Mungu wangu! Siamini kama ile ni kondoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu wangu! Siamini kama ile ni kondoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mataka, Jul 20, 2011.

 1. m

  mataka JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Jamani wana jf tembea uone, uangalie jinsi Tanzania ilivyo, nilibahatika kwenda kondoa miezi iliyopita hali ya uko hususan miundombinu ya barabara inatisha, mimi nilipanda basi la kondoa via kiteto, yani ile tunaiacha barabara ya kwenda makao makuu ya nchi na chama, barabara yote kuanzia hapo ni vumbi tupu na makorongo mbaya zaidi usafiri wa uko ni shida,watu wanabanana afadhali hata ya posta asubuhi, kwa kifupi wilaya nzima haina lami? Lami uchwara inaonekana kwenye daraja lilojengwa enzi za mkoloni, naona kwa wakazi wa hapo ambao hawajawahi kutoka nje ya wilaya yao lami wanaionea hapo, huwezi kudhani kama hapo ndo makao makuu ya wilaya nyumba za polisi utadhani mabanda ya ng'ombe, benki wana moja tu NMB.kondoa jinsi ilivyo utadhani si mji wa kihistoria, manake una michoro ya mapangoni na mali kare kibao. Kwa kifupi kondoa ovyo.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sikonge hata LAMI UCHWARA haipo na watu wanapangwa humo ndani kama meli ya kubeba Konteina.

  Halafu basi lenyewe la Shakira unakuta hadi sakafu yake imetoboka chini na limepigwa welding kila kona.

  Sisi sasa tusemeje? Ila wenyewe tulichagua November mwaka jana viongozi waliokuwepo waendelee.

  Sasa leo tunamlilia nani? Utavuna ulichopanda. (Chini, SHAKIRA BUS upande wa kushoto).

  [​IMG]
   
 3. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiyo faida ya Miaka 50 ya Uhuru ngoja wakazi wa Kondoa wafaidi matunda ya Uhuru. Kisha napenda kujua jimbo hilo safari hii linaongozwa na Mbunge wa Chama gani?. Kama bado ni wa CCM no comment hiyo ni halali yao.
   
 4. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,017
  Likes Received: 3,201
  Trophy Points: 280
  Watu wa kondoa hawajui chama kingine zaidi ya CUF au CCM.

  Mimi nimesoma shule ya Miningani kama unaenda kondoa girls, darasani tulikua wakristu wawili tu.
  Shule nzima ilikuwa na wakristu wasiozidi 20.
   
 5. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hiyo ya Kondoa ni picha tu nenda Kbondo ukaone ya dunia kuna basi la Mwarabu linatoka Kigoma hadi Kahama lenyewe tu ni vumbi linalotembea ukiwa ndani unaweza kuona hata matairi yanavyozunguka lakini bado linapakia binadamu,kwa maeneo ya Kondoa Babati au kanda ya kaskazini haliwezi kupakia hata ng`ombe sembuse binadamu, lakini linafanya kazi na polisi wanaliangalia tu.
   
 6. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wee MATAKA inaonekana ni mgenii hapa nchini, au umekuwa mtoto wa mjini maana unashangaa. Unashangaa nini? WENZIO TUSHAZOEA, ,MIMI KAZINI KWANGU KILA MWAKA HUWA NINAPATA BAHATI YA KWENDA MIKOANI NA HUCHAGUA MKOA NIUTAKAO, KWA SASA NIMESHAONA MENGI NA NIMECHOKA. MAENEO MENGINE UKIBAHATIKA KUKUTANA NA MAJI YA MTO YANATIRIRIKA UNASEMA ALHAMDULIAHI, UNAPIGA MAGOTI UNAKUNYWA KAMA NG'OMBE, MAANA HUJUI UTAKUTANA NAYO WAPI, USAFIRI SAHAU, HATA KAMA UNA HELA ZAKO HAKUNA CHA KUKODI HATA BAISKELI HAKUNA, UNACHAPA KWA MGUU KILOMETA 30, NA KUENDELEA. SEMBUSE WEWE HUKO KUNA BASI JAPO NI UCHWARA.

  KAZI NI KWAKO
   
 7. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  itakuwa ni sababu maana hawa jamaa huwa hawana maono ni
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mheshimiwa Kikwete akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kondoa, Mheshimiwa Zubein Mhita baada ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni Kondo Mjini leo hii.

  Maelfu ya wanachama wa CCM wamempa mapokezi makubwa Mwenyekiti wa CCM taifa na mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Kondoa mjini alipowasili kufanya mkutano wa kampeni.  Mheshimiwa Kikwete alichukua muda mwingi wa hotuba yake kufafanua jitihada zitakazochukuliwa na CCM kama ikirudi kuongoza serikali kuhakikisha kuwa huduma bora ya afya inapatikana kwa kila Mtanzania. Alielezea ujenzi wa zahanati kila kata, utoaji wa vyandarua viwili kwa kila kaya, na jitihada za kuchanja wanawake bure kuzuia kansa ya shingo ya uzazi.  Kwa upande wa utoaji huduma ya maji, Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa vijiji 27 vya Kondoa Mjini vitapata maji ya uhakika kwa kupitia mpango mkubwa wa kusambaza maji kwa kushirikiana na Benki ya dunia. Mheshimiwa Kikwete alisema wilaya nyingi nchini mpango huu unashirikisha vijiji 10 hadi 15, lakini kwa kutambua ukubwa wa tatizo la maji Wilayani Kondoa ndipo maamuzi ya vijiji 27 yalifikiwa.  Mheshimiwa Kikwete pia alifafanua mafanikio yaliyopatikana kwenye upande wa elimu ya msingi na sekondari, sekta ya kilimo na mifugo, uwezeshwaji wa wananchi kiuchumi na ujenzi wa barabara.  Mwishoni Mheshimiwa Kikwete aliwanadi wagombea udiwani na ubunge na kuomba wananchi wachague CCM na wagombea wote kwa staili ya mafiga matatu.


   
 9. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Wananchi nao bila ya kuchanganya na .....zao, wakachagua kweli CCM!!

   
 10. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  kama ni sehemu ya historia wanarekebisha ya nini? maajabu ya kuandika ungeyapata wapi, hawa watu wanaogopa kenya isijesema na kwenyewe ni sehemu ya mali yao ya historia kwa kuwa binadamu wa kale alipatika pale, wakiboresha njia itakula kwetu, waache wabaki hivyo hivyo kama hifadhi ya taifa, isije haribiwa kama makumbusho sehemu ya hifadhi inakuwa ya burudani na uaribifu alafu unaita makumbusho!!! tunakmbuka nini pale kwenye starehe?
   
 11. V

  Vonix JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu mbunge wao mbona hata bungeni hasikiki akisema au kumbana magufuli atengeneze barabara ya dodoma-kondoa anapokea posho tu na kupiga uzingizi kweli wajinga ndio waliwao,hapo ndio unajiuliza kila mahali watu wamelogwa tu.
   
 12. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jamani msipindishe kauli,hiyo barabara ni kipande cha international road ya RSA TO MISRI.na kipande kuanzia mtera hadi mazengo shule ya msingi{mean iringa road} na kipande cha kuanzia mwisho wa lami maili mbili hadi babati kupitia kondoa ndo hakina lami. Na hela imeshatengwa na upembuzi yakinifu ulifanywa.katika bajet ya mwaka jana kama sio juzi,pesa yake ilitoka kwa pinde sana.
   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Wakuu simulizini zenu zimeniacha mbavu sina!!! Naona itabidi tuanzishe thread wachangiaji wawe wanatoa shuhuda za aina hii kutoka vijiji mbalimbali...
   
 14. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Katika nchi yetu hali za vijiji ni mbaya sana,unaongelea barabara peke yake nenda kwenye maswala ya maji huko utatoa machozi kwani mabomba yanatoa kutu na tope.mungu ibariki tanzania.
   
 15. k

  kakolo Senior Member

  #15
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  We hapo umependekeza kweli, mi nipo Kahama huku sasa shughuli zangu ziko vijijini hayo mnayosema ni ya kawaida. Acha barabara hazina lami, Bomba watu hawalijui, huduma za afya hadi Kahama mjini. Kama wana mgonjwa mikokoteni ya ng'ombe inakesha na huko Kahama wanapiga kambi hospitali wanapika hapohapo. Vijiji kama Kawe, Ishiki, Budutu, Ufala, yaani huenda wanajua Nyerere bado rais. Hali mbaya sana hata kama kuna njaa hakuna takwimu. Kuna kazi kubwa sana kuwaelimisha na serikali ina take advantage kutowafumbua macho ili iongoze kwa urahisi. Ila wkt Wa vita vya Uganda kila mji ulichangishwa ng'ombe mmoja eti mboga ya wanajeshi!! Sijui kama ilikuwa sera ya serikali au ufisadi ulifanyika. It's very sad talking about this.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kinachorudisha nyuma watu wa kondoa ni unafiki, udini, elimu duni na kumsikiliza mbunge mpumbavu na aliyelaaniwa kama zabein mhita

  Ban me mods
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kinachowaua warangi ni ile division ya udini inayopandwa na wachache.... imefikia hatua hata kama unapita tu kwennda babati au hata kiteto unaweza kuulizwa dini, ole wako useme mkristu

  watakuacha hapohapo hata kama umepata matatizo
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hivi unamjua vizuri huyu mama?
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  MTM kwenye orodha yako umesahau ushirikina.

  Btw: mbunge wao ni nani tena?
   
 20. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,240
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa kuishi "Posta" miaka yote hiyo. Yanii ndo'umeanza leo kiijua nchi yako? Ukitoka huko pita na Makete, kibondo, chamwino, kantaramba, na kwingineko alafu ndo'uchukue hatua..
   
Loading...