Muongo Vs. Mengi. Kimenuka !

Muongo Vs. Mengi. Kimenuka !

Mkuu usipende kuamini ngonjera za kina Mengi!
Niambie ni mtanzania au kampuni ya kitanzania gani aliyewekeza katika tafiti za rasilimali zetu hasa hayo mafuta na gesi?
Kina mengi wabakie kuuza soda na juisi tu,wasijidai na kujikweza kwa vitu wasivyoviweza.
Watanzania hatujawekeza katika utaalamu vya kutosha!tunatakiwa kufanya hivyo sasa...

Basi isichimbwe hiyo gesi..Kwani hao wazungu walipata investors kutoka mbinguni walipoanza chimba gas..mana unaonakama kitu impossible kwetu kiinvest
 
Basi isichimbwe hiyo gesi..Kwani hao wazungu walipata investors kutoka mbinguni walipoanza chimba gas..mana unaonakama kitu impossible kwetu kiinvest

Tatizo watanzania tunaona mambo ni rahisi kama tunavyoona kwenye movies!hatujishughulishi kiakili kujua ni kwa vipi wenzetu walifika hapo tunapotaka kuigiliza!
Tunadhani tukijenga uwanja mkubwa na kuvalisha suti wachezaji wetu basi watashinda kama Brasil,Tunadhani kujenga vyuo vikubwa kama UDOM tutakuwa na wasomi walioshiba!Tunadhani kusema sasa ni wakati wa Big results now basi mambo yatabadilika ghafla...yaani tunadhani vitu vinatokea tu bila kuandaliwa!hizi ndio mbwembwe za kina mengi na wazee wa NICOL!!
 
Mengi hana hela ya kuwekeza zaidi ya udalali alete wazungu na yeye apate cha juu....watz hawana uzoefu, ujuzi wala rasilimali za kuwekeza kwenye natural gas sasa mlitaka Muhongo aseme uongo mfurahi au?...hatutaki jwatu wachache kama hawa akina Mengi waje wanufaike na rasilimali za taifa zima kwa kupewa vitalu halafu wenyewe waviuze kwa wawekezaji waweke pesa mfukoni...
 
Tatizo la watanzania tunapenda sana kupakwa mafuta ili hali kweli hatuwezi.Kila sehemu tunapenda usanii.Prof aliona billioner wa bongo amewekeza sana kwenye viwanda vya vyakula ndio maana akasema ukweli gasi hatuwezi.uwekezaji katika Gas si mchezo.hata maofisini mbogo akikosea anataka aambiwe kwa kubembelezwa,ndio maana hatufiki.

wewe pengine ni vyema upuuzwe? amejuaje hawawezi kuwekeza kwenye gas kama hata nafasi hataki kuwapa?
MUONGO ANA MATATIZO MAKUBWA NA NI HATARI KWA TAIFA
ULIDIRIKI KUSEMA HANA MUDA WA KUONGEA NAO.
HIVI KWELI NI KAULI YA WAZIRI ALIYE TIMAMU?
 
Mengi hana hela ya kuwekeza zaidi ya udalali alete wazungu na yeye apate cha juu....watz hawana uzoefu, ujuzi wala rasilimali za kuwekeza kwenye natural gas sasa mlitaka Muhongo aseme uongo mfurahi au?...hatutaki jwatu wachache kama hawa akina Mengi waje wanufaike na rasilimali za taifa zima kwa kupewa vitalu halafu wenyewe waviuze kwa wawekezaji waweke pesa mfukoni...

comments za watoto hizi.
 
Hapo Prof. asaidiwe maana kapotoka kidogo.
Wasomi wengi hasa maprofesor wanastaha sana na wanakubali/wanakiri makosa bila kupoteza mda.
Namwomba Mh.Prof.Muhongo aridhie kuwapatia Wazawa vitalu ikibidi na mitaji maana ndio Mwl. Nyerere alipigania hili kiasi cha kuacha kuchimba kwaajili ya kuwapa wazawa mda wakujipanga na kuweza "utilize resouces" tulizonazo.
Itakuwa ni fedheha sana tupigane vikumbo na wageni kwa hili.
Nyerere alipigania uhuru wa nchi hii na kuwafukuza wakoloni ili mwananchi wa kawaida aweze kujikomboa na kuwasaidia wananchi wengine wasio na uwezo lakini inaelekea kuwa kinyume!
Viongozi wengi wamebadilika na kujisahau kwa kuwakumbatia wawekezaji wa kigeni na kuwatosa wazawa.Hakika dhambi hii ni ufisadi ambao hauvumiliki na hautusaidii kabisa watanzania.
Tutalaumiwa hadi vizazi vyetu hadi vya tatu na vya nne.Tubadilike Viongozi kabla mambo hayaja haribika.
 
Tatizo bw. Mengi hukimbilia media na wananchi anaposhindwa kushawishi juu ya mambo yake ya kibiashara.

I support Muhongo kwamba watanzania hatuna uwezo.....suluhisho sio kuwapa wageni bali ni kama alivyotuasa baba wa Taifa!
Mengi na kundi lake waache ulaghai.

wewe utakuwa na matatizo ya akili. Kwa nini watanzania ambao ni wenye nchi wasihamasishwe na kupewa vipaumbele kuwekeza kwenye gas kama mtu mmoja mmoja kama Mengi na wale wenye kidogo wakanunua hisa kwenye makampuni ya uchimbaji na usambazaji wa gas? Tatizo lenu baadhi ya viumbe mmejaa ushabiki usiokuwa na maana. Hivi unaelewa kwamba kama watanzia watawakeza kwenye maliasili watatumia faida watakazopata kwa kiwango kikubwa kuendelea kuwekeza hapa nchini kuliko hao wageni mnaowaabudu?
huyo prof. mnayefanana mitazamo akubali amekosea na awatake radhi watanzania na aangalie namna ambavyo uvunaji wa gas unaweza kuwashirikisha watanzania wenye uwezo.Unastahili viboko kwa upofu wako wa akili.
 
Uwe unasoma nilichoandika kabla ya kukurupuka na majibu yako ya kishabiki.
Nimesema suluhisho 'ni kama alivyotuasa hayati baba wa taifa'
sasa kama hujui baba wa taifa alishauri nini kuhusu rasilimali zetu nakupa pole.
unashangaza hata hujui ulichoandika kabla,
 
comments za watoto hizi.

na wewe ni dalali wa kimataifa kama mkuu wako Mengi na wenzake wanaojiita wazawa wenye parochial interests walizozivalisha magwanda ya economic indigenization...nway kila mtu na tumbo lake nenda kapiganie vitalu October siyo mbali, sisi wengine bado watoto kama unavyopenda kufikiri.
 
Uprofesa wa jamaa unanitia shaka sana....au ni profesa mjinga....le profesol....maneno yake hayaonekani km yanatoka kwa profesa....


Mkuu Dr.Mo

Nimekuwa nikimfuatilia Profesa Muhongo tangu wakati ule wa mgogoro wa gas Mtwara hadi sasa hii issue yake wawekezaji wazawa, huyu jamaa ametawaliwa sana na intellectual arrogance.

Hii ni kasumba inayowatawala wasomi wengi wa kariba yake, ndiyo maana wengi hufeli vibaya katika masuala ya uongozi. Uongozi ni busara, uongozi ni kushauriana na kusikiliza, na uongozi ni kujishusha ili kutengeneza daraja na watu. Hili kwa hawa ndugu zetu wasomi wa taaluma halipo maana wao hudhani kila kitu wanakijua.
 
Wakati wamakonde wanapinga ujenzi wa bomba la gas kuelekea huko munakoita Tanganyika, kabla ya sera ya gas,yeye Mengi na vyombo vyake walituhadaa wanakusini eti ni wahaini na wabinafsi wa gas akidhani yeye na wadanganyika watafaidika. Mfn vipima baridi vyake dhahiri vilionesha kutukandamiza wanakusini juu ya madai yetu halali....HAYA SASA MUTAJIONEA WENYEWE SS MANTIKI YA WAMAKONDE IKO WAPI!!
 
Meningitis is defined as an inflammation of the meninges (protective membrane covering the brain and the spinal cord).
The most common symptoms of meningitis are headache and neck stiffness associated with fever, confusion or altered consciousness, vomiting, and an inability to tolerate light or loud noises.
Basing on your ID name, you're pretty right with your comment!!!
 
Meningitis is defined as an inflammation of the meninges (protective membrane covering the brain and the spinal cord).
The most common symptoms of meningitis are headache and neck stiffness associated with fever, confusion or altered consciousness, vomiting, and an inability to tolerate light or loud noises.
Basing on your ID name, you're pretty right with your comment!!!
Aisee nimekupa like ya ukweli..,yaani huyu jamaa labda ajipofue macho na fikra ili asiione wala kuielewa hii comment.
 
UBINAFSI NA UFISADI WA MENGI NA CHUKINA FITINA KATIKA MAENDELEO.


[FONT=Times New Roman, serif]Hivikaribuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watanzaniadhidi ya Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Prof SospeterMuhongo yakiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta BinafsiTanzania (TPSF) ambae pia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, BwanaReginald Mengi. Malalamiko hayo ambayo yameendelea kunukuliwa nabaadhi ya vyombo vya habari na kupelekea hata baadhi ya wahusikakutoka wizarani, Idara na Mashirika yake kulazimika kujibu na kutoleaufafanuzi malalamiko na tuhuma hizo nzito dhidi yao. Moja ya vyombohivyo ni gazeti la NIPASHE linalomilikiwa na IPP media la tarehe6septemba, 2013 katika ukurasa wake wa tatu kuna habari inasema"SERIKALI YAZIDI KUPUUZA USHAURI WA TPSF" Inaeleza habari hiyokuwa " ..Wakatitaasisi ya sekta binafsi (TPSF) ikiishaurikuharakisha sera ya gesibadala ya ugawaji vitalu, serikaliimeendelea kupuuza ushauri huo nasasa kupitia Shirika la maendeleoya petroli Tanzania (TPDC)imetangaza rasmi kuharakisha suala hilokwa madai ya kuwahi ushindaniwa masoko ulimwenguni.."


LakiniTPDF nao katika gazeti la UHURU la jana Ijumaa katika ukurasa wakewatatu imeandikwa habari yenye anuani "MWENYEKITI TPDC: UBINAFSIUNAWAPONZA WATANZANIA. ->wengi wanalalamika uwezohawana,
->Zabuniza vitalu mwezi ujao." katika habari hiyo Mwandishi ameandikakuwa "Mwenyekitiwa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) , Michael Mwanda, amesema ubinafsi miongoni mwa watanzaniandio unaowafanya washindwe kunufaika na fursa za kiuchumi zilizoponchini, zikiwemo mafuta na gesi. Mwanda alisema hayo jana jijini Dares salaam, alipokuwa akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habarijuu ya malalamiko ya baadhi ya watanzania kuwa hawapewi nafasikushiriki katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta nagesi."


Malumbanohayo kupitia vyombo vya habari baina ya pande mbili yaani Mengi naIPPyake na Muhongo na Mashirika yake ambayo yamedumu kwa muda, sasayanachukua sura mpya baada ya kuwepo kwa taarifa za chini chini kuwaMwenyekiti huyo wa TPSF na IPP ameandaa mpango wa kuwatumia vijanawaChama Cha Siasa cha Upinzani (CHADEMA) kufanya kongamano lenyemaudhui "rasilimali za nchi na manufaa kwa wazalendo" ambapokongamano hilo limepangwa kupewa airtime katika kituo maarufu chatelevision hapa nchini cha ITV ambacho kinamilikiwa na IPP medialakini pia posho, chakula na incentives mbalimbali zimepangwakutolewa katika Kongamano hilo.


Kamailivyo katika mkakati huo, lengo lililopo nyuma ya pazia la kongamanohilo ni kutaka kuionyesha jamii kuwa Waziri na Wizara kwa ujumlahaijali maslahi ya wazawa na kwamba viongozi wakuu wa Wizara husikahawana Utaifa wala Uzalendo (kwa maana ya upendo kwa Taifa) hivyowanataka kuzitumia nafasi zao ndani ya wizara katika kujitajirishabinafsi na kufanya upendeleo kwa wawekezaji wageni ambao hawanamanufaa ya moja kwa moja katika maendeleo ya wananchi.


Madhumuniya andiko langu hili na kuvuta utafakari makini na wa wengi katikasuala hili ambalo kama hatua muhimu na za haraka hazitachukuliwakatika kulikabili linaweza kuleta tafsiri hasi kwa jamii na hivyokuwagawa na kuwavuruga watanzania na hasa kuwafanya wapoteze imani namatumaini yao kwa Serikali, Waziri, Wizara, Idara na Mashirikayaliyopewa dhamana ya usimamizi wa rasilimali za nchi hii.


Naombaikumbukwe kuwa si mara ya kwanza kwa seke seke la aina hii kuzuka amakuzushwa chini ya uratibu na usimamizi wa Mzee Mengi. Na mara zoteamekuwa akitumia nguvu ya ushawishi wa vyombo vya habarianavyovimiliki katika kutafuta kuungwa mkono na hata kuonyesha ubayawa wabaya wake. Ubaya, malumbano na mizengwe mingi ambayo huzalishwana kusimamiwa na Mzee Mengi asili yake ni Ubinafsi na kuguswa kwamaslahi ya kiuchumi aliyonayo katika Sekta mbalimbali hapanchini.


Hivikaribuni kulizuka sekeseke mfano wa hili la sasa ambalo lilihusuVING'AMUZI na kabla ya hapo TBC, UBINAFSISHAJI WA KILIMANJAROHOTEL,SUALA LA YUSUPH MANJI, SHEIKH AL BASALEHE na katika migogoroyote hiyo Mzee Mengi amekuwa akitumia vyombo vya habari katikakuwakandamiza, kuwazushia, kuwatuhumu na hata kuwadhalilishawapinzani wake. Nitaomba wanajamvi wakumbuke kuwa Mwaka 2008kulipokuwepo mgogoro baina ya Mzee Mengi na Al Basalehe, Katikamgogoro huo Mzee mengi alimrubuni Ustadhi Mmoja wa madrasa (jinalinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) na kuwatumia wanafunzi wamadrasa hiyo kutunga nyimbo za kaswida za kumdhalilisha SheikhAlBasalahe na kisha nyimbo hiyo kupewa airtime katika kituo cha ITV,na kwa mfano kama huo akaitumia ITV kuwataja washindani wake kiuchumikuwa ni MAFISADI PAPA.
Sinakumbukumbu kuwa alitumia vigezo gani kuwataja wapinzani wake haokibiashara kama mafisadi papa, ila kumbukumbu yangu inaniambiaaliwataja hadharani na kupelekea baadhi kumpeleka mahakamani nakumfungilia kesi ambazo hata hivyo hazikupata airtime za kutoshakwenye vyombo vya habari na hata mwisho wake haukuwa umefahamika kwawengi.


Tukirudikatika hoja yetu ya vitalu vya gesi ambavyo Mwenyekiti huyo wa IPPnaTPSF amekuwa akividai kwa hamu kubwa na kuwatuhumu Viongozi waWizara, Wakuu wa Idara na Mashirika yanayohusu Rasilimali gesi namafuta kuwa hawana hata chembe ya Uzalendo na wabinafsi, na hofunitaeleweka vibaya kwa baadhi ya watu nikisema kuwa kauli hii hainauhalisia na si ya kweli, na kwamba inalenga kuchochea hisia za chukina imetolewa kwa misingi ya Chuki, it's simply a hate speech thathate are produced.


Kwamujibu wa TPDC, kuchimba kisima kimoja kwa ajili ya kutafuta gesi namafuta katika nchi kavu ni dola za Marekani milioni 40 (Tshs.Bilioni64) na kwa kina kirefu cha bahari ni dola 120 (Tshs Bilioni190) na pia ili kupata mafuta au gesi baada ya kupata uhakika,mwekezaji anapaswa kuchimba visima vinne hadi vitano, hivyo inahitajimwekezaji kuwa na mtaji usiopungua dola za kimarekani milioni 600 ~800 kiasi ambacho watanzania wengi hawana (MENGI akiwemo) na kwaKauli ya Mwanda, Mwenyekiti wa TPDC alisema kuwa Watanzania iliwaweze kunufaika na rasilimali hiyo, hawana budi kuungana na wabiawenye uwezo wa kimtaji na teknolojia (Suala ambalo Mengianalipinga)


Tatizola kimsingi hapa ni Ubinafsi wa baadhi ya watu ambao wanatakaupendeleo kwa maslahi binafsi ya kibiashara kwa nembo ya uzalendo nauzawa. Kumekuwepo na rekodi zenye kusikitisha ambazo zinaonyeshatatizo la msingi linalowakabili hawa tycoon wetu katika mikopowaliyochukua katika mabenki makubwa mbalimbali hapa nchini na hatanje ambapo bado hawajarejesha mikopo hiyo na hivyo kutokopesheka tenakwa miradi mikubwa kama hii ya vitalu vya gesi lakini pia zipo rekodinyingine zinazoonyesha wametumia mikopo kwa shughuli ambazohawakuombea mikopo hiyo ikiwemo mikopo kutoka benki ya kilimo(Takwimuzipo)


Kamahayo ya mikopo hayatoshi, tayari Kampuni za Mzee Mengi zinashikiliavitalu takribani 59 vya madini vyenye Ukubwa wa mita za mraba3,752.37 (sq km) na baadhi ya vitalu hivyo alivyovishikiliaameshindwa kuviendeleza na matokeo yake Serikali inakosa mapatokutokana na kutoendelezwa kwa vitalu hivyo lakini pia watanzaniawanakosa ajira na manufaa mengine, najiuliza kama hii ndio tafsiri yaUZAWA ambayo Mzee Mengi anaizungumza ama ni AINA nyingine ya UFISADIambayo watanzania walio wengi bado hawajaung'amua kwa kuwa vyombo vyahabari haviandiki wala kusema kuhusu habari hizi. Katika attachmentni orodha ya vitalu mbalimbali vya madini vinavyomilikiwa na Kampuniza Mzee Mengi hapa nchini.


Tunawezakutofautiana katika mengine lakini katika yale yanayohusumustakabaliwa nchi naomba watanzania tuungane na tuseme hapana.Matumizi ya Vyama vya Siasa, wanasiasa na hata pressure group katikakutetea maslahi ya baadhi ya tycoon wa hapa nchini na hata nje nikatika makosa makubwa ambayo yanaweza kutuletea madhara makubwa sanahasa kutokana na rasilimali zilizopo hivi sasa hapa nchini ambazozinatolewa macho na mamilionea wakubwa wa ndani na nje na hata nchitajiri duniani.

Nitoeombi kwa Vijana hawa wa Chadema wanaoandaa Kongamano hilo, watambuenafasi yao kama vijana na Safari waliyonayo ya kuijenga kesho yao nakusahau posho hizo za siku moja na vyakula. Ni wakati wa kusimamiahaki na kuitetea kweli, hata ikiwa kweli hiyo inakinzana na maslahibinafsi. Si wakati wa kutanguliza maslahi ya tumbo, ama maslahi yachama bali ni wakati wa kutanguliza UTAIFA na UPENDO wa kweli kwanchi yetu.

MunguIbariki TANZANIA. [/FONT]
 
Tatizo bw. Mengi hukimbilia media na wananchi anaposhindwa kushawishi juu ya mambo yake ya kibiashara.

I support Muhongo kwamba watanzania hatuna uwezo.....suluhisho sio kuwapa wageni bali ni kama alivyotuasa baba wa Taifa!
Mengi na kundi lake waache ulaghai.

unasikitisha sana kama unafikiria kwa kiwango hiki... kwa iyo kama huna capacity dawa ni kugawa tu kwa wageni??? kama huo ndio uwezo wako wa kufikiria basi kumbe hata uhuru kina nyerere wasingeudai maana hatukua na capacity yoyote ya kujiendesha!!! njia za kushirikisha watnzania ni kama ifuatavyo wala huitaji uwezo
1. joint venture - kampuni zite za nje ziwe na at least 30percent TZ kampuni ktk umiliki
2. kutumia kampuni za uwekezaji za kitanzania kama NICOL
3. uchimbaji tu ndio uwe foreign issue kama logisitics, distribution, marketing etc vifanywe na kampuni za TZ
4. kuhamasisha wawekezaji wa TZ kuungana na kupewa priority ktk kila fursa ambayo haiitaji utaalamu wa nje
5. minimum number ya workers amabo ni local

kwa iyo fursa ni nyingi ila si izi za kijinga zinazohubiriwa na clouds fm za kuuza madafu, kuuza juisi, kupika mama ntilie... tumefanywa tuamini kua sekta rasmi zote ni za wazungu tu na sie sekta zetu ni izi za kimachinga tu!!!
 
Hili ni Tatizo la Rais kuteua mtu ambae sidhani kama alikuwa anaifahamu vizuri background yake hapa inawezekana alishauri tu na mtu wake wa karibu ili kumpa ulaji jamaa yake Muhongo madhara yake ndio haya na hapa ndio tunapomtofautisha Kikwete na Baba wa Taifa kwani Baba wa Taifa alikuwa anawafahamu vizuri watu wake wote wa chini na hii ilimsaidia sana kutochagua vilaza kama hawa akina Muhongo.
 
Wakati wamakonde wanapinga ujenzi wa bomba la gas kuelekea huko munakoita Tanganyika, kabla ya sera ya gas,yeye Mengi na vyombo vyake walituhadaa wanakusini eti ni wahaini na wabinafsi wa gas akidhani yeye na wadanganyika watafaidika. Mfn vipima baridi vyake dhahiri vilionesha kutukandamiza wanakusini juu ya madai yetu halali....HAYA SASA MUTAJIONEA WENYEWE SS MANTIKI YA WAMAKONDE IKO WAPI!!

Hili ndilo jambo tunalosahau kwa urahisi!
Chukua LIKE MKUU!
 
Back
Top Bottom