MUSA na NEEMA wako wapi?

Mr & Mrs Daud kwa sasa wote marehemu, bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe. Mr Daud alikuwa na rafiki yake kipenzi Mr Balali. Mr Balali alipo mpata first born wake akampa jina la Daud. Baadae Daud Balali akawa msomi mzuri sana mpaka akawa mfanyakazi bank ya dunia. Baadae Mkapa akamwingiza choo cha kike naye akiingia kichwa kichwa. Kwa sasa Daud Balali kafa Tanzania ila nchi nyingine yuu hai. Amekuwa kama Michal Jackson ila hali huku Tanzania Dada zake, Mdogo wake wa kiume wameuza viwanja, mashamba yake kama awana akili nzuri. Yale maroli aliye yaacha kwa kaburu jirani yake sijui yamepotelea wapi. Yule mzee msimamizi wa mali zake almanusra wamtoe roho, mzee kaumwa ehheee mpaka sasa ufahamu wa ubongo wake umekuwa upepo.

Mussa yupo uturuki sasa hivi na mke wake mzungu ili hali Neema alizalishwa ovyo ovyo hana mbele wala nyuma. Baraka yeye ni lecture Toronto University.
 
Tehtehtehhh.... nimecheka hadi nimepaliwa lol!
Musa na Neema walikuwa vichwa wale, nadhani walivyoona miyeyusho hapa bongo wakaenda zao nje ya nje, nadhani wako botswana wanapiga mzigo wa udaktari huko

wamekua wwakubwa wamebadili majina wanajiita diamond na wema.
 
Woooh, you made my day... thanks very much Balantanda

Hawa hapa....

395011_344736028877114_1023084701_n.jpg
 
Last edited by a moderator:
Yule mama alikuwa anauza vyungu halafu kavaa hereni kubwa mbuzi akaja kudumbukiza mguu kwenye hereni yake anaitwa nani yule mama jamani, manake alilia balaa

Ila ile story ya Manenge ilikuwa bomba sana " Tumbo niache nimwachie Manenge Uji" Hawa vijuza nadhani walishakufa kwenye ile hadithi
 
Tena hawa enzi hizo walikuwa darasa la pili
Aise vile vitabu havitakaa vitokee tena, hata ukiangalia vitabu vya kiswahili na jiografia navyo vilikuwa na mtiririko mzuri kuanzia darasa la tatu hadi la saba
Miaka hii sasa kila shule na vitabu vyake lol!

yaani ilikuwa ni balaaa aiseee!! Ile hadithi ya Babu aliyekuwa mjanja(sikumbuki ni darasa la ngapi) anamuongelesha mjukuu wake ili chai ipoe........ Mara utasikia Siafuuuuuuuu!!!! Kumbe ndio anapuliza chai hivyo........
 
  • Thanks
Reactions: ram
Nilisoma Iwanga na Manow kulikuwa na maktaba za shule. full madawati.kaka yetu ujaye turudishie mama yetu Tabitha Siwale
 
Ulieleta hii mada Barikiwa sana,,,!! Umenikumbusha KAMBI ya KABOYA dah,,,! Nway kipindi kile shule zilikuwa tam sana! Ukifika shule unapiga mchakamchaka wa Nguvu Damu inachemka ukiingia CLASS mwili uko vzr Kiukweli zilikuwa ni cku zakupendeza sana! natamani wanangu nao wangepitia mambo km yale lkn waapii,,!! Kipindi hicho madogo 2likuwa wakakamavu ckdg Sio cku hz watoto hata kupanda school BUS hadi kashikwe mkono kamelegeaaa khaaa,,,,!!!
 
yaani ilikuwa ni balaaa aiseee!! Ile hadithi ya Babu aliyekuwa mjanja(sikumbuki ni darasa la ngapi) anamuongelesha mjukuu wake ili chai ipoe........ Mara utasikia Siafuuuuuuuu!!!! Kumbe ndio anapuliza chai hivyo........

Ha ha haaaa! ndgu acha kabisa Enzi hizo,,!
 
Rafiki ni bora kuliko mwanasesere
Enzi za Juma na Roza Hizo!!!!
 
Ulieleta hii mada Barikiwa sana,,,!! Umenikumbusha KAMBI ya KABOYA dah,,,! Nway kipindi kile shule zilikuwa tam sana! Ukifika shule unapiga mchakamchaka wa Nguvu Damu inachemka ukiingia CLASS mwili uko vzr Kiukweli zilikuwa ni cku zakupendeza sana! natamani wanangu nao wangepitia mambo km yale lkn waapii,,!! Kipindi hicho madogo 2likuwa wakakamavu ckdg Sio cku hz watoto hata kupanda school BUS hadi kashikwe mkono kamelegeaaa khaaa,,,,!!!

gwaride la ukaguzi wa usafi, kila juma tatu na juma tano, ole wako usiwe umekata kucha au kunyoosha uniform, unakumbana na fimbo za kutosha, kuingia madarasani kwa ngoma na filimbi, kuimba nyimbo za kuwalaani makabaila na mapebari..shule zilikua nzuri sana
 
Aksante kwa taarifa japo sikujua km kweli Familia hii iliokuwa ya kufikilika ili kuleta mtiririko mzuri wa mafunzo. kwaani mpaka sasa vitabu vile vimenasa vichwani siwezi kusahau. Nimesoma sekondari mpaka chuo lkn nimeshasahau cha kushangaza nakumbuka yale ya primary. Kuna kitabu cha darasa la kwanza na la pili wapo akina Juma na Rosa, Damas na wengine. Kuna shairi darasa la tatu la sungura akitaka kula ndizi aliruka lakini hakufanikiwa kuzifikia mwisho akasema hazitaki mbichi hizi. siku moja nilishika kitabu cha mtoto wangu wa darasa la 3, nilishangaa maswali wanayoulizwa wakati hata hichio kiingereza chenyewe bado, swali what is constitution? what is democracy? what is reproduction system?

Mr & Mrs Daud kwa sasa wote marehemu, bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe. Mr Daud alikuwa na rafiki yake kipenzi Mr Balali. Mr Balali alipo mpata first born wake akampa jina la Daud. Baadae Daud Balali akawa msomi mzuri sana mpaka akawa mfanyakazi bank ya dunia. Baadae Mkapa akamwingiza choo cha kike naye akiingia kichwa kichwa. Kwa sasa Daud Balali kafa Tanzania ila nchi nyingine yuu hai. Amekuwa kama Michal Jackson ila hali huku Tanzania Dada zake, Mdogo wake wa kiume wameuza viwanja, mashamba yake kama awana akili nzuri. Yale maroli aliye yaacha kwa kaburu jirani yake sijui yamepotelea wapi. Yule mzee msimamizi wa mali zake almanusra wamtoe roho, mzee kaumwa ehheee mpaka sasa ufahamu wa ubongo wake umekuwa upepo.

Mussa yupo uturuki sasa hivi na mke wake mzungu ili hali Neema alizalishwa ovyo ovyo hana mbele wala nyuma. Baraka yeye ni lecture TorontoUniversity.
 
Watoto wageuka mawe...
Awafu mwenye nguvu..
Mkwawa shujaaa
Mchoyo hana rafiki..
Andunje na wadudu..
Safari yenye mkosi....
Jogoo aliyesema....
Heri mimi sikusema...
 
kibanga ampiga mkoloni..... kweli maisha yanabadilika
Watoto wageuka mawe... Awafu mwenye nguvu.. Mkwawa shujaaa Mchoyo hana rafiki.. Andunje na wadudu.. Safari yenye mkosi.... Jogoo aliyesema.... Heri mimi sikusema...
 
Ulieleta hii mada Barikiwa sana,,,!! Umenikumbusha KAMBI ya KABOYA dah,,,! Nway kipindi kile shule zilikuwa tam sana! Ukifika shule unapiga mchakamchaka wa Nguvu Damu inachemka ukiingia CLASS mwili uko vzr Kiukweli zilikuwa ni cku zakupendeza sana! natamani wanangu nao wangepitia mambo km yale lkn waapii,,!! Kipindi hicho madogo 2likuwa wakakamavu ckdg Sio cku hz watoto hata kupanda school BUS hadi kashikwe mkono kamelegeaaa khaaa,,,,!!!

Aaaah! Hii sasa mkuu tunazungumzia miaka gani vile? Kuishia 80's?

Kwa kweli enzi hizo shule ilikuwa burudani pamoja na kwamba mijamaa ilikuwa inatembeza viboko siyo kawaida lakini mtu ulikuwa na hamu tu ya kwenda shule. Maana shule zenyewe kwanza zilikuwa na vitabu vya kutosha kwenye maktaba ya shule ile saa 4 wakati wa mapumziko madogo mmebanana maktaba kuazima vitabu [KKKT - Asha apotea sokoni, Alfu lela ulela, zamani mpaka siku hizi, someni kwa furaha (kile cha mpiga filimbi wa Hamelin), Mwanamalundi mtu maarufu katika historia ya Usukumani, Adili na nduguze,n.k]

Tuwape pole tu watoto wetu wamekosa uhondo!!
 
siku hizi mda wa kusoma hadithi haupo,katoto kadogo la kwanza kanasoma masomo 12 hapo hakajabeba kuni,jembe,maji na mfagio mwishoe vitoto vinapinda migogo.
 
yaani ilikuwa ni balaaa aiseee!! Ile hadithi ya Babu aliyekuwa mjanja(sikumbuki ni darasa la ngapi) anamuongelesha mjukuu wake ili chai ipoe........ Mara utasikia Siafuuuuuuuu!!!! Kumbe ndio anapuliza chai hivyo........
Eti babu anaweza kunywa chai ya moto. Akaanza mbwembwe mara ohhhh!

Wazazi wako wanakusifuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!

Mlima kilimanjaro ni mlima mrefuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!

Angalia hao siafuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!

Kijana ndo akastuka, babu siafu wako wapi? Kunywa basi hiyo chai mwishowe itapoa!! Babu akapiga chai yake.
 
Kuna na ile hadithi ya Sungura Mjanja;

Aliyemfunga Simba kwenye mti ili akachote maji. eti anamsuka nywele kumbe anamfunga kwa nywele zake kwenye tawi la mti.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom