Mungu kwa nini alimchukua Mke wangu?

Mungu kwa nini alimchukua Mke wangu?

Mke wangu alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita, alifariki kifo kibaya sana maana aliniachia mtoto mchanga wa wiki tatu. Baada ya kuhuzunika sana sikuwa na jinsi, nikamuomba Sister wangu ahamie kwangu ili maisha ya pale home yasisimame maana nina mtoto mwingine mkubwa kidogo. Yule mdogo alichukuliwa na Bibi yake.

Sasa sister kanigeuka yaani, amekuwa ni mtu wa kujiachia mno na maisha, bahati mbaya kazi zangu ni za kusafiri safiri sana sasa kila ninaporudi nyumbani ni kukarabati vitu tu maana hakuna usimamizi kabisa, mwanangu huyo mkubwa ni kama anajilea mwenyewe akifanya homework ni sawa asipofanya ni sawa pia! Muda mwingi sister anakuwa kazini na kwenye mishe mishe. Kila nikianzisha kaujenzi fulani pale home au chochote pesa inaishia kwenye castle lite tu sasa hata pesa nayotoa ya kula inaishia kwenye castle lite na viwanja, mtoto anakula 'kinachopatikana'.

Nikapata mwenzangu nikaanza kumshirikisha na maisha yangu, kama kununua chakula na kuwapelekea pale home au kama kuna ka project namtumia pesa awalipe mafundi sasa kumewaka moto! Sister anani mind ile mbaya na anazambaza maneno hasa kwa ndugu na jamaa, wamemchafua mno binti wa watu kuanzia kuambiwa mshirikina na mengineyo ila mimi, baba yangu na baadhi ya ndugu hatuuoni huo ubaya wake, nifanye nini waungwana wa JF? lengo langu ni kumuoa huyu binti na kujaribu kujenga upya familia yangu, hadi sasa sijaona kosa lake na anaonekana kumjali mtoto wangu(?).

Kwanza nakupa pole ya kuondokewa mkeo. Innalillahi wainailayhi rajuun. Mwenyezi Mungu atakufanyia wepesi inshaallah.
Suluhisho la hiyo shida yako ni kupata mwenzio mnayependana, kama hakuna mapenzi ni bora hata uajiri housegerl akutunzie mwanao. Huyo unayesema umepata ni ana mapenzi au anatafutia kwako cheti cha ndoa, kutumbua mali zako na haki ya kurithi? Angalia vizuri.
 
pole kakaangu huyo binti unataka kumuoa umemfaham kwa muda gani manake madada wa mujini nao ni noma na ni waigizaji sana mchunguze vzr
 
inauma mnoooooo kumpoteza mwenzio! kakangu alifiwa na mke hivyo hivyo, bahati nzuri nilikuwa bedrest ya twins, so nikapewa jukumu la kumlea mtoto wake, aliachwa akiwa na miezi minne!! sasa ni binti mkubwa wa miaka 6, yupo grade one! nililea mwenyewe mpaka wakati nakaribia najifungua, dadangu mkubwa akaendelea!

naelewa hali uliyonayo, maana kakangu naye alikuwa kama amedata! ila nilimsupport na wote tulimsuport huwa hasahau, sasa ameoa mke mwingine, ila mtoto tupo naye wenyewe!
 
Duh we kweli unamoyo my fridnd fukuza hupo kunguni mana anakunyonya tu, kama ye mjanja kwanini asiolewe akale vya mumewe hebu asimbania mwenzie. Nawewe ni mwanaume haya yote umeyataka inamana ulishindwa kusoma alama za nyakati mapema? Kalagabaho
 
Lait Noir- Pole sana kwa kufiwa mke tena akaacha mtoto mchanga. Maisha lazima yasonge mbele na watoto wako ni muhimu wakue katika maadili ya familia.

Kwa kuwa umeona umepata rafiki- wewe ni mtu mzima -msome ipasavyo na umueleweshe mategemeo yako kwenye maisha yenu ya baadae. Na kwa kuwa wewe ni kichwa cha familia maamuzi ya kujenga nyumba bora yako mikononi mwako- you got to face your sister and tell the truth. Kama unakwazika na kuzurura na kutokumwangalia mtoto ni vema ukamweleza kwa busara kuwa hupendezwi. Kwani ndio ndugu pekee awezaye kukaa na mtoto?

Pili ndugu yangu -pamoja na kutafuta pesa na maisha hakuna kitu kizuri kama kuwa na muda na mwanao- maisha ya makuzi ya watoto wadogo yanadefine sana atakuwa na tabia gani ukubwani. Tafadhali kama unaweza punguza baadhi ya safari ambazo si lazima- spend that precious time with you kids.
Kuliko ndugu pasua kichwa ni heri uweke housegirl mwaminifu (kumpata sasa ndio issue).

All in all- kama mwanaume ni lazima ufanye maamuzi sahihi kwako na kwa wanao. Na jihakikishe kuwa mchumba wako wa sasa yu tayari kulea wanao. Mama wa kambo wengine ni wazuri sana ili mradi hawana chokochoko za familia ya mume au ya mke wa kwanza. Kuna upotoshaji sana kuwa mama wa kambo si mama- si kweli , nimeona mama wa kambo wengi tu wakilea watoto kwa tunu na mwishoni hao watoto ndio wamekuwa msaada kwenye uzee wake. Make bold decisions bro
 
Kama huyo binti umempenda, muoe fasta ili akae hapo nyumbani na kuweka mambo sawa. Huyo dada yako mrudishe kwa wazazi wake akaendelee kujifunza maisha kwanza.

mie bwana katika vitu ambavyo havinishindagi ndio hivi, siwezi kukosa amani kisa mtu mmoja ananizingua na ninammudu, huwa sijali lawama ninapoona nina haki ya kuwa na amani, tena huyo ndugu wa damu mbona aesy, watu tuliwapumzisha mawifi mpaka kikaeleweka, sema mleta thread kanigusa kweli, kasema kwa hisia sana, pole ndugu yangu.
 
mtu mzima, anafanya kazi, si alikua hapo kwaajili ya kutunza watoto na sasa umepata mwenza, hakuna sababu ya yeye kuendelea kukaa hapo, follow your heart mpendwa.
 
mie bwana katika vitu ambavyo havinishindagi ndio hivi, siwezi kukosa amani kisa mtu mmoja ananizingua na ninammudu, huwa sijali lawama ninapoona nina haki ya kuwa na amani, tena huyo ndugu wa damu mbona aesy, watu tuliwapumzisha mawifi mpaka kikaeleweka, sema mleta thread kanigusa kweli, kasema kwa hisia sana, pole ndugu yangu.

Asante sana Nyamayao
 
Duh we kweli unamoyo my fridnd fukuza hupo kunguni mana anakunyonya tu, kama ye mjanja kwanini asiolewe akale vya mumewe hebu asimbania mwenzie. Nawewe ni mwanaume haya yote umeyataka inamana ulishindwa kusoma alama za nyakati mapema? Kalagabaho

kuna kusoma alama za nyakati mkuu ukifiwa, na hapo hapo umeachiwa mtoto wa wiki 2?
 
Fukuza huyo ndugu yako manake anaonekana wala hana huruma....... Pole kwa kumpoteza mkeo....... Kazi ya mungu haina makosa ndugu yangu
 
Lait noir, bet strong and follow your heart. Ulsmlaumu Mungu kwa kummchukua mke wako, he has a great plan for each of us. Naamini wanao wote watakua kwa nguvu zake Mungu. Shukuru at least they have you, kuna ambao hawana baba wala mama. Kama wewe hujaona ubaya wa huyo rafiki yako basi endelea nae tu, tena kwa kumpa nguvu zaidi muoe kabisa maana unaweza kuta hata marhem mke wako walimsema pia ni mbaya, au ni mshirikina.
In any case if you need hepl please reach me through PM. Pamoja sana
 
Last edited by a moderator:

Aksante sana Roulette, nitakuandikia vikinifika zaidi
 
Nilivyoona heading, nikakufikiria. Wewe ulisaidiwa na nani?

Hahaaaa eti ulikumbuka? Weweeeeeee....., My mum.... mama yangu alinisaidia sana na anaendelea kunisaidia mpaka sasa. Bila yeye sijui my malaika angekua wapi. Sina dada sijaoa tena, its tough ila mama yangu yupo upande wangu.
 
Bahati yako mkuu mama yupo, mimi mama nae alishatangulia mbele za haki, huwa nawaza sana kama agekuwepo yaani. Infact nimepata uchungu mpya kabisa wa kufiwa na mama kipindi wife kafariki
 
pole sana kaka kwa kufiwa na mke, siku zote wewe ndo kiongozi wa maisha yako na wewe ndie utayafanya maisha yako yawe mabaya au mazuri. hakuna mtu anaeweza kubalisha maisha yako ivo basi kama mwanaume fanya maamuzi magumu, ondoa dada yako hapo nyumbani tena mwambie akitaka kuja hapo anakutaarifu.
 
Back
Top Bottom