg

Rias wa Uganda, Yoweri Museven (kulia), akimwagiza Katibu Mkuu wa SADC, Thomaz Salomao (aliyesimama)kupeleka nakala ya hotuba yake kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC, jijini Dar es Salaam jana. Museveni alibainisha chanzo cha migogoro ya vita DRC kwenye mkutano huo. Kushoto ni mwenyekiti wao, Rais Jakaya Mrisho Kikwete na katikati ni Mwenyekiti wa SADC, Rais wa Msumbuji, Armando Guebuza.

Katika picha viongozi wenzake wanaonekana kusoma kitu kingine kinyume cha anachosema Yowel Museven kuliko anachokiongea.
 
Kuna wanaoneemeka na yanayoendelea DRC Congo...inawezekana na yeye pia ni muhusika.... ingawa kwenye hoja yake ya kwamba UN Troops ni watalii kule Congo, Museveni yuko sahihi.
 
Kuna wanaoneemeka na yanayoendelea DRC Congo...inawezekana na yeye pia ni muhusika.... ingawa kwenye hoja yake ya kwamba UN Troops ni watalii kule Congo, Museveni yuko sahihi.

Hali ndiyo hiyo, lakini picha hii inazungumza zaidi ya maneno, kwani Kikwete hakuweza kuficha hisia zake kwa namna anavyomtazama Yowel akiongea, hali kadhalika mwenyekiti wao Rais wa Msumbiji anaonekana kujawa na mengi kichwani hadi kuduwaa katika matamshi hayo ya Museven. Mkuktano huo umewakutanisha mahasimu wakubwa Kabila na Museven.
 
Jambo hili ni very serious, lakini mbona baba yetu wa Magogoni anatabasamu? Kulikoni?
 
Kuna wanaoneemeka na yanayoendelea DRC Congo...inawezekana na yeye pia ni muhusika.... ingawa kwenye hoja yake ya kwamba UN Troops ni watalii kule Congo, Museveni yuko sahihi.

Yoweri Kaguta Museven ni mmoja wa wanaofaidika na rasilimali za DRC hilo halina ubishi hata kidogo.

Yoweri Kaguta Museven ni mmoja wa wanaofaidika na rasilimali za DRC hilo halina ubishi hata kidogo.

6.jpg

Unaona katika picha anavyomkejeli kwa kumpelekea Kabila nakala ya hotuba yake huko akifanya masikhala.
 
Kuna wanaoneemeka na yanayoendelea DRC Congo...inawezekana na yeye pia ni muhusika.... ingawa kwenye hoja yake ya kwamba UN Troops ni watalii kule Congo, Museveni yuko sahihi.

Anayesema hayo as if yeye hausiki moja kwa moja na hali ya kusikitisha ndani ya DRC! M7 alitoa logistic support kwa M23 na Kagame ka-contribute wanajeshi zaidi ya 1000+. Leo hii wanataka kuhadaa DUNIA.
 
Kiboko yake Angola,Zimbabwe na Namibia. Waliyafurusha majeshi ya Uganda na Rwanda kama paka wanga!
 
Back
Top Bottom