Museveni amteua Mke wake kuwa Waziri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Museveni amteua Mke wake kuwa Waziri!

Discussion in 'International Forum' started by MzalendoHalisi, Feb 17, 2009.

 1. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Museveni (M7) amekaa ktk madaraka miaka 24!

  Kweli Power Corrupts!!

  Amini usiamini...M7 amamteua mke wake kuwa waziri atakayeshughulika na eneo la Karamajon!

  Source: BBC
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  - Katiba ya Uganda inasemaje kuhusu hilo?

  - If permitted by the Law of the Land, we have got not to show any concern (right?)
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Let the king rule
   
 4. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Sasa Tatizo hapo ni nini?, Hivi Uganda ile ya enzi za mauaji ya kila siku miaka ya themanini sasa imetulia kiasi ukiondoa kasoro ndogndogo za LRA(lord Resistance Army) hakuna matatizo makubwa. M7 kaweza kuifanya nchi ikawa na heshma na utawala wa sheria. sioni kama ni kosa kwa kiongozi mzuri kukaa madarakani hata umri wake wote.

  Kumteuwa Mkewe kuwa waziri si kosa kama mke anavyovigezo stahili vya kuweza kufanya kazi hiyo na katiba inaruhusu. umewaona vipi wake za wenzio ukawateua uwaziri ushindwe kumuona mama watoto?.

  Hongera M7 kwani "charity begins at home".
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama wadau wengine walivyo sema, nafikiri si tatizo kubwa sana kukaa madarakani muda mrefu kama ni kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Ofcourse kwa M7 nafikiri, kuna kipindi fulani alibadirisha katiba ili kumruhusu kugombea urais kwa vipindi zaid ya viwili, sasa maadamu nilo liliridhiwa na bunge na wananchi wa Ug, hakuna tatizo hapo.

  Na pia kumchagua mkewe kuwa waziri, sidhani kama kuna shida kama mama huyo ana sifa zinazotakiwa kwa nafasi hiyo, na pia kama katiba, sheria na taratibu nyingine zinaruhusu hilo.
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mrs Janet Museveni ni mbunge wa jimbo la Ruhaama tena kwa kugombea (alipata ushindi wa kishindo)na si kuteuliwa.Anazo sifa stahiki kupata huo uwaziri.

  Inataka moyo hata hivyo kwa Rais kufumba macho na kumpa nafasi mkewe maana kibinadamu watu lazima wataweka maswali na manung'uniko.

  Tumpe hongera zake tu.
   
 7. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ni poa kumpa wife cheo hata ingekuwa vaisi presida. Suala ni uwajibikaji. Je amtamtendea haki akiboronga? Na akiboronga akawa jasiri kumtimua ndoa itasimama upande upi?

  Wengi wangependa kufanya hivyo lakini .......Ndoa nayo muhimu.
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ni kweli ndugu yangu ulichosema kuwa ndoa ni Muhimu! Lkn mimi nimesema kama Katiba yao inaruhusu Rais kumteua closely related person kny such post basi haina neno, manake itakuwa (katiba) imeangalia vilevile suala la Conflict of Interest (Mgongano wa maslahi) ambayo ni big issue hata kama mtu huyo ana sifa zinazotakiwa! Kny issue ya kitaifa, ndoa comes later mkuu hasa katika issue za kisiasa!
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Katiba kabadilisha yeye. Labda si tatizo huko 3rd world kwa akina M7, Hugo Rafael Chávez Frías, Gadaffi, Nguema na wachovu wengine
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mimi nachanganyikiwa hapa, maana naona M7 na Mugabe ngoma droo.
  Huyu jamaa si ndio alitaka kuwa Rais wa kwanza EA?
  Angetuteulia mkewe kuwa gavana wa suala lolote EA ingekaaje?
  Power corrupts kweli kweli,mzee M7 si ajabu hajioni masikini.
  Kwa misingi tu ya utawala bora huyu mama sasa ni makamu wa Rais.
  Mbishie hata ukiwa waziri na utaonja joto ya jiwe, sikapewa rungu?
  Ni pale Lucy Kibaki akipewa uwaziri , uuuwi sijui itakuwaje!
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ushindi wa Kishindo??????

  Hata Mama Salma akigombea Temeke leo je hatapata ushindi wa kishindo??

  I think kumteua mke Waziri..hata kama ana uwezo is it wrong! Nadhani duniani she is the only 1st lady amabe pia ni waziri!

  Role ya 1st Lady atafanya lini?

  Je Uganda hakuna waengine wanaofaa kuwa mawaziri??

  Majority ya waganda hawampendi M7 sema ni dictator!

  Kumbuka alihonga 4 m Tshs kwa kila mbunge ili wabadili katiba azidi kuwa raisi!

  Wizi wa kura kwake ni jambo la kawaida..na dhani he is the most skilled president ktk wizi wa kura EA!

  Angalia he was the only President EA kutambua matokeo ya Kibaki..yet hata Kivuitu alionyesha wasi2!

  sasa amemteau mke waziri, je kesho akiwateua watoto wake maziri, na wakuu wa mashiriki..hata wana uwezo..is it fair kama raisi?

  Huyu mama angeperfom tu role ya 1st Lady...inatosha awaachie wengine uwaziri!

  Je is it possible kusema hii appoitment sii bedroom decision??
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mimi naona wengine hatuoni uzito wa jamabo hili kwa sababu halitugusi. Lakini kama kweli tunataka watu wafanye kazi, na kama watu wenyewe wanaujua uzito wa kazi zenyewe kama alivoysema Pinda kuhusu nafasi ya uwaziri mkuu, basi ningewashauri ndugu zake rais wafanye kazi nyingine wakati yeye akiwa madarakani. Kama alivyosema M/Halisi hapo juu haifai first lady kujiingiza kwenye siasa kiasi hicho kwani ikitokea tatizo rais naye atakuwa matatani. Mfano, ingetokea kwamba rais ana watoto kama 10 ambao ni wabunge na pia anatokea kwenye ukoo mkubwa ambao una wabunge wengi (wengine wa kuteuliwa) na ana wake kama 4 na wote ni wabunge akaunda baraza la mawaziri la ukoo, tutamlaumu? Ni ajabu kwa nchi nyingi za Africa kuongelea katiba. Katiba zenyewe zinabadilishwa kirahisi kama kwenda kupiga copy za madesa!! Mahali pengine ni muhimu kutumia busara.
   
 13. m

  mutua12 Member

  #13
  Feb 17, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama hata fanya majukumu yake ipasavyo kwani kila wakati ataambatana na mzee ,labda sasa m7 ana second lady. Maana loo kazi ipo
   
 14. N

  NTIRU Member

  #14
  Feb 17, 2009
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafikiri si jambo zuri Rais kumteua mkewe kuwa Waziri ukitilia maanani kuwa tayari ana wadhifa mkubwa katika taifa, 1st-Lady. Okey, kwa vile labda Katiba inampa Rais uwezo wa kumchagua yeyote kuwa Waziri, hata akiwa mkewe, mwanae, kaka yake n.k. (Kumbuka F. Castro wa Cuba na mdogo wake) basi M7 anayo haki ya kumteua mkewe kuwa hata Makamu wa Rais. Hata hivyo, si jambo la busara. Enzi za usultani zilikwisha zamani. Ni vyema kuheshimu muda uliowekwa na katiba kwa Rais kuwa madarakani. Si jambo jema kwa M7 kujiongezea muda eti anaongoza vizuri. Huo ni uchu wa madaraka ambao matokeo yake ni kama yale ya Mugabe wa Zimbabwe aliyeirudisha nchi yake karne za nyuma katika ulimwengu huu wa sayansi na tekinolojia.
   
 15. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  si bora huyo kaweka wazi kuliko 'mr. Clean' aliyemfanya mke wake kuwa 'waziri kivuli wa biashara na uwekezaji'.Ebu tuangalie boliti kwenye macho yetu kwanza.
   
 16. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa wanaomuunga mkono Museveni, niwaulize, vipi JK akiamua kumpa mwanawe Ridhwani ubunge wa kuteuliwa na hatimaye Uwaziri say wa Fedha, tutasema katiba inamruhusu au tutakuwa wa kwanza kumshupalia???....Just thinking aloud.
   
 17. M

  Mwanazuoni Member

  #17
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete uko wapi wenzako wakifnya mambo? nawe Mpe mama salma wizara isiyokuwa na kazi maalum...nadhani wizara hizi zilikuwepo enzi za mwalimu.


  Africa tuna vituko vingi hasa kwenye siasa zetu ambazo si hasa. M7 kila siku anaunda wizara mpya kuridhisha watu wake. Nadhani ni kati ya serikali zenye mawaziri wengi zaidi africa kama sio duniani. Wananchi wa Uganda wanapata shida sana. hali ya maisha ni ngumu na mishahara ni midogo sana. nashangaa baadhi yetu twashabikia kumpa mke wizara bila kuangalia kuwa licha na kitu hicho kuleta maswali lakini ni gharama kubwa kwa wanchi. Labda walikua na bifu home au alipewa penzi la kutisha akaamua kuropoka kuunda wizara.


  hayeni
   
 18. Charles Mtekateka

  Charles Mtekateka Verified User

  #18
  Feb 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 310
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  kama katiba ipo silent let him use this lp hole, ila mimi maoni yangu ni kuwa je pakwep na kosa anaweza kumwadhibu na je hap kuna utawala bora mana lazma Confrict of Interest itawabana!!!!
   
 19. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama madai haya ni kweli, basi ni taahira,na tunapashwa kumuonea huruma kama mgonjwa wa akili!Na hata hivyo,hivi kilichotusibu wananchi mpaka tunafanyiwa mambo ya ajabu ya namna hii ni nini hasa, maana ujinga unaofanana na huu upo sehemu nyingi katika nchi zetu,hasa za Africa.Mmm,kazi.
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwaka 1962 rais Kennedy alimteua mdogo wake Robert Kennedy kuwa Attorney General.
  Wakati huo katiba ilikuwa kimya. Robert Kennedy alikuwa wakili mzuri tu na mpaka hivi leo sifa za utendaji kazi wake zinafahamika. Lakini Wamarekani kwa busara tu wakapitisha sheria kuwa rais wa Marekani asimchague ndugu yake kufanya kazi yeyote ile katika serikali yake.
   
Loading...