Ni ukweli ulio wazi ila ni ngumu kukubalika hasa kwa watu waliokaririshwa imani.
Iko hivi Mungu angekuwa anaijua kesho yako kusingekuwepo na kitu kinachoitwa dhambi, kwa sababu, mfano mtu amechinjwa hapo hakuna dhambi maana tayari mungu alishapanga utachinjwa au huo uovu unaoufanya sasa ungekuwa sio dhambi maana mungu alishapanga.
Njia unayoipitia ndiyo hatima ya maisha yako.
Kuna watu wanamtumikia Mungu mpaka wanazeeka na pia wapo wanamtumikia shetani mpaka wanazeeka.
Pia wapo walikuwa wanamtumikia Mungu ila hawajauona hata ujana.
Maisha ni kama simu tu utachagua uitumieje vile unaitumia ndiyo inakupa majibu unayoyataka wewe.
Hoja yako inaonyesha unataka ku-escape responsibilities zako na kumshutumu muumba wako. Alikupa akili na utashi vya kazi gani kama jukumu la kukuziwia wewe usifanye dhambi ni lake? Aliumba mwanadamu timamu mwenye kujua mema na mabaya na sio roboti wa kuongozwa kwa vibatani na vitufe. Mipango ya maisha yako ni wajibu wako, Mungu anahusika kwenye kuifanikisha mipango yako pale tu atakapoamua kumtafuta kwa moyo wako wote, akili zako zote na nguvu zako zote, ndivyo alivyoagiza tumtafute kwa namna hiyo. Mungu anafanya kazi pamoja na wampendao coz hao ndo watendao mapenz yake.
Mithali 16:9
"Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake."
Proverbs 16:9
"A man's mind plans his way, but the Lord directs his steps and makes them sure."
Hivyo, mwenendo mbaya wa maisha yako ni matokeo ya matumizi ya mabaya ya akili ulzopewa, umeamua kuishi bora liende na madhara yanakupata sababu ya maamuzi na matendo yako, afu unataka Mungu awajibishwe, kweliiiiiii?
Mungu anaijua kesho yako coz anajua matokeo ya njia yoyote utakayoamua kuipita, Mungu ni wa utaratibu na kanuni na kila taratibu na kanuni zina matokeo yake.
Kumbukumbu la torati 11:26-28
26 Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana;
27 baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo;
28 na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
Ata ivo Mungu alipomuumba mwanadamu alimuweka duniani ili aitawale, hivyo tangu hapo Mungu hajiamuli mambo hovyo hovyo pasipo kushirikiana na mwanadamu.
Kasome stori ya Sodoma na Gomora, Mungu alimshirikisha Ibrahimu na wakabageini kimtindo ili Mungu asiangamize miji ile. Kipindi cha gharika, Nuhu alimshirikisha Nuhu.
Note: Kujua tabia ya Mungu na kwa nini anaruhusu maovu kuendelea kutokea, inabidi ukae karibu sana na NENO lake ujifunze kwa makini, yena ukiwa open minded.
Kwa kuhitimisha.
Mungu aliweka utaratibu wa maisha ambao mwanadamu anapaswa kuishi kwa kuufuata na alikua na matarajio ya sisi kuishi kwa utaratibu huo, LAKINI sisi ndio tumeasi na kumtenda dhambi Mungu, na tumeamua kuzifuata njia zetu wenyewe ambazo ni za mauti na majuto na maumivu.
Mithali 14:12
"Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti."
Kwa hiyo kutenda kwako dhambi ni UTASHI wako na kiburi chako na ujeuri wako wa kutotii maagizo ya Mungu. Iko wazi kabisa mshahara wa dhambi ni mauti.
Haya mabaya na maovu yanayoendelea na matokeo ya utashi wetu na matumizi ya akili zetu, na ubinafsi uliotujaa. Tumeamua kumtii shetani na haya ndo malipo yetu, bali kama tungeamua kumtii Mungu stori ingekua nyngne kabsa, coz nia ya Mungu kwa wanadamu inajulikana na nia ya shetani vivyo hivyo! Naomba kuwasilisha.