MUSA na NEEMA wako wapi?

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,067
709
Poleni najukumu wana jamii, kwa waliosoma shule za miaka ya nyuma kidogo kabla ya mkapa osis. Katika shule za msingi Tanzania kulikuwa na mtiririko wa story kuanzia darasa la tatu mpaka la saba. Katika vitabu vya kiiengereza wahusika walikuwa familia ya Mr$Mrs Daud huku watoto wao wakiwa Musa na Neema na mdogo wao Baraka.
Vitabu vile vilikuwa na mtiririko mzuri wa habari za kumvutia msomaji. Lkn watunzi wa sasa vitabu vyao ninakopy hadithi ambazo kila mmoja anazijua, hawana ubunifu. Mtunzi wa vitabu alikuwa nani?
 
Hivi vile vitabu havikuwa vinatolewa na Taasisi ya Kukuza Mitaala kweli. Ngoja watatusaidia wengine.

Vilikuwa vizuri ni mfano wa vile vya Oxford for Easy African Schools.
 
Ni vigumu sana kuamini wakiniambia walikufa. Kama akina Bulicheka wako mtaani haiwezekani hawa wakawa wamekufa.

Hivi nyumbani kwao akina Musa si palikuwa National Printpak Industry (KIUTA)?
 
Nafikiri kiuta walikuwa wachapaji tu lkn kuna vichwa vilikuwa vinafanya kazi. Tangu walipotoweka na elimu ilishuka km mshumaa unavyoungua.
 
Ni vigumu sana kuamini wakiniambia walikufa. Kama akina Bulicheka wako mtaani haiwezekani hawa wakawa wamekufa.

Hivi nyumbani kwao akina Musa si palikuwa National Printpak Industry (KIUTA)?

Nyumbani kwao ni moshi...according to story lakini sijui kams kuna uhalisia.

Pia kuna akina masanja na kwilasa...
 
Nafikiri kiuta walikuwa wachapaji tu lkn kuna vichwa vilikuwa vinafanya kazi. Tangu walipotoweka na elimu ilishuka km mshumaa unavyoungua.

Mimi nakikumbuka kichwa kimoja,S.M Tangaro,baada ya kustaafu serikalini kichwa hiki kilikuja kufundisha pale Geita High School miaka ya 90s,kilinifua Literature pale,sijui yupo wapi huyu mzee kwa sasa
 
Hadithi ya Fikiri na Sadiki ndio inayojidhihirisha kwa sasa.
 
Mi namkumbuka yule Matola ambaye alikuwa mchoyo kiasi kwamba hata wakati wa msosi alikuwa anajificha, kuna siku alikuwa anakula gizani kwa bahati mbaya akala na mdudu! nadhani kitabu hiki kitakuwa na cha darasa la 1 au 2, enzi hizo.
 
Last edited by a moderator:
"Musa is cleaning the blackboard"
"Neema is sweeping the floor"

I am Musa
I am a boy
I am ... years old

IT WAS GOOD!
 
kuna mkenya mmoja nasikia alipopewa wizara tu akaanza yake.
Na harufu ya ufyuz wake ndo mpka leo bado unaivuruga wizara na uelekeo haueleweki.
Wanahangaika na walipoangukia badala ya walipo jikwaa
 
Tusilaumu sana maana ukichunguza utagundua ni baadhi yetu tuliokwenda shule na kina Juma na Roza, ni sisi sisi tuliokuwa tukigombea mwanasesere na motokaa...wachache wetu kati ya wale tuliokuwa nao ndio waliofanya haya mpaka sasa tunashindwa kula nao kwani wana mikono michafu.

Ni sisi tulioipata elimu ile nzuri tulioiua elimu ile nzuri....ama kweli ni wapi tulioojikwaa??!
 
kuna mkenya mmoja nasikia alipopewa wizara tu akaanza yake.
Na harufu ya ufyuz wake ndo mpka leo bado unaivuruga wizara na uelekeo haueleweki.
Wanahangaika na walipoangukia badala ya walipo jikwaa

Huyu ndiye aliyeivuruga Familia ya Mr&Mrs Daud. mpaka sasa hatujui Musa na Neema wako wapi.
 
Back
Top Bottom