Ni ukweli ulio wazi ila ni ngumu kukubalika hasa kwa watu waliokaririshwa imani.
Iko hivi Mungu angekuwa anaijua kesho yako kusingekuwepo na kitu kinachoitwa dhambi, kwa sababu, mfano mtu amechinjwa hapo hakuna dhambi maana tayari mungu alishapanga utachinjwa au huo uovu unaoufanya sasa ungekuwa sio dhambi maana mungu alishapanga.
Njia unayoipitia ndiyo hatima ya maisha yako.
Kuna watu wanamtumikia Mungu mpaka wanazeeka na pia wapo wanamtumikia shetani mpaka wanazeeka.
Pia wapo walikuwa wanamtumikia Mungu ila hawajauona hata ujana.
Maisha ni kama simu tu utachagua uitumieje vile unaitumia ndiyo inakupa majibu unayoyataka wewe.