Mungu haijui kesho yako

Mungu haijui kesho yako

Acheni upumbavu, mbona hukanyagi moto ukuunguze mguu ilihali uwezo wa kuukanyaga unao?

Au mbona hujipeleki huko vitani Ukraine ukafe nakati uwezo wa kwenda unao?

Au kwanini hujilazi kwenye reli ili treni ikija ipite nawe ufe nakati una uwezo huo?
Hayo unayoyasema ni kusababisha maumivu na si kuepusha maumivu, ulipaswa kuniambia kwanini nisizuie mauaji huko Ukraine endapo uwezo ninano? Hio ingemake sense, ila sasa , mimi sina huo uwezo, ningekuwa nao na badi nikaacha watu wauwawe Ukraine hapo nitakuwa ‘Sadist’
 
Hapa wachague moja kati ya haya mawili

1.) Mungu kama anaijua kesho yetu maana yake ameshapanga kesho yetu, hivyo dhambi zote mtuhumiwa namba 1 ni yeye.

2.) Kama dhambi ni zetu, maana yake yeye hakupanga sisi tufanye dhambi bali ni uamuzi wetu sisi wenyewe, hivyo haijui kesho yetu.

Chagueni moja hapo
Boss Usilazimishe.

1.) Wewe kujua kuwa ukiharibikiwa na tumbo utachafuka iwapo hutaenda maliwatoni inamaanisha kuwa ulipanga uharibikiwe na tumbo? (MUNGU KUIJUA KESHO YAKO HAIMAANISHI KUWA AMEIPANGA)

2.) Kama hukupanga kuharibikiwa na tumbo ukifanya uamuzi wa kwenda maliwatoni haimaanishi kwamba ulijua kuwa ukienda maliwatoni tatizo litakwisha? (MUNGU KUTOKUIPANGA KESHO YAKO HAIMAANISHI KUWA HAIFAHAMU KESHO YAKO)
 
Hilo gari limeundwa ni mashine halina utambuzi, nimelitumia tu kama mfano uone katika kipengele cha kufahamu jambo kutokana na sifa za hilo jambo. Sifa za cc kubwa ni kula mafuta sijaongelea uhusika wa uumbaji wake.

Binadamu ana uhuru wa kuchagua ila chaguzi zina maandalizi. MUNGU anayaona maandalizi ndipo anajua utakachokifanya.
Sasa kama binadanu anakuwa na uhuru wa kuchagua basi huwezi kusema mungu anajua mwisho wake utakuaje sababu huo sio uhuru, tayari mwisho upo pre determined
 
Sasa kama binadanu anakuwa na uhuru wa kuchagua basi huwezi kusema mungu anajua mwisho wake utakuaje sababu huo sio uhuru, tayari mwisho upo pre determined
Kwann unalinganisha kufahamu mwisho na kuupanga mwisho? Mwisho wa filamu uliyoitazama unaufahamu sababu uliupanga?
 
Kwann unalinganisha kufahamu mwisho na kuupanga mwisho? Mwisho wa filamu uliyoitazama unaufahamu sababu uliupanga?
Sasa filamu kama hukushiriki kuiandaa wewe utajuaje mwisho wake upoje? Ama Ulishainagalia hiyo filamu kabla hadi ikafika mwisho? Au uliambiwa na mtu mwingine aliyekwisha iona?
 
Lengo ni hitimisho la maisha yako ya umilele, Mungu hana hasara hata ukipotea,maana ana viumbe wengine mamilioni kwenye sayari zingine wasio na dhambi, anakupa muongozo kwa faida yako Ili uishi vyema hapa duniani na kesho ahera.
Ameeeeeeeeen
 
Sasa filamu kama hukushiriki kuiandaa wewe utajuaje mwisho wake upoje? Ama Ulishainagalia hiyo filamu kabla hadi ikafika mwisho? Au uliambiwa na mtu mwingine aliyekwisha iona?
Ndo maana nakwambia hakuna tendo lisilo na maandalizi, MUNGU anaangalia maandalizi ya matendo unayotaka kuyafanya kabla hujayafanya anajua huyu anaenda kufanya nn.

Ni sawa na wewe unavyoangalia igizo ambalo uliona maandalizi yake. Sasa yeye kufahamu utakalolifanya haimaanishi kapanga ufanye.
 
Ndo maana nakwambia hakuna tendo liailo na maandalizi, MUNGU anaangalia maandalizi ya matendo unayotaka kuyafanya kabla hujayafanya anajua huyu anaenda kufanya nn.

Ni sawa na wewe unavyoangalia igizo ambalo uliona maandalizi yake. Sasa yeye kufahamu utakalolifanya haimaanishi kapanga ufanye.
So kwa hiyo mpaka mungu aone maandalizi ninayoyafanya ndio atajua nitaenda kufanya nini sio?
 
So kwa hiyo mpaka mungu aone maandalizi ninayoyafanya ndio atajua nitaenda kufanya nini sio?
Yap. Na huwezi kutenda lolote bila maandalizi. Hakuna chochote utaweza kufanya bila maandalizi. Kuanzia seli zinazounda DNA yako mpaka ubongo kupata maelekezo na mwili kufanya maamuzi ni zoezi ambalo MUNGU ana uwezo wa kuliona tangu mwanzo kule kwenye chumba cha siri kabisa cha kiini cha nuclear zako.
 
Yap. Na huwezi kutenda lolote bila maandalizi. Hakuna chochote utaweza kufanya bila maandalizi. Kuanzia seli zinazounda DNA yako mpaka ubongo kupata maelekezo na mwili kufanya maamuzi ni zoezi ambalo MUNGU ana uwezo wa kuliona tangu mwanzo.
kwa hiyo tuseme hajui future yangu sababu kwenye kufanya hayo maandalizi yeye hahusiki bali ni nutashi wangu
 
Haimake Sense hata kidogoo...!! Maisha ya mwanadamu kila kinachotokea kina sababu na Mungu anajua sio kesho yako tu hata maisha yako yote hapa duniani mwanzo mpaka mwisho...
Kabisa
 
kwa hiyo tuseme hajui future yangu sababu kwenye kufanya hayo maandalizi yeye hahusiki bali ni nutashi wangu
Sasa kujua future yako kunatokana na matendo na matendo yana maandalizi. Tatizo linakuja huwezi kumficha maandalizi ya utakachokifanya. Otherwise ingekuwa ni tofauti tungekuwa maroboti yasiyo na maamuzi.
 
Yeye amejuaje kwamba sisi tutafanya uasi with 100% specifity and certainity kama hakupanga? Na kwakuwa ni miweza wa yote, angeepusha tu all together, au anapenda kuona dhambi ikitendeka? Ana enjoy sio? Ni Sadist?
Mwanadamu umepewa uwezo wa kuishinda dhambi,kiburi chako tu.
Dunia imewekwa kwenye kanuni Ili uishi vyema, maana kuishi ni ibada na kufa ni faida.
 
Hao viumbe wa Sayari nyingine ni kwanini hawana dhambi? Ila sisi tuwe na dhambi?
Sababu wanaishi kwa kufuata Sheria na kanuni za MUNGU.
Ukifata kanuni za MUNGU yaani kuishi Maisha matakatifu ya utauwa huwezi kuwa na dhambi, dhambi zitakukimbia.
 
Sasa kwanini aruhusu mi nizaliwe si angepotezea tu nisiwepo?
Ameruhusu uzaliwe Ili umuabudu,Mungu si dikteta thus amekupa akili ya kujua mema na mabaya yote haya mwanadamu uyatenda kwa kuamua mwenyewe.
So hana hasara bali hasara ni kwa aipotezae roho yake.
 
Ameruhusu uzaliwe Ili umuabudu,Mungu si dikteta thus amekupa akili ya kujua mema na mabaya yote haya mwanadamu uyatenda kwa kuamua mwenyewe.
So hana hasara bali hasara ni kwa aipotezae roho yake.
Yaah free will
 
Sio kweli. Kujua mwisho wako haimaaniishi kuwa alipanga uwe hivyo. Kwani wewe unavyomuona mtu akinywa sumu si unaujua mwisho wake? Inamaanisha kuwa ulipanga anywe hiyo sumu?

Embu Tunga simulizi hapo alafu weka HAO wahusika uone Kama watajipangia wenyewe visa katika hiyo simulizi pasipo ya wewe(mtunzi) kuwapangia.

Mungu ndiye mpangaji WA yote elewa hivyo
 
Embu Tunga simulizi hapo alafu weka HAO wahusika uone Kama watajipangia wenyewe visa katika hiyo simulizi pasipo ya wewe(mtunzi) kuwapangia.

Mungu ndiye mpangaji WA yote elewa hivyo

MUNGU sio mtunzi wa simulizi yako, ni muumbaji wa wahusika, mtunzi wa simulizi ni wewe mwenyewe yeye ana uwezo tu wa kujua unaloenda kutunga kabla hujalitunga kwa kuyatazama maandalizi yako ya utunzi.

Uhuru tulionao ndio unaowezesha wengine kuchagua kuwa hakuna MUNGU. Au MUNGU aliwapangia ili ajipinge uwepo wake?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom