Mungu wa kweli hahitaji haya tunayoaminishwa

Mimi sijakataa wao wasipewe sadaka Mkuu. Ninachokataa ni wao kusema Mungu ndiye anataka sadaka tena wameenda mbali zaidi kwa kusema fungu la kum(9zaka) ni la Mungu jambo ambalo si kweli. Tunajua umuhimu wa huduma yao lakini isiwe sababu ya wao kumsingizia Mungu eti anahitaji zaka. Tena ni lazima.
Hahahahahahaha
 
Fungu la kumi lipo moyoni mwako ,jamii inayokuzunguka watu wenye shida unawafahamu , wape mwenyewe , achana na hizi taasisi za wapiga dili . Wanadiriki kusema Mungu anahitaji pesa !! Ni uwongo mchana kweupeee !!


Binafsi nitawapa kutokana na huduma zao lakin si kwa kutishwa na kuogopeshwa eti namuibia Mungu. Hivi mali yako inaweza kujiiba yenyewe.
 
Unacheka nin Boss
Mkuu kuna agenda kubwa sana ya hawa viongozi wa dini kwenye suala zima la sadaka na zaka, hususan viongozi wa makanisa. Sadaka katika uislam zimeshajihishwa zielekezwe kwa wahitaji na kuna aya nzima kwenye qur an inayozungumzia hilo na mgawanyo unatakiwa uweje. Tena mpaka mpangilio wa wanaopata hizo sadaka. Yaani anatakiwa apate nani kwanza halafu nani apate baadae. Mtume Muhammad (s.a.w) anatuambia hakuna sadaka bora zaidi ya ile unayowapa wazazi wawili, halafu watu wa nyumbani, halafu majirani, halafu maskini, halafu wapita njia, mlolongo unaendeleeaaaa. Hawa wanakuja wakaomba wakaomba misikitini wanakuwa ni magumashi tu na ki-ukweli hili suala ni zito zaidi makanisani kwa uono wangu
 
Mkuu kuna agenda kubwa sana ya hawa viongozi wa dini kwenye suala zima la sadaka na zaka, hususan viongozi wa makanisa. Sadaka katika uislam zimeshajihishwa zielekezwe kwa wahitaji na kuna aya nzima kwenye qur an inayozungumzia hilo na mgawanyo unatakiwa uweje. Tena mpaka mpangilio wa wanaopata hizo sadaka. Yaani anatakiwa apate nani kwanza halafu nani apate baadae. Mtume Muhammad (s.a.w) anatuambia hakuna sadaka bora zaidi ya ile unayowapa wazazi wawili, halafu watu wa nyumbani, halafu majirani, halafu maskini, halafu wapita njia, mlolongo unaendeleeaaaa. Hawa wanakuja wakaomba wakaomba misikitini wanakuwa ni magumashi tu na ki-ukweli hili suala ni zito zaidi makanisani kwa uono wangu


Yaani unalikuta ljitu hata halisaidii wazazi wake, wala watoto wa ndugu zake, au majirani lakini usishangae huko kwenye mahekalu akifanya fujo za sadaka na harambee
 
Mungu unamjua automatic tuu bila kuambiwa na mtu. Kama watu wasingeletewa dini bado wangejua Mungu yupo.

Nimemtaja Yesu kwa Muktadha wa wakristo(Nikiwa miongoni mwao na najivunia kuwa miongoni mwa wakristo ambao ni watu bora katika zama hizi)

Huko kanisani kwenu wanatumia mbinu gani kupata sadaka hasa katika uhamasishaji?
Mh..unamjuaje Mungu bila kufahamishwa?
 
Naomba uzungumzie upande wa Pili
Ama kuhusu Waislam,samahani,hili litoe kbs Chief

Uislam halisi,haukusanyi Sadaka na Zaka,kisha wakala Masheikh!!!
Hili hakuna Kisheria

Zaka
Ni mali ambazo,huchukuliwa kutoka kwa Matajiri na kupelekwa kwa Maskini

Huu ndio Uislam
Kadhalika sadaka
Habari wakuu!

Mungu wa kweli, mwenye uweza wote, na aliyeumba kila kitu hahitaji mambo yafuatayo:-

1. Hahitaji Zaka wala Sadaka
Mungu wa kweli si mhitaji, uhitaji ni karba ya viumbe. Mungu hana anachohitaji kutoka kwa kiumbe. Yeye ndiye huamua nini kiwe na nini kisiwe. Mungu wa kweli hahitaji sadaka kama watu wengi wanavyoaminishwa. Hahitaji zaka kama wachungaji wanavyosema. Wachungaji wanamsingizia Mungu mambo mengi ikiwemo hili la zaka na sadaka. Wanachoshindwa kusema ni kuwa wao ndio wanahitaji hizo zaka na sadaka kama sehemu ya huduma yao. Ni uongo na dhambi kubwa kusema Mungu anataka sadaka na zaka jambo ambalo linamdhalilisha Mungu muweza wa yote.

Wachungaji, mashehe na viongozi wote wa dini kwa majina yao. Muache kuhadaa watu na kumdhalilisha Mungu. Tutatoa sadaka na zaka kwa kujua kuwa mnatupa huduma za kiroho na si kusema kuwa Mungu anahitaji sadaka na zaka tena fungu la kumi. Kama tunawalipa waalimu, madaktari, wanasheria na kada zingine iweje tusiwalipe nyie. Kwa nini mumsingizie Mungu mambo ya uongo. Eti fungu la kumi ni la Mungu. Si kweli. Mtu atatoa zaka na sadaka kulingana na umuhimu wa huduma anayoipata na si kumtishia vitisho vya uongo.

2. Kafara si ondoleo la dhambi
Watu wameaminishwa kuwa eti ili mtu asamehewe dhambi basi sharti amwage damu. Zamani walimwaga damu ya wanyama lakini sasa hivi wanaamini kuwa Yesu(mtu ninayemheshimu sana) alikufa kwa ajili ya watu jambo ambalo ni uongo. Mungu wa kweli hawezi kufikiri achilia mbali kutenda jambo kama hilo. Hiyo ni mila za kuabudu miungu ya Kiyahudi ambayo msingi wake mkuu umetokana na Abrahamu aliyechukua baadhi ya mila za Kiashuru( kwa sasa ni Syria). Miungu ya Abrahamu ndiyo ilimtaka amtoe Isaka kafara kama ilivyodesturi.

Mungu wa kweli hahitaji mchakato huo kusamehe dhambi, na kumwaga damu si suluhu ya dhambi kuishi. Kwa kutambua hili jambo hili moja kwa moja linaonekana ni wazo la kibinadamu zaidi kuliko la Mungu.

3. Maombi hayabadili chochote kwa Mungu mwenye uweza.
Wachungaji, mashehe na viongozi wa dini wengine kwa majina yao wanawadanganya watu kuwa ukimuomba Mungu jambo lolote anaweza akakupa kitu ambacho si kweli hata kidogo. Vile Mungu alivyopanga kabla hajakuumba ndivyo itakavyokuwa. Kusema kuwa ukimuomba Mungu anabadili mipango yake ni kujidanganya na kupoteza muda. Kumuomba Mungu ni kumfundisha namna ya kufanya mambo yake. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kuwa mtu akiomba jambo kwa Mungu hupewa isipokuwa ushahidi uliowazi ni kuwa Mtu akifuata maagizo ya Mungu na sheria zake ndio hupata akitakacho. Mungu anataka watu wafuate sheria zake na si kuomba omba tuu.

Hii inamaanisha kuwa viongozi wa dini jukumu lao ni kuwafundisha watu sheria za Mungu na si kuwadanganya waombe au kuwaombea. Kuwaombea watu ni kuwafundisha uvivu. Na kuamini katika hamna.

Ukitaka uamini nikisemacho, kaa ndani omba alafu usiende kufanya kazi uone kama Mungu atakupa ukitakacho, alafu mwenzako asiombe aende kufanya kazi uone nani atapewa/atapata. Hakuna sheria ya Mungu mahali popote kwenye torati inayomtaka mtu aombe. Tafsiri yake nadhani mnaelewa ni nini. Usishangae kwa nini bara la Afrika ni masikini ilhali ndilo linaloongoza kwa waumini wenye kuomba makanisani na misikitini. Jibu unalo.

4. Wachungaji/mashehe na viongozi wa dini si watu pekee wanaotakiwa kuheshimiwa.
Kuna dhana watu huaminishwa kuwa kundi fulani la watu ndilo linalotakiwa kupewa heshima kuliko kundi jingine. Huu ni uongo mkubwa. Mchungaji ni mtumishi kama walivyo watumishi wengine. Anahudumia watu kama wanavyohudumia wengine. Hana uspesho wowote zaidi ya wao kuwahadaa watu wenye akili ndogo na wasioujua ukweli ndio maana wamegeuka watumwa wa makuhani na mashehe. Kila mtu duniani anahitaji heshima ikiwa anafanya kazi ya kuhudumia wengine. Iwe ni fundi nguo, fundi magari, mbunge, mwalimu, muuguzi, mhandisi wote wapo sawa na wote wanategemeana. Kumpa mtu fulani heshima kuliko mwingine si tu kwamba ni ukosefu wa maarifa bali ni kuonyesha hali ya kutoujua ukweli.'

Viongozi wa dini wamejipa hadhi kubwa na kujiona wao ndio wenye mamlaka. Usishangae kiongozi wa dini mjinga akisema kuwa anakulaani kwa Mungu. Nikisiaga hivi huwa nacheka sana. Mtu hupata laana kwa kuacha sheria za Mungu na si maneno ya Mchungaji au mzazi. Kwa ujumla ni kuwa mtu hujilaani yeye mwenyewe ikiwa ataacha sheria za Mungu.

Hivyo watu wamejikuta wakiwaogopa wanadamu wenzao kwa kutoujua ukweli. Unamuogopa mtu aliyezaliwa na mwanamke? Mtu anayehitaji chakula ili apate nguvu ya kuishi. Unakuta mtu anaenda kanisani anaitwa na mchungaji mbele ya kanisa na kutabiriwa vitu vya uongo na yeye anasema kweli wakati sio kweli. Kwa mfano;
Mchungaji: wewe unatatizo la ugumba
muumini: Kweli
Mchungaji: Mama yako anakuloga
Muumini: Kweli
wakati yote ni uongo, anasema kweli kwa uoga na utumwa wa kifikra.

Wito wangu, lazima watu waishi kwa kupendana na kuzishika amri na sheria za Mungu ili wapate kuwa huru na maisha. Vinginevyo tutabaki kuwa watumwa na kuona sisi ni wasindikizaji wakati wengine ndio walioumbiwa huu ulimwengu jambo ambalo si kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom