Mungu wangu! Siamini kama ile ni kondoa

Mungu wangu! Siamini kama ile ni kondoa

Hiyo ndiyo faida ya Miaka 50 ya Uhuru ngoja wakazi wa Kondoa wafaidi matunda ya Uhuru. Kisha napenda kujua jimbo hilo safari hii linaongozwa na Mbunge wa Chama gani?. Kama bado ni wa CCM no comment hiyo ni halali yao.
Juma Nkamia
 
Watu wa kondoa hawajui chama kingine zaidi ya CUF au CCM.Mimi nimesoma shule ya Miningani kama unaenda kondoa girls, darasani tulikua wakristu wawili tu.Shule nzima ilikuwa na wakristu wasiozidi 20.
pia kondoa ina wakristo kadiri ya madhehebu ya katoliki na hivi karbun kondoa imekuwa ni moja ya jimbo la kanisa katoliki na askofu wake ni aliyekuwa makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mt. Agustino upande wa taaluma anaitwa Fr. Dr Bernadin Mfumbusa.
 
Sikonge hata LAMI UCHWARA haipo na watu wanapangwa humo ndani kama meli ya kubeba Konteina.

Halafu basi lenyewe la Shakira unakuta hadi sakafu yake imetoboka chini na limepigwa welding kila kona.

Sisi sasa tusemeje? Ila wenyewe tulichagua November mwaka jana viongozi waliokuwepo waendelee.

Sasa leo tunamlilia nani? Utavuna ulichopanda.

Kaka umesahau konda ndiyo anakalia gia isichomoke, then moshi unatokea pale kwa juu. Gari likitaka kusimama linapunguza mwendo then konda anashuka na kipisi ya gogo kwenda kuweka kwenye tairi - hiyo ndiyo breaking system.

Mlio wakati wa kubadilisha gia kama una presha basi unataka roho.

Ukiangalia kwenye chesis ya gari imetoboka toboka kiasi unaona ardhi wakati gari lipo kwenye motion. Anashangaa nini jamaa? haya ndiyo matunda ya uhuru wetu 50 yrs.
 
Jamani msipindishe kauli,hiyo barabara ni kipande cha international road ya RSA TO MISRI.na kipande kuanzia mtera hadi mazengo shule ya msingi{mean iringa road} na kipande cha kuanzia mwisho wa lami maili mbili hadi babati kupitia kondoa ndo hakina lami. Na hela imeshatengwa na upembuzi yakinifu ulifanywa.katika bajet ya mwaka jana kama sio juzi,pesa yake ilitoka kwa pinde sana.
kwa maana hiyo tokea hili taifa lizaliwe, bajeti ya kujenga barabara ya kondoa ndo imepitishwa hivi karibuni
 
Jamani wana jf tembea uone, uangalie jinsi Tanzania ilivyo, nilibahatika kwenda kondoa miezi iliyopita hali ya uko hususan miundombinu ya barabara inatisha, mimi nilipanda basi la kondoa via kiteto, yani ile tunaiacha barabara ya kwenda makao makuu ya nchi na chama, barabara yote kuanzia hapo ni vumbi tupu na makorongo mbaya zaidi usafiri wa uko ni shida,watu wanabanana afadhali hata ya posta asubuhi, kwa kifupi wilaya nzima haina lami? Lami uchwara inaonekana kwenye daraja lilojengwa enzi za mkoloni, naona kwa wakazi wa hapo ambao hawajawahi kutoka nje ya wilaya yao lami wanaionea hapo, huwezi kudhani kama hapo ndo makao makuu ya wilaya nyumba za polisi utadhani mabanda ya ng'ombe, benki wana moja tu NMB.kondoa jinsi ilivyo utadhani si mji wa kihistoria, manake una michoro ya mapangoni na mali kare kibao. Kwa kifupi kondoa ovyo.

Hivi, wewe unatokea Mars, au unyamwezini, ili uyaone ya kondoa ya ajabu? Ulitegemea kuona kondoa ikoje kama DDM iko ilivyo! Ulitegemea Moro iweje Kama Dar haina hata flyover.

Come on, get real man/gal!
 
KOndoa is predominantly waislamu sawa tu na kigomaTatizo kubwa la pale limeshaelezwa hapo juu na kingine ni elimu duni... ni wilaya ya mwisho kwa performance ya form four mwaka 2010, huku wilaya hiyo ikiwa ndio iliyovunja rekodi kwa kuwa na barabara ya great north (cape to cairo) ambayo daraja lake la kolo lilivunjika a decade ago na hakuna kinachofanyika ingawa njia hiyo alipita sumaye, lowassa, nagu, nyang'anyi, wabunge wote wa mkoa wa arusha na manyara pamoja na mh sitta wa east africaMbunge wao inasemekana hajaonekana tena tangu ashinde ubunge
Dini zetu zinachangia kudumaa kwa maendeleo. Atakaebisha shauri yake
 
Wee MATAKA inaonekana ni mgenii hapa nchini, au umekuwa mtoto wa mjini maana unashangaa. Unashangaa nini? WENZIO TUSHAZOEA, ,MIMI KAZINI KWANGU KILA MWAKA HUWA NINAPATA BAHATI YA KWENDA MIKOANI NA HUCHAGUA MKOA NIUTAKAO, KWA SASA NIMESHAONA MENGI NA NIMECHOKA. MAENEO MENGINE UKIBAHATIKA KUKUTANA NA MAJI YA MTO YANATIRIRIKA UNASEMA ALHAMDULIAHI, UNAPIGA MAGOTI UNAKUNYWA KAMA NG'OMBE, MAANA HUJUI UTAKUTANA NAYO WAPI, USAFIRI SAHAU, HATA KAMA UNA HELA ZAKO HAKUNA CHA KUKODI HATA BAISKELI HAKUNA, UNACHAPA KWA MGUU KILOMETA 30, NA KUENDELEA. SEMBUSE WEWE HUKO KUNA BASI JAPO NI UCHWARA.KAZI NI KWAKO
mimi nimeshazoea kwetu, kwanza natoka mikoa maskin zaidi Tanzania kwa hiyo kitu kama icho nakiona cha kawaida,sisi kwetu hatujui umeme, barabara wala maji, tunategemea maji kipindi cha mvua yanayokaa kwenye mashamba ya mpunga.

Ila nimeshangaa kama haya matatizo yapo hata sehemu zinazoonekana zimeendelea. Sisi usafiri tunaoutegemea ni wanten land rover chakavu safari moja kwa siku toka kijijin kwenda mjini kabla ya hapo tulikuwa tunatembea kwa miguu
 
kinachorudisha nyuma watu wa kondoa ni unafiki, udini, elimu duni na kumsikiliza mbunge mpumbavu na aliyelaaniwa kama zabein mhitaBan me mods
umesahau na uchawi
 
Hivi, wewe unatokea Mars, au unyamwezini, ili uyaone ya kondoa ya ajabu? Ulitegemea kuona kondoa ikoje kama DDM iko ilivyo! Ulitegemea Moro iweje Kama Dar haina hata flyover.Come on, get real man/gal!
nimetokea pluto
 
Haaaa Hahaaa, maasi ya Seif Hamdani sijui? Maana Sabena walau alikuwa na nafuu. Elnino, kuna Group wameanzisha vijana kwenye Facebook linaitwa Tabora Ndio Kwetu na Sikonge Development. Karibu sana huko ukipata nafasi. Naona wameweka hadi picha ya Sabena leo, hahaaa.....

Chini ni Bus la SHAKIRA. Angalia dirishani jinsi walivyounga kwa kuchomelea badala ya mipira ya kushika kioo...

Shakira.JPG


Kaka umesahau konda ndiyo anakalia gia isichomoke, then moshi unatokea pale kwa juu. Gari likitaka kusimama linapunguza mwendo then konda anashuka na kipisi ya gogo kwenda kuweka kwenye tairi - hiyo ndiyo breaking system.

Mlio wakati wa kubadilisha gia kama una presha basi unataka roho.

Ukiangalia kwenye chesis ya gari imetoboka toboka kiasi unaona ardhi wakati gari lipo kwenye motion. Anashangaa nini jamaa? haya ndiyo matunda ya uhuru wetu 50 yrs.
 
Watu wa kondoa hawajui chama kingine zaidi ya CUF au CCM.

Mimi nimesoma shule ya Miningani kama unaenda kondoa girls, darasani tulikua wakristu wawili tu.
Shule nzima ilikuwa na wakristu wasiozidi 20.




Sasa ukristu unahusiana nini na maendeleo ya kondoa?
Mbona unaongea upupu?
Kama hauna cha kuchangia kaa kimya, sio udini usiokua na msingi.
 
kinachowaua warangi ni ile division ya udini inayopandwa na wachache.... imefikia hatua hata kama unapita tu kwennda babati au hata kiteto unaweza kuulizwa dini, ole wako useme mkristu

watakuacha hapohapo hata kama umepata matatizo
chuki zingine bwana ni shida sana. HAta uwachukie waislam wewe si wa kwanza na wala si wa mwisho. Mungu akusamehe kwa kuongopa humu.
 
ukitaka kujua udini na ukabila ni kitu gani nenda kondoa mkuu.. hawa watu hata wasome vipi haya mambo hawaachi + unafiki



ushirikina hapo mkuu wakubwa wako wa nchi ndio wanapozindikwa, huwa wanatunga ziara za huko kwakutumia helicopter hahahaaaa nakumbuka mkulu aliyepita alitua pale nakupikwa vilivyo na wazee wa pilau ambapo mmoja alikuja kuwa mkuu wa baraza la pilau tz
so sad. ninachokiona hapa ni kejeli na dharau tu wala si kingine.
 
wakristo wakondoa hebu tuthibitishieni hivi ni kweli huko kondoa mnatengwa kama inavyodaiwa hapa? gari ikiwakuta njiana inawaacha? Mbona nyie watu wa JF mnachuki hivi. DU!
kweli hii ni chadema forum, the home of christians Hypocrites.
 
Jamani msipindishe kauli,hiyo barabara ni kipande cha international road ya RSA TO MISRI.na kipande kuanzia mtera hadi mazengo shule ya msingi{mean iringa road} na kipande cha kuanzia mwisho wa lami maili mbili hadi babati kupitia kondoa ndo hakina lami. Na hela imeshatengwa na upembuzi yakinifu ulifanywa.katika bajet ya mwaka jana kama sio juzi,pesa yake ilitoka kwa pinde sana.

Yale yale kama misamiati ya ndugu yetu Ngeleja, upembuzi yakinifu, mpango wa muda mrefu na kadhalika. Hivi bado kuna ndoto ya kuwa na barabara ya lami kutoka Cape Town mpaka Cairo?

I dought! Na kama ndoto hiyo bado ipo, ndiyo tumekaa tu kusubiri mpaka Umoja wa Afrika uje kujenga hiyo barabara? Sielewi. Ila nashindwa kuyazoea majibu rahisi kwenye maswali magumu ndani ya viongozi wa nchi hii.

Ndio maana wazungu wanawadharau sana na Ijumaa hii wataandaliwa chakula cha jioni na Vodacom, kwa kuwa posho haziwatoshi kujinunulia chakula.
 
wakristo wakondoa hebu tuthibitishieni hivi ni kweli huko kondoa mnatengwa kama inavyodaiwa hapa? gari ikiwakuta njiana inawaacha? Mbona nyie watu wa JF mnachuki hivi. DU!kweli hii ni chadema forum, the home of christians Hypocrites.
si ndo hapo! Kila nikijaribu kureflect wapi kuna ubaguzi wala siuoni, mbona watu wa uko wamemlimia kamanda wao shamba zima la mahindi,walichokifanya ni kumkabidhi yakiwa tayari yameshavunwa na ni magunia kibao. Na huyo kamanda ni mkristo. Mbona nimekaa mwezi mzima sijaona element za udini?.

Pia watumishi wa uko wengi si wazawa na wana kuja dini mchanganyiko mbona wanaishi tu vizuri na wazawa? Acheni unafki mnaojiita great thinkers kumbe ni low thinkers!
 
Unajua, tunapochangia mada na kuanza kuponda kitu kwa misingi ya udini, tunabomoa na si kujenga, hivi nyinyi mnaofanya ivyo hamjui ndo mnahiaribu cdm badala ya kukujinga? Kwa mnachokifanya msitegemee kupata waislam kujiunga na cdm. Hebu mbowe na crew yako take action wanakuharibia hawa jamaa.
 
wakristo wakondoa hebu tuthibitishieni hivi ni kweli huko kondoa mnatengwa kama inavyodaiwa hapa? gari ikiwakuta njiana inawaacha? Mbona nyie watu wa JF mnachuki hivi. DU!kweli hii ni chadema forum, the home of christians Hypocrites.
kwahilo la gari kuwaacha njiani wakristo sina hakika nalo, nisingependa mfikirie kama uislamu ni mbaya la hasha to be honest maendeleo ya kondoa yamedumazwa na udini ambapo elimu dunia haipewi uzito na uktaka kudhibtsha hilo kwa kijiji kama HAUBI ambapo kuna wakristo wengi kwa kiasi fulani kuna maendeleo na hata warangi wengi walioosoma kama kina Prof semesi(RIP), jaji lubuva, damian foka katbu mkuu mstaafu wa bunge n.k wametokea eneo hilo.
 
Back
Top Bottom