Bifu maarufu la Shah Rukh Khan na Sunny Deol lililodumu kwa miaka zaidi ya 20 mpaka kuisha kwake mwaka huu, tuna la kujifunza hapa

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,434
21,121
Miongoni mwa mabifu yaliyowahi kutikisa nchini India basi bila shaka utazungumzia bifu lililokuwepo baina ya Shah Rukh Khan ukipenda muite King Khan au SRK na mbabe Sunny Deol.

Hili bifu lilianzia kwenye Ile filamu ya Darr iliyotoka mwaka 1993 iliyowakutanisha Sunny Deol aliyecheza kama Starring akitumia jina la Sunil Malhotra ,Shah Rukh Khan aliyecheza kama adui/mhalifu aliyekuwa akimtongoza mke wa Sunny Deol akitumia jina la Rahul Mehra,na mwanadada Juhi Chawla aliyecheza kama Kiran Awasti (Mke wa Sunny Deol).

Kipindi hii filamu inatengenezwa Sunny Deol tayari alishakuwa super star maana alianza kuigiza tangu mwaka 1983 hivyo alikuwa na jina kubwa sana ila kwa upande wa King Khana yeye bado alikuwa underground maana yeye ameanza kuigiza mwaka 1992 hivyo mpaka anakuja kucheza filamu ya Darr hakuwa akifahamika kiviile.

Ugomvi ulitokana na wivu kutoka kwa Sunny Deol akimuonea wivu Shah Rukh Khan (SRK) ,SRK licha ya kucheza adui na bado ni underground lakini alitokea kuwa kipenzi cha watu sana na alimfunika vibaya mno Sunny Deol kwenye hiyo filamu jambo ambalo lilimuuma Sunny Deol.

Sunny Deol alikuwa na hasira kwa sababu alihisi kuwa jukumu la SRK katika filamu lilikuwa likisifika sana na kuonyeshwa kwa njia nzuri zaidi kuliko yake. Kipande maarufu cha filamu hicho kilikuwa kinahusisha SRK kutamka "I Love You K-k-k-Kiran" wakati wa kumtongoza mke wa Sunny Deol.

Sunny Deol alikasirika maana aliona SRK analivua jukumu lake hivyo kumfanya yeye asionekane muhimu hivyo akaapa hatokaa afanye naye kazi tena .

Wawili hawa tofauti zao wamezizika rasmi mwaka huu baada ya Sunny Deol kutoa filamu mpya ya Gadar 2 ambayo ni muendelezo wa Gadar 1 iliyotoka mwaka 2001 na kuonekana kupendwa zaidi na mashabiki hivyo kuililia muda mrefu muendelezo wake.

SRK alimpigia simu kumpongeza Sunny Deol na hatimaye wawili hawa wakipata kualikana sehemu mbalimbali na kuonekana kwenye hafla mbalimbali hivyo bifu kulizika rasmi na huenda wakafanya pamoja filamu nyingine.

Ikumbukwe SRK naye ametoa filamu yake mpya mwaka huu inaitwa Pathaan akishirikiana na John Abraham, ni filamu mzuri sana na imepokelewa vizuri mno sawa na Gadar 2 nayo imepokelewa vizuri mno sokoni.

Kila la heri kwao.


649037960.jpg
-1173303818.jpg
images (4).jpeg
images (6).jpeg
images (5).jpeg
 
Ikumbukwe SRK hakuwa chaguo la kwanza kucheza hiyo filamu ya Darr.

Walichaguliwa mastaa kadhaa akiwemo Ajay Devgan, Amir Khan, Akshay Kumar lakini wote walikataa kuigiza maadui ni sawa walivyokataa kwenye filamu ya Baazigar ambayo iliwataka wacheze maadui ila wakagoma na zote akacheza SRK.
 
Sunny Deol ni mshamba sana, Sana unamchukiaje mtu aliiyekufunika kwenye kazi? Jamaa majivuno mengi ndio yaliyokua yanamsumbua. Alishindwa kukubali kijani mdogo from no were alimfunika na the rest ikawa ni history.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom