Mungu wangu! Siamini kama ile ni kondoa

Mungu wangu! Siamini kama ile ni kondoa

kinachowaua warangi ni ile division ya udini inayopandwa na wachache.... imefikia hatua hata kama unapita tu kwennda babati au hata kiteto unaweza kuulizwa dini, ole wako useme mkristu

watakuacha hapohapo hata kama umepata matatizo

ukitaka kujua udini na ukabila ni kitu gani nenda kondoa mkuu.. hawa watu hata wasome vipi haya mambo hawaachi + unafiki

MTM kwenye orodha yako umesahau ushirikina.

Btw: mbunge wao ni nani tena?

ushirikina hapo mkuu wakubwa wako wa nchi ndio wanapozindikwa, huwa wanatunga ziara za huko kwakutumia helicopter hahahaaaa nakumbuka mkulu aliyepita alitua pale nakupikwa vilivyo na wazee wa pilau ambapo mmoja alikuja kuwa mkuu wa baraza la pilau tz
 
Sikonge hata LAMI UCHWARA haipo na watu wanapangwa humo ndani kama meli ya kubeba Konteina.Halafu basi lenyewe la Shakira unakuta hadi sakafu yake imetoboka chini na limepigwa welding kila kona.Sisi sasa tusemeje? Ila wenyewe tulichagua November mwaka jana viongozi waliokuwepo waendelee.Sasa leo tunamlilia nani? Utavuna ulichopanda.
mkuu nilikuwa ipole wilayan sikonge barabara mbovu mno, hata ya nzega tbr nayo mbaya mpaka magari yanazungukia bukene kwenye unafuu, kwa kifupi tabora haina barabara
 
that is so unfair, yaani kumbe wao wanenda kupigiwa madogoli huko kwa helkopta ndo maana hata hawawakumbuki waganga wao japo kabarabara ka lami!



Tuache na masihara, mimi hiyo inanikera sana aisee! Yaani wanatia huruma! Kukamatana uchawi tu. Ndo maana wanajisahau hata kutahmini utendaji wa viongozi wao.
 
Hii nchi jamani bado iko nyuma saaana tena saana, ukienda wilayani na vijijini ndo utajua hakuna kilichofanyika toka uhuru, mweeeeeee sijui watanganyika wamelogwaaaaaa
 
Samahani wapendwa naomba kuuliza. Wenyeji wa kondoa wengi wao ni Dini gani?
 
Katika nchi yetu hali za vijiji ni mbaya sana,unaongelea barabara peke yake nenda kwenye maswala ya maji huko utatoa machozi kwani mabomba yanatoa kutu na tope.mungu ibariki tanzania.
mkulu unaongelea mabomba! Kijijini kwetu tunachota kwenye visima vya asili!
 
dini inahusika vipi na haya matatizo bana?

Kama ishu ni udini lazima kutahusisha dini zaidi ya moja.
kuna wakristo na waislamu kule.
 
Sikonge hata LAMI UCHWARA haipo na watu wanapangwa humo ndani kama meli ya kubeba Konteina.

Halafu basi lenyewe la Shakira unakuta hadi sakafu yake imetoboka chini na limepigwa welding kila kona.

Sisi sasa tusemeje? Ila wenyewe tulichagua November mwaka jana viongozi waliokuwepo waendelee.

Sasa leo tunamlilia nani? Utavuna ulichopanda.
Mimi siku hizi nimebadili mawazo mkuu Sikonge,lawama zote nawatupia wananchi walioridhika na shida hizo.Advantage walioitumia wakoloni weupe ndiyo inayotumiwa na hawa wakoloni weusi.

Tena afadhali hata mkoloni mweupe alijenga barabara licha ya kwamba zilikuwa ni strategically kwa ajili ya usafirishaji wa malighafi,lakini bado zimewasaidia wananchi na ndizo zinazoonekana hadi leo.

Juhudi za kujikomboa zitatokana na wananchi wenyewe. Akijitokeza wa kuwakomboa kama na yeye ana maslahi yake binafsi, then ni vigumu kuwafanyia kazi wananchi wajinga. Ujinga wa watanzania ni kama mwanamke mwenye kimini kwa mbakaji(mafisadi)Unawatamanisha kutaka madaraka ili waendeleze ubakaji.

Mkuu nimeshaanza kukata tamaa.Ila wananchi nitawapa vidonge vyao.Ni ujinga wao unao wa attract mafisadi. Unadhani wananchi wangekuwa ngangari kuna kiongozi mwenye nia mbovu ataomba madaraka.
 
Nimepita hiyo njia ya Kondoa kuelekea Kiteto. Safari yangu ilikuwa inaishia Matui. Matui ni sehemu iliyochangamka kidogo maana kuna wakulima wa kati wa mahindi, maharage alizeti n.k. Kilimo cha huko tunaweza sema ni cha wakulima wa kati maana wao hata zana zao za kilimo ni bora zaidi (matrekta ya kulima na kupukuchua mahindi ni mengi sana eneo lile), kwa hiyo kipato chao si haba.

Wakati naingia Matui, nilifarijika kuonga nguzo zinazofanana na za simu. Nikawa nashangaa iweje kusiwe na umeme lakini kukawa na huduma ya simu? Kumbe zilikuwa cable za TV watu wameunganishiana-huku wakitumia umeme wa Jenereta. Hili lilinifurahisha maana kama watu wanapata habari, wanaweza kupata ukombozi-hata kama utachelewa.

Barabara ni za vumbi (wala si changarawe) mwanzo mpaka mwisho. Lakini lililonisikitisha zaidi ni mabwawa ya maji yaliyochimbwa kando kando ya barabara. Haya si mabwawa yaliyochimbwa kitaalaam kama bwawa la Mindu Morogoro, ni mabwawa yaliyojaa tope. Literally, maji ya kwenye mabwawa hayo ni matope, ni maji ambayo hata ng'ombe huwezi kumpa anywe kama unajali afya yake. Hayo maji ya kwenye mabwawa ndio wanayokunywa ndugu zetu-yanatumika kwa kila kitu. Kama ni kunywa, wao huyaacha yatuame kwanza na hutumia.

Mtu mwenye nia ya dhati kabisa ya kutuongoza, lazima ayajue maisha wanayoishi watu wa vijijini. Naamini kama ni mbabaishaji, roho itamsuta. Mantiki yangu ni kwamba, kuna jamii ambazo zinaweza kumudu gharama za huduma muhimu kama maji na umeme, lakini haziwezi kupata huduma hizo kwa kuwa serikali haijaweka miundombinu.
 
Kama umeshawahi kutembea nje ya nchi ama kuishi nje ya nchi,basi utapatwa na hasira mara mia zaidi tofauti na ikiwa hujawahi toka nje ya bongo kabisa. Ndo maana viongozi wengi wanawachukia wananchi walio nje ya nchi na kuwaita wabeba box.

Kiukweli utakuwa na hasira zaidi na it really pains ukiangalia maisha ya wananchi.

Kuanzia wa mijini hadi vijijini. Na hasira hiyo inaweza kuwa mbaya sana.
 
Katika nchi yetu hali za vijiji ni mbaya sana,unaongelea barabara peke yake nenda kwenye maswala ya maji huko utatoa machozi kwani mabomba yanatoa kutu na tope.mungu ibariki tanzania.
mkuu hapo kwenye red mkuu ashasema kuna ukame...........kama mnataka maji tengenezeni mawingu mvua inyeshe mito na maziwa yajae maji...
habari ndo hiyo!!!
 
AKondoa-Mjini+(26).jpg


Mheshimiwa Kikwete akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kondoa, Mheshimiwa Zubein Mhita baada ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni Kondo Mjini leo hii.

Maelfu ya wanachama wa CCM wamempa mapokezi makubwa Mwenyekiti wa CCM taifa na mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Kondoa mjini alipowasili kufanya mkutano wa kampeni.



Mheshimiwa Kikwete alichukua muda mwingi wa hotuba yake kufafanua jitihada zitakazochukuliwa na CCM kama ikirudi kuongoza serikali kuhakikisha kuwa huduma bora ya afya inapatikana kwa kila Mtanzania. Alielezea ujenzi wa zahanati kila kata, utoaji wa vyandarua viwili kwa kila kaya, na jitihada za kuchanja wanawake bure kuzuia kansa ya shingo ya uzazi.



Kwa upande wa utoaji huduma ya maji, Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa vijiji 27 vya Kondoa Mjini vitapata maji ya uhakika kwa kupitia mpango mkubwa wa kusambaza maji kwa kushirikiana na Benki ya dunia. Mheshimiwa Kikwete alisema wilaya nyingi nchini mpango huu unashirikisha vijiji 10 hadi 15, lakini kwa kutambua ukubwa wa tatizo la maji Wilayani Kondoa ndipo maamuzi ya vijiji 27 yalifikiwa.



Mheshimiwa Kikwete pia alifafanua mafanikio yaliyopatikana kwenye upande wa elimu ya msingi na sekondari, sekta ya kilimo na mifugo, uwezeshwaji wa wananchi kiuchumi na ujenzi wa barabara.



Mwishoni Mheshimiwa Kikwete aliwanadi wagombea udiwani na ubunge na kuomba wananchi wachague CCM na wagombea wote kwa staili ya mafiga matatu.


Inaudhi sana pale watu wanapokuamini na kukupa kura uwatetee halafu unaenda Mjengoni unaungana na wapumbavu wengine na kupoteza muda mwingi huku mkibishania POSHO ZENU ZIONGEZWE NA MTU ASISUBUTU KUFUTA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! kufaa kwake kupo wapi??????
 
Samahani wapendwa naomba kuuliza. Wenyeji wa kondoa wengi wao ni Dini gani?
KOndoa is predominantly waislamu sawa tu na kigoma

Tatizo kubwa la pale limeshaelezwa hapo juu na kingine ni elimu duni... ni wilaya ya mwisho kwa performance ya form four mwaka 2010, huku wilaya hiyo ikiwa ndio iliyovunja rekodi kwa kuwa na barabara ya great north (cape to cairo) ambayo daraja lake la kolo lilivunjika a decade ago na hakuna kinachofanyika ingawa njia hiyo alipita sumaye, lowassa, nagu, nyang'anyi, wabunge wote wa mkoa wa arusha na manyara pamoja na mh sitta wa east africa

Mbunge wao inasemekana hajaonekana tena tangu ashinde ubunge
 
achilia mbali njia ya babati au ile ya kiteto.hebu jaribu kupita njia inayoenda kondoa kupitia njia panda ya zamayero au kule ovaada/kwamtoro utalia .yani barabara mwanzo mwisho ni korongo tene ukizingatia ule msitu wenye mbung'o usipo jipepea namajani utang'atwa mpaka ukome na homa yake usipime.halaf basi zenyewe kinanda na machame line zinapita tu bila waswas.mi naona matajiri wa mabasi waanzishe mgomo il serikali itengeneze barabara.
 
Poleni tataizo si tu kuwa na mbunge wa CCM bali mbunge huyo kujua wajibu wake.

Pamoja na picha inayoonekana Kondoa mbunge huyo siku zote anawakilisha hoja za serikali na si wananchi wake. Badala ya kuwakilisha matatizo ya jimbo lake anachoweza best ni kusifia serikali wakati hapo Kondoa upatikaji wa maji ni shughuli kweli kweli.
 
Samahani wapendwa naomba kuuliza. Wenyeji wa kondoa wengi wao ni Dini gani?
kabila kubwa ni Warangi ambalo linapatkana karbu eneo lote la wilaya. Pia kuna waburunge, wasi, wasandawe na wafyomi. Mbunge Nkamia
 
Sikonge hata LAMI UCHWARA haipo na watu wanapangwa humo ndani kama meli ya kubeba Konteina.

Halafu basi lenyewe la Shakira unakuta hadi sakafu yake imetoboka chini na limepigwa welding kila kona.

Sisi sasa tusemeje? Ila wenyewe tulichagua November mwaka jana viongozi waliokuwepo waendelee.

Sasa leo tunamlilia nani? Utavuna ulichopanda.

Mkuu Tabora karibu yote haina lami,zaidi ya ile inayopta Igunga-Nzega-Shy.Hata pale mjini mni vumbi tu.Ndo nchi yetu hii .
 
Back
Top Bottom