Mungu anatenda kwa njia za ajabu

Mungu anatenda kwa njia za ajabu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,437
Hii habari nimeelezwa na mama ninaefanya nae kazi. Huyu mama ni mpiganaji haswa wa maisha. Mume alimuacha na kuoa spring chicken. Sasa nyumbani yeye ndiyo baba na mama.

Alipata safari ya kwenda Afrika y Kusini ki kazi kwa wiki mbili. Pesa aliyopewa kazini haikutosha kuwaachia nyumbani. Na mama yake ambae ni kikongwe amehamia kwake.

Mama alisali sana kwa wiki moja na kumkabidhi Mungu hili tatizo. Wakati anajiandaa na safari alitafuta koti la baridi. Alipita mtumbani akanunua koti, amefika nyumbani alianza kusoma maelekezo ya ufuaji wa koti lile. Alikuta $500 kwenye mfuko wa koti.

Alipiga magoti na kumshukuru Mungu kwa utendaji wake. Msiende kumaliza makoti ya mitumba nimeileta habari hii ili kama ushuhuda wa miitikio ya Mungu katika shida zenu.
 
$500 kwenye nguo ya mtumba? Unbelievable, yaani noti tano za $100? Hongera zake. Ila bwana, Kwa nini usifikiri ni bahati yake na sio Mungu?
 
Mungu huwa anakupa kitachokusaidia hasa tatitzo likiwa lishakufika ama linakuja, mfano, unaweza kuwa na tatizo ambalo lahitaji laki 5, mpaka siku ya tukio ikawa huna hata mbuni, ajabu iko hapa, utapata pesa ki ajabu ajabu japo kwa machozi jasho na damu kwa kuungaunga utapata tuu, tatizo litaisha na pesa zesha zoote, sasaukiwa ni mtu wa kulalamika tuu siku zote, unaweza laumu, nimepata pesa zimeisha zote kwa matatizo, kumbe kuna nguvu flani nyuma yako
 
Imani ni fumbo ukilielewa utamtukuza Mungu usiku na mchana
 
hata ukitoa onyo bado makoti ya mitumba yatamalizwa huko kwa kununuliwa
 
Hii habari nimeelezwa na mama ninaefanya nae kazi. Huyu mama ni mpiganaji haswa wa maisha. Mume alimuacha na kuoa spring chicken. Sasa nyumbani yeye ndiyo baba na mama.

Alipata safari ya kwenda Afrika y Kusini ki kazi kwa wiki mbili. Pesa aliyopewa kazini haikutosha kuwaachia nyumbani. Na mama yake ambae ni kikongwe amehamia kwake.

Mama alisali sana kwa wiki moja na kumkabidhi Mungu hili tatizo. Wakati anajiandaa na safari alitafuta koti la baridi. Alipita mtumbani akanunua koti, amefika nyumbani alianza kusoma maelekezo ya ufuaji wa koti lile. Alikuta $500 kwenye mfuko wa koti.

Alipiga magoti na kumshukuru Mungu kwa utendaji wake. Msiende kumaliza makoti ya mitumba nimeileta habari hii ili kama ushuhuda wa miitikio ya Mungu katika shida zenu.

Kweli ukimtegemea yeye aliye juu hkika atatenda tu.
 
Back
Top Bottom