Jakubumba
JF-Expert Member
- Mar 5, 2011
- 1,624
- 501
So sad!
Ndugu, huyo muhongo alikuwa ni mtumishi (mtafiti) wa wizara hiyo, alikuwa mkweli saaana na alikuwa anakipindi TBC radio. Ngeleja alikuwa hampendi mno kwani alikuwa anaweka kila kitu bayana kuhusu madini nchi nzima yaani alikuwa hafichi kitu. Hicho anacho kikataa leo, yeye alikuwa anakishauri jinsi ya kukitelekeza. Kwa masikio yangu mimi nilikuwa namsikia akizungumza haya. Muhongo alivutia watu wengi sana kwa jinsi alivyokuwa anazungu na kuishauri serikali. Ngeleja alikuwa hampendi kwa kuwa bwana Muhongo alikuwa anayaweka mambo yote bayana hivyo kuhatarisha ulaji. Muhongo alikuwa anagawa namba zake za simu redioni kwa yeyote aliyetaka kujua kuhusu masuhala ya madini amuulize. Ngeleja na Muhongo walikuwa mahasimu wakubwa. Ngeleja akamhandalia zengwe, kabla mambo ayajajipa mara gafla kibao kikageuka, Rais akamteuwa Muhongo kushika nafasi ya Ngeleja.
Watu sasa tukajua mpinga ufisadi kaingia kazini, sasa mambo yataenda saaafi kwa umakini, kumbe wapiiii... Yeye ndio nyangumi kabisaaa... kelele za mwanzoni ilikuwa msukumo wa njaa na utapia mlo tu. LEO anajipinga mwenyewe alivyowai kuvipendekeza kutoka kinywani mwake akiwa redioni.
Waliokuwa wakivisikiliza vipindi vyake TBC radio enzi zile watakubaliana na mimi. NASEMA HIVI, NI KWELI CCM NI CHAMA CHA KISHIRIKINA, HATA KAMA UKIWA MSAFI VIPI, UKIINGIA TU HALMASHAURI KUU/ KAMATI KUU, UNAKUWA FISADI LA KUTUPA. Jamaa ndio hivyo tena nae leo hii sio mwenzetu.