Mungu kwa nini alimchukua Mke wangu?

Mungu kwa nini alimchukua Mke wangu?

Lait noir

Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
96
Reaction score
49
Mke wangu alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita, alifariki kifo kibaya sana maana aliniachia mtoto mchanga wa wiki tatu. Baada ya kuhuzunika sana sikuwa na jinsi, nikamuomba Sister wangu ahamie kwangu ili maisha ya pale home yasisimame maana nina mtoto mwingine mkubwa kidogo. Yule mdogo alichukuliwa na Bibi yake.

Sasa sister kanigeuka yaani, amekuwa ni mtu wa kujiachia mno na maisha, bahati mbaya kazi zangu ni za kusafiri safiri sana sasa kila ninaporudi nyumbani ni kukarabati vitu tu maana hakuna usimamizi kabisa, mwanangu huyo mkubwa ni kama anajilea mwenyewe akifanya homework ni sawa asipofanya ni sawa pia! Muda mwingi sister anakuwa kazini na kwenye mishe mishe. Kila nikianzisha kaujenzi fulani pale home au chochote pesa inaishia kwenye castle lite tu sasa hata pesa nayotoa ya kula inaishia kwenye castle lite na viwanja, mtoto anakula 'kinachopatikana'.

Nikapata mwenzangu nikaanza kumshirikisha na maisha yangu, kama kununua chakula na kuwapelekea pale home au kama kuna ka project namtumia pesa awalipe mafundi sasa kumewaka moto! Sister anani mind ile mbaya na anazambaza maneno hasa kwa ndugu na jamaa, wamemchafua mno binti wa watu kuanzia kuambiwa mshirikina na mengineyo ila mimi, baba yangu na baadhi ya ndugu hatuuoni huo ubaya wake, nifanye nini waungwana wa JF? lengo langu ni kumuoa huyu binti na kujaribu kujenga upya familia yangu, hadi sasa sijaona kosa lake na anaonekana kumjali mtoto wangu(?).
 
Endelea kupambana tu; hakuna haja ya kumlaumu Mungu katika hili. Wewe si wa kwanza kufiwa.
 
fukuza huyo dada yako bora lawama kuliko kuishi na majonzi moyoni
bora aumie mtu mmoja kuliko roho 100 zipotee
pole sana kwa kupoteza mke jamani... ila sio vizuri kumtuma huyo mchumba wako kwa sasa tafuta ndugu mwingine akusaidie hadi muoane
 
Niliwahi kumtumia kaka yangu mkubwa hali ndio ikawa balaa, kazi ya milioni 2 ilifanywa kwa milioni 8 na nusu na haikuisha hadi leo!
 
Pole sana kaka,chukulia yote kama mitihani ya mwenyezi mungu na inshallah mungu atakupa uhai mrefu uweze kuwalea watoto wako kwa mapenzi na imani ya dini yako,bila kusahau kumuombea dua mzazi mwenzako alie tangulia mbele ya haki..
Kuhusu huyo mdogo wako anaglia sana sababu ndugu wengi hawaelewani na mke ambae hapendi kufuja vitu,huyo mchumba wako angekua mfujaji kama yeye au angekua kamtafuta yeye wangeiva lakini hapo ameshaona kitumbua chake nishaanza kutiwa mchanga ndio mana maneno mengi yatasemwa,chamsing ni wewe kua na mamuzi yakiume,sababu huwezi huwezi kuridhisha wote.
 
Nakusoma kaka.....
 
Lait noir ("maziwa meusi"!?) kwanza pole kwa kuondokewa na mkeo.

Je hakuna namna ya kumwondosha (kistaarabu!) huyo dadako na kuweka mtu/ndugu mwingine kwa muda? Kwa jinsi ulivyosimulia huyo dadako ni hatari maana ameshindwa kutunza nyumba na bado anataka kukuzuia usio mtu unayempenda!
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi kumtumia kaka yangu mkubwa hali ndio ikawa balaa, kazi ya milioni 2 ilifanywa kwa milioni 8 na nusu na haikuisha hadi leo!
basi kwa muda huu ambao una ubavu wako jitahidi kufanya mambo yako mwenyewe. si unajua wanawake hatupendani? yaani kaka amtume mpenzi wake nyumbani kuleta hela home yaani hilo liwivu halibebeki bwana.
kama vp mtume kwa siri siri sana
 
"Bwana(Mungu) ametoa na Bwana ametwaa..."
Hayo ni maneno ambayo pasi na shaka umekuwa ukiyasikia.
Mungu alimchukua mkeo kwa kuwa ndiye aliyemuumba.

Pili, huyo dada yako uliyemwalika nyumbani kwako, kipi kinakushinda kumuondoa??
 
Mke wangu alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita, alifariki kifo kibaya sana maana aliniachia mtoto mchanga wa wiki tatu. Baada ya kuhuzunika sana sikuwa na jinsi, nikamuomba Sister wangu ahamie kwangu ili maisha ya pale home yasisimame maana nina mtoto mwingine mkubwa kidogo. Yule mdogo alichukuliwa na Bibi yake.

Sasa sister kanigeuka yaani, amekuwa ni mtu wa kujiachia mno na maisha, bahati mbaya kazi zangu ni za kusafiri safiri sana sasa kila ninaporudi nyumbani ni kukarabati vitu tu maana hakuna usimamizi kabisa, mwanangu huyo mkubwa ni kama anajilea mwenyewe akifanya homework ni sawa asipofanya ni sawa pia! Muda mwingi sister anakuwa kazini na kwenye mishe mishe. Kila nikianzisha kaujenzi fulani pale home au chochote pesa inaishia kwenye castle lite tu sasa hata pesa nayotoa ya kula inaishia kwenye castle lite na viwanja, mtoto anakula 'kinachopatikana'.

Nikapata mwenzangu nikaanza kumshirikisha na maisha yangu, kama kununua chakula na kuwapelekea pale home au kama kuna ka project namtumia pesa awalipe mafundi sasa kumewaka moto! Sister anani mind ile mbaya na anazambaza maneno hasa kwa ndugu na jamaa, wamemchafua mno binti wa watu kuanzia kuambiwa mshirikina na mengineyo ila mimi, baba yangu na baadhi ya ndugu hatuuoni huo ubaya wake, nifanye nini waungwana wa JF? lengo langu ni kumuoa huyu binti na kujaribu kujenga upya familia yangu, hadi sasa sijaona kosa lake na anaonekana kumjali mtoto wangu(?).
Undugu si kuzaana, undugu ni kufanana. Inaonekana unafanana na huyo binti mwingine na si dada yako. Ondoa haraka huyo dada ambatana na huyo mnayefanana (kimawazo) ili ujenge maisha yako, yake na ya watoto wako
 
"Bwana(Mungu) ametoa na Bwana ametwaa..."
Hayo ni maneno ambayo pasi na shaka umekuwa ukiyasikia.
Mungu alimchukua mkeo kwa kuwa ndiye aliyemuumba.

Pili, huyo dada yako uliyemwalika nyumbani kwako, kipi kinakushinda kumuondoa??

Nikimuondoa kwa sasa nani atabaki na nyumba sasa kiongozi?
 
Kama huyo binti umempenda, muoe fasta ili akae hapo nyumbani na kuweka mambo sawa. Huyo dada yako mrudishe kwa wazazi wake akaendelee kujifunza maisha kwanza.
 
Lait noir ("maziwa meusi"!?) kwanza pole kwa kuondokewa na mkeo.

Je hakuna namna ya kumwondosha (kistaarabu!) huyo dadako na kuweka mtu/ndugu mwingine kwa muda? Kwa jinsi ulivyosimulia huyo dadako ni hatari maana ameshindwa kutunza nyumba na bado anataka kukuzuia usio mtu unayempenda!
ustaarabu wa kumtoa hapo ni kumtafutia mume aolewe tu basi
 
  • Thanks
Reactions: SMU
maamuzi magumu siku zote ndo yanayosaidia nakushauri ifike mahala ufanye uamuzi mgumu kwa manufaa yako. hapo ni kwamba ur looking of whether ur future or ur relatives
 
Kama huyo binti umempenda, muoe fasta ili akae hapo nyumbani na kuweka mambo sawa. Huyo dada yako mrudishe kwa wazazi wake akaendelee kujifunza maisha kwanza.

Du lakini nyie Wanawake mnatutesa humu duniani, ndio maana tunakufa haraka. Si dada wale Mke wote taabu tupu.
 
how old is your sister?dada yako anajua kabisa utakapooa hatapata mwanya tena wakufuja pesa nakupata pesa za bure yaani ile loop itakuwa totaly closed ndio sababu anafanya hivyo na anaweza ishi hapo kwako mpaka akazeekea hapo asiolewe ninavyowafahamu wanawake.na ukaoa akiwepo hapo nyumbani hao bata wawili mke mpya na dada yako watakupasua huo ubongo vipande vipande ,naongea kw uzoefu ni heri kufuga mabata 20 kuliko hao wanawake wawili,lakufnya ni kuwa huyo dada yako aondoke hapo nyumbani nakujitegemea mwongeze mtaji asonge mbele wewe sio mumewe.oa mke ila i worn yo kuwa kribu sana na mtoto wako muulize maswali kuhusu maisha yaani kuwa mre than father pindi utakapooa awe rafiki yako wa karibu,awe anakueleza yote anayofanyiwa na yanayojiri ukiwa haupo hapo.mwisho :kazana sana wanao wapate elimu bora watakufuta machozi baadae.
 
Back
Top Bottom