Mungu haijui kesho yako

Mungu haijui kesho yako

hoja dhaifu sana. Kesho ya Kila mtu huwa imepangwa na Mungu mwenyew tena Mungu humwazia mema kila mtu ila dhambi ndio hublock baraka bora za kesho ya mtu na kwakua ibilisi yuko against na mema Mungu anayowatakia watu wake. hutumia mlango wa dhambi kama kichocheo cha kublock baraka hizo kwakushawishi wanadamu kujiingiza huko. hakuna baya au zuri linalo mpata mtu kwa mpango wa mungu lile lisilo bora kwa huyo mtu. elewa sio kila jambo baya linalomtokea mtu Mungu anataka limpate
Inamaana huyo Mungu wenu amemshindwa kabisa huyo ibilisi kiasi wanashindana Kama ccm na chadema
 
Yani hata usipoenda jua ndivyo ilivyopangwaaa 😀 😀 usidhani kwamba ukienda sijui kuna mpango utaubadilisha hapana ndo maana unaweza toka kanisani na still ukagongwa na gari ukafa... haubadilishi kitu ila hivyo ndivyo ilivyoandikwa juu ya maisha yako zaidi ukienda Kanisani unatengeneza maisha yako baada ya kifo.
Unabadilisha Nini wakati kasha panga ukitoka kanisani unaenda kwa mchepuko? Je tunaweza kumshangaza Mungu kwa kutenda Jambo ambalo yeye hakulipanga? Kama jibu Ni ndio Basi hajui Kila kitu na Kama jibu Ni hapana Basi huna utakacho badilisha iwe kwa kwenda kanisani au msikitini
 
kuna tofauti sana kwa anayeleta hoja flani kwa kutaka kuelewa na mwngine kwa kuleta ubishani hawa ni watu tofauti ukweli unauelewa ila unaamua kuleta kubisha



chief ukweli ww unaujua ila unaleta hoja ili kuleta ubishani. kuna tofauti kubwa ya mtu kuleta hoja kwa kutaka kuelewa na kutaka kuleta ubishani

mithali 26:4 " usimjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake usije ukafanana nae, umjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake asije akawa mwenye hekima machoni pake"

hapa inategemea mpumbavu unae deal nae kuna ya kujibu pale anapohitaji kuelewa mtu kuna wa kukaa kimya pale anapohitaji tufanane kwa upumbavu
Tayari umesha tafuta kichaka Cha kujificha
 
Hapana. Ishu ni kwamba anaziona njia zako, matendo yako, maamuzi yako, mfumo wa moyo wako na matamanio yake hivyo yeye kujua kuwa utabadilika au kuacha unachokifanya ni rahisi, huwezi kumfanyia suprice., mwisho wako anaujua.

Ni kama vile wewe unaangalia movie ambayo ulishaiona, unajua kabisa kitakachotokea sio kwa sababu umekifanya kitokee au umepanga ila ni kwa sababu unajua kitatokea sababu una uzoefu wa hiyo filamu.

Sasa MUNGU anaona matamanio ya moyo wako na anajua matokeo ya hayo matamanio siku zote ni nini kitafuata maana matendo ya binadamu ni yale yale tu hakuna jipya ambalo litakuwa suprice.
Sasa Kama alishajua sita mtii kabla hata sijazaliwa kwanini aliruhusu nizaliwe? Sababu Alisha hua sitakua mtiifu kwake kabisa na atanichoma Moto Sasa so angezuia uwezakano wa Mimi kutokuwepo kabisa
 
Sasa kujua future yako kunatokana na matendo na matendo yana maandalizi. Tatizo linakuja huwezi kumficha maandalizi ya utakachokifanya. Otherwise ingekuwa ni tofauti tungekuwa maroboti yasiyo na maamuzi.
Kwa hiyo kabla sijafanya hayo maandalizi, tayari mungu anajua nitafanya maandalizi fulani?
 
Sio kweli. Kujua mwisho wako haimaaniishi kuwa alipanga uwe hivyo. Kwani wewe unavyomuona mtu akinywa sumu si unaujua mwisho wake? Inamaanisha kuwa ulipanga anywe hiyo sumu?
Sasa mbona huyo Mungu wenu mnampa Tena sifa za kibinadam si mnasema Ni muweza wa yote? Kama Mimi nikijua kesho utakunywa sumu nitakupa dawa za usingizi ulale ili hiyo kesho ipite
 
Ameruhusu uzaliwe Ili umuabudu,Mungu si dikteta thus amekupa akili ya kujua mema na mabaya yote haya mwanadamu uyatenda kwa kuamua mwenyewe.
So hana hasara bali hasara ni kwa aipotezae roho yake.
Sasa nabadilishaje wakati yeye amesha panga kabla hata sijazaliwa anajua nitakupa mwizi mzinzi muuwaji na mwisho atanichoma Moto. Na badishaje au naweza kum saprais Mungu
 
Sasa mbona huyo Mungu wenu mnampa Tena sifa za kibinadam si mnasema Ni muweza wa yote? Kama Mimi nikijua kesho utakunywa sumu nitakupa dawa za usingizi ulale ili hiyo kesho ipite
Wa kwako ana sifa zipi?
 
Ni ukweli ulio wazi ila ni ngumu kukubalika hasa kwa watu waliokaririshwa imani.

Iko hivi Mungu angekuwa anaijua kesho yako kusingekuwepo na kitu kinachoitwa dhambi, kwa sababu, mfano mtu amechinjwa hapo hakuna dhambi maana tayari mungu alishapanga utachinjwa au huo uovu unaoufanya sasa ungekuwa sio dhambi maana mungu alishapanga.

Njia unayoipitia ndiyo hatima ya maisha yako.

Kuna watu wanamtumikia Mungu mpaka wanazeeka na pia wapo wanamtumikia shetani mpaka wanazeeka.

Pia wapo walikuwa wanamtumikia Mungu ila hawajauona hata ujana.

Maisha ni kama simu tu utachagua uitumieje vile unaitumia ndiyo inakupa majibu unayoyataka wewe.
Title yako tu inaonesha usivyomjua Mungu. Ni bora ungekiri kuwa Mungu hayupo kuliko kukirinuwspo wake kisha ukamshusha uwezo wake!! Mungu anajua yaliyopita, yaliyopo na yajayo (Omniscient). Utambuzi wa Mungu hauna mipaka!
 
Sasa nabadilishaje wakati yeye amesha panga kabla hata sijazaliwa anajua nitakupa mwizi mzinzi muuwaji na mwisho atanichoma Moto. Na badishaje au naweza kum saprais Mungu
Umepewa akili ya ujuzi wa mema na mabaya.Hakuna atendae dhambi pasipo kukusudua hata kwa mujibu wa sheria za asili kabla ya ujio wa dini,mema na mabaya yanatenganika.
 
Hakuna watu ambao sitakuja kukaa kuungana nao mkono kama Waumini wa dhana na Fatalism, yani kwa mfano yule jamaa aliyefia kwenye kifua cha yule Malaya kule Malawi ni Mungu alitaka iwe hivyo?

Mtu anakwambia Mungu alimuandaa huyo awe funzo kwa waumini wake, sasa kama ni hivyo, kuna haja gani ya kumtoa mwanawe wa pekee afe kwa ajili ya wa dhambi. People don't even think, hawajui kama Mungu si dikteta na alituumba kwa mfano wake, na mtoto wa nyoka hawi jongoo.
 
So hii inamaanisha yeye atakuwa anajua ?
Inamaanisha kuwa kitu dhaifu hakiwezi chambua kitu kisicho dhaifu na kuvumbua madhaifu ya kisicho dhaifu.

Mfano: unadhani wale mende chumbani kwako wanaweza kukaa na kujadili uwezo wako?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom